Maadili ya mtanzania ni yapi-ngono mseto au ndoa moja

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
"Quran 17:32
And do not approach unlawful sexual intercourse. Indeed, it is ever an immorality and is evil as a way.

Leviticus 20:10
"If a man commits adultery with the wife of his neighbor, both the adulterer and the adulteress shall surely be put to death.

Matthew 5:27-30
"You have heard that it was said, ‘You shall not commit adultery.' But I say to you that everyone who looks at a woman with lustful intent has already committed adultery with her in his heart. If your right eye causes you to sin, tear it out and throw it away. For it is better that you lose one of your members than that your whole body be thrown into hell. And if your right hand causes you to sin, cut it off and throw it away. For it is better that you lose one of your members than that your whole body go into hell. "
Kiongozi anatakiwa kuwa kioo cha jamii. Kioo kinaakisi jamii husika kutokana na maadili, tamaduni, taratibu, mila na desturi zinazokubalika kwenye jamii husika.
Tanzania ina mila na desturi mbali mbali kutokana na koo, kabila, dini, desturi na mila. Koo nyingi na tamaduni nyingi Tanzania zinaishi na ndoa zaidi ya moja zinaitwa kienyeji, na hizi ndoa zimerithiwa kutoka tangia zama za kale ambapo mababu zetu waliziasisi. Koo na kabila mbali mbali zimetokana na ndoa zaidi ya umoja. Wazee wa zamani walikuwa wakiishi na wake zao ama wawili watatu au zaidi. Mpaka leo Tanzania Tanzania kuishi na mwanamke zaidi ya mmoja halionekani ni janga au kitu cha ajabu, kwani mila bado zinaruhusu au kuvumilia.

Zilipoingia tamaduni za magharibi na mashariki ya kati yaani dini ukristo na uislamu, mila na desturi zikaanza kusahaulika na kukumbatia tamaduni hizi za kimagharibi na mashariki ya kati. Tamaduni hizi zinakinzana kidogo hasa kwenye maswala ya kuowa na kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.
Nchi kama Marekani ukisikika tu kwa mbali kwamba uliwahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa na ukawa unawania ofisi ya umma hasa kutoka na kura unawakati mgumu sana kushinda. Taifa la marekani kwa miaka mingi limejipambanua kama taifa la kikrustu na kufuata mafundisho kadhaa ya kitabu cha wakristu kama chanzo kikuu cha maadili ya viongozi. Taifa hili linaamini kabisa lazima uheshimu ndoa, usivunje ndoa, na uishi na mke mmoja tu ili uonekane mfano kwenye mila, desturi na makubaliano ya kimaadili ya kimarekani.

Hili swala la maadili ya kingoni linasumbua sana watanzania. Tunaposema kiongozi haruhusiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja tukubaliene wote kuwa tunaamua kutumia biblia kama chanzo kikuu cha maadili ya nchi yetu, na kusahau Quran, na dini nyingine ambazo zinakubali ndoa zaidi ya moja au mila na desturi zetu ambazo zinakubali mitala na ndoa mseto.

Maadili ya kibunge na kiserikali lazima yawe wazi kiongozi gani na matendo gani ni uchafu kwenye jamii. Je wote wenye ndoa halali zaidi ya moja kutokana na dini, mila na tamaduni zao bila kuvunja sheria za nchi ni wahalifu? Tuwe makini sana tunapoanza kutumia upande mmoja kujadili maadili. Nchini Mareakani wasio wakristu walianza kujiuliza je sisi nafasi yetu ikoje kama kila sehemu maadili ya kikrustu? Inategemea ni dini gani ila kila dhehebu na dini inathamini sana kitabu chake kitakatifu na kumjaji kila mtu kutokana na mafundisho ya kitabu chao.
Wakristu wanalaani sana ndoa msetu, ngono kabla ya ndoa, na kuzalisha hovyo mitaani. Wanaona kila aliyefanya hivyo hafai katika ufalme wa mungu na sio kioo cha kikrustu, Waislamu wanaamini kunasababu ambazo unaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja ila lazima utimize masharti ya kidini na wanaamini ngono nje ya ndoa ni dhambi na unakiuka maadili na mafundisho ya kiislamu. Wanaoamini kwenye mila na desturi hakuna sehemu ya kisheria kusema sasa ni ndoa bali ni makubaliano tu ya hiari kati msichana na mvulana kuishi pamoja na inaweza kuwa ni kati mume na wanawake kadhaa, hii haihitaji cheti, shahidi, wala umati wa watu kushuhudia. Wapagani wao hawana kipingamizi chochote wanaishi wanavyoona inafaa isipokuwa lazima makundi yote yafuate sheria za nchi.

Leo mijadala ikiwa imejikita zaidi kwenye ngono, nani kalala na nani na wapi kwa nini, inatupasa kufikiri na kutafakari. Sheria za nchi zinakataza kabisa kubaka, kudhalilisha, na nrushwa za ngono. Kutembea na watoto chini ya umri wa miaka 18, au kutumia madaraka vibaya. Ila haisemi kabisa kuhusu watu wazima wanaokubaliana kujamiina.
Jamii ya kitanzania haioni ngono kama ni fedheha au jambo la ajabu, leo ukitembea mitaani nyumba ndogo, bustani, wake wawili au wanne wameshamiri na ni kawaida na kuonekana ndio maadili na mfumo wa kidesturi wa mtanzania.
Wasichana wengi wapo sokoni ama kwa kupenda , ama shida au ukosefu wa mtu wamtakaye kuwa mmoja au sababu yeyote ile. Maofisini ni kuchafu sana ukianzia ikulu mpaka ofisi ya kijiji. Je ni dhambi, ni kuvunja sheria za nchi, ukosefu wa maadili inategemea wewe upo kundi gani.

Ukiangalia wabunge tangia enzi zile za bunge la chama kimoja, wapo wabunge wengi kina mama wamezaa na wabunge zaidi mmoja wengie walikuwa maspika, mawaziri, maraisi nk. Tukianza kutaja watoto mazao ya ngono ya kibunge hapatakalika Tanzania. Ukiingia misikini, makanisani, mashuleni utabakia unajiuliza huku ni sehemu ya maadili ya kiroho au kiwanda cha ngono.

Maadili maana yake ni nini na nani anatakiwa ayasimamia. Chanzo cha maadili ni nani na wapi.
Bill Clinton alipofumaniwa ikulu pamoja na maadili ya kimarekani kuwa hili ni kosa kubwa sana, wananchi walipima manufaa ya Bill na ngona ya hiaria walitenda yeye na yule binti. Wakaona hakuna madhara kwa uongozi wake ijapokuwa aliichafua ikulu.

Mimi binafsi naalani sana kumdhalilisha mwanamke, kubaka au tendo lolote la kingono dhidi ya mtoto. Kuhusu ngono za makubaliano inategemea imani za kidini, mila desturi na mtanzamo wa mtu binafsi.
Kama Taifa tujadili ni nini maadili ya nchi kwenye swala la ngono mseto. Je ni dhambi, haifai, mwenye ngono mseto haruhusiwi kuwa kiongozi ili tuanze kuwawinda na kumchomoa mmoja baada ya mwingine au tuibadili nchi itumie biblia kudhibiti ngono na nyumba ndogo? Au tutumie quran kuhalialisha ndoa halali zaidi ya moja kwa mujibu wa kitabu baada ya kufuata masharti au tutumia mila zetu za ndoa mseto na ngono mvurugano?
Chief Mkwawa
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
13,922
2,000
Hivi yule anayeitwa mtume aliyeoa kabinti na miaka16 na aliyeruhusu kulala na vivulana vidogo anaitwa nani? Nadhani hiyo ndo anafaa kumfuata.
 

alfazulu

JF-Expert Member
May 6, 2012
734
0
sisi na watznia, waafrka, wabantu...tamaduni zetu ndizo zinatu~define sisi. bnafs nimemkuta babu yangu akiwa hai..alikuwa na familia tatu tofauti...mila zetu ziliruhusu. ukristu na uislamu haikuwa mila yetu, tulivipokea tu nadhani bila hata kufahamu nikwanamna gani vitaadhiri au vitaoana na mila na maadili yetu ya kiafrika/ktanzania. nandio maana watuwakajikuta wanachagua ukrstu/uislam huku wakiendelea kupractice baadhi ya vpngele vya mila zao. wamarekani wanamila zao ambazo nitofauti sana na zetu kiasi kwamba waliona kma mila zetu nizakishetani. kujaribu kulinganisha moja kwamoja umarekani na utanzania nadhani sii vyma sana. ila nakubali kuwa umefika wakati ambapo mila ziwe adopted to the time..yani ziwe updated sio mila zetu ziwe za kimarekani..sisi sii wamarkani..tuanzie ktka mifmo ya elimu mashuleni na habari..watu waelimshwe mila zote potofu ziwe updated...wanahabari nao wanacheksha..ukiskia wanaonglea kuhsu mila potofu utajuatu wanazngumzia ukketaj na uonevu kw knamama na watoto..nothn more or less...
 

Me370

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
991
0
Tanzania haina maadili tena siku hizi, imebaki story.
Kizazi chetu sijui tayari kimesha laaniwa? Mungu atunusuru tu na janga hili.
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,679
2,000
Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kutokutunza/kwenda accordingly na mila za mababu zetu. Tumekalia kubishana kuhusu dini za wazungu na waarabu tu
 
Top Bottom