Maadhimisho Ya Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maadhimisho Ya Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani 2012

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by AMEND, Sep 14, 2012.

 1. AMEND

  AMEND Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yataadhimishwa rasmi mkoani Iringa kuanzia tarehe 17 hadi 22 Septemba. Kauri mbiu ni "Pambana Na Ajali Za Barabarani Zingatia Sheria". Mkoani Dar es Salaam uzinduzi utafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia sa mbili asubuhi.

  Ajali na usalama barabarani ni masuala yaliyosahaulika sana nchini kwetu Tanzania na bado ni changamoto kubwa kwa Watanzania kijamii na kiuchumi. Zaidi ya 3.4% ya pato la Taifa Tanzania linapotea kila mwaka kutokana na ajali za barabarani. 75% ya ajali husababishwa na kutowajibika kwa madereva wawapo barabarani (The Guardian; 'ItÂ’s time for Sumatra and traffic police to act' - IPP Media, 2011). Mbaya zaidi ya yote, hali inazidi kuwa mbaya, kila mwaka. Karibu kila siku tunasoma, tunasikia na kuangalia habari kuhusu VVU / UKIMWI na Malaria kutoka vyombo mbalimbali vya habari, lakini mara ni mara ngapi umma wa Watanzania unasikia kuhusu usalama barabarani na athari za kijamii na kiuchumi zinayosababishwa na ajali za barabarani? Ajali za barabarani ni janga kubwa duniani kote. Ni wakati sasa tushirikiane sote kubadili hali hii na si kusubiri mara moja kila mwaka ili kufanikisha hili.
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,105
  Likes Received: 10,459
  Trophy Points: 280
  Hii mambo si inahusika na polisccm?....ptuuuuuuu!!! go to hell polisccm.
   
 3. N

  Nguto JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Waandishi wa Dar hawajasusia kuripoti habari za jeshi la polisi na wizara yake hadi kieleweke? Hata hapa jamvini tungeacha kuandika mambo ya polisi.
   
Loading...