Maadhimisho ya Mwaka Mmoja ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuwa madarakani

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
Kutoka Oysterbay, Dar:

Mkuu wa Mkoa, Ndg. Paul Makonda yupo mbashara, katika maadhimisho ya Mwaka Mmoja tangu awe Mkuu wa Mkoa.

Fuatana nasi:


au



======​

Sirro: Langu ni moja tu, kazi hii ni kubwa. Watu waendelee kutoa taarifa. Nina jambo moja tu kwa viongozi. Mkoa wa Pwani viongozi wengi wanauawa. Tuna changamoto Tanga na hata Mwanza.

Kuna mazoezi ya Judo na Kareti kwenye makanisa, kwenye misikiti, kwenye nyumba za ibada kwa ujumla, tutunze sana waumini wetu. Sisi tuna mipaka lakini huwa tunatuma vijana wetu, tunawaweka watoto kwenye mazingira mabovu, Asnteni kwa kunisikiliza.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar: Sasa RC Makonda umekomaa, haiwezekani kila anayekuchokoza ukamjibu.

Tuwatazame mateja kama ndugu zetu, tusiwaue wala kuwachoma moto wafanyapo uhalifu bali tuwape msaada wanaoutaka.

TID: Ningependa niwe mfano wa mambo mema yanayofanyika mkoa wa DSM na Tanzania nzima

Baadhi ya wasanii wanaona njia niliyoichagua siyo sawa, sidhani kama ni wakati wa kukataa ukweli haiitaji hata kwenda chama kingine

Sidhani kama kuna chama kinaweza kukubali msanii mwanamuziki anayetumia dawa za kulevya awepo kwenye chama chao

Haihitaji uwe mwanasiasa ili kukemea matumizi ya dawa za kulevya, hii inahitaji uwe mtanzania kwanza kwa sababu ili ni janga ni la taifa

Diamond Platinumz: Namshukuru Mungu kupata mwaliko huu. Nampongeza RC Makonda kwa kazi nzuri pamoja na changamoto anazokumbana nazo

Ukiwa unatumia #DawaZaKulevya unapungukiwa na ubunifu na unapoteza hata heshima katika jamii inayokuzunguka.

RC Makonda: Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.

Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!

Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidie #JFLeo

Mwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.

Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.

Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosi

Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wangu

Tumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramu

Hatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunacheka

Kupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande


Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lake

Tutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedha

Kipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kidete

Changamoto mojawapo niliyokutana nayo ni MUDA! Muda hautoshi, nahitaji hata miaka kadhaa ili kumsikiliza kila mwananchi

Changamoto nyingine ni mazoea ya Watendaji wa Serikali ktk kutoa huduma. "Njoo kesho" imekuwa kero kwangu na kwa wananchi

Kuzungushwa kwa wananchi kunapelekea changamoto katika za Serikali za Mitaa kuletwa ofisini kwangu. Hili nalo ni tatizo!

Nampongeza sana Kamishna Sirro na Awadhi (wa Usalama barabarani) kwa kusimamia ulinzi na usalama jijini Dar

Milio ya risasi ilikuwa kawaida Dar, watu waliogopa hata kwenda Mlimani City kwa hofu ya kuporwa. Tumeyakomesha yote hayo

Kuna kampuni mbili za ujenzi wa barabara nimezipiga marufuku mkoani kwangu(Dar) kwa kujenga barabara zenye viwango duni

Nilihakikisha Mahakama ya Ardhi ya Kinondoni inatenda haki na kutoa hukumu kwa wakati. Sasa wanafanya kazi hadi Jumamosi

Mtu anataka nikae kimya wakati wananchi wangu Dar wanateseka kwa matumizi ya #DawazaKulevya... Nauliza "Wewe ni NANI?"

Tunapambana kupigania ndoto za vijana na matumaini ya wazazi wao. Haijalishi tumechelewa kiasi gani lakini hatutoacha!

Wapiga dili wa Bandarini jijini Dar wamekuwa wakisumbua kwa fedha zisizo halali na kuwasumbua wafanyabiashara halali

Sibabaishwi na watu wanaonichukia wakati nikitekeleza majukumu niliyopangiwa na Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa.

Bureau de Change zinatumika kufichia pesa haramu. Wiki ijayo moto utawaka, lazima tushughulikie maficho haya.

Sasa foleni jijini Dar imepunguzwa kwa kiwango kikubwa na askari. Ukifurahishwa na trafiki toa shukrani zako, tuwape moyo.

Mwaka huu wa pili tutakazia sana kwenye utumishi. Nitaanzia kwenye Serikali za Mitaa nione jinsi wanavyowasaidia wananchi.

Nataka mwananchi apate majibu kamili aendapo Ofisi ya Umma. Kama hawawezi kumsaidia waende wao ofisi ya juu sio mwananchi.

Wanaoishi mabondeni jijini Dar na wana hati halali nitawapa viwanja. Watendaji waliotoa hizo hati nitawashughulikia!

Jijini Dar, Uwezo wa umeme tunao, tatizo ni miundombinu ya kuusambaza. Nina imani Prof. Muhongo atatumalizia tatizo hili

Wananchi jijini Dar wasikae maeneo hatarishi. Hatuwachukii bali tunawapenda sana, hayo si maisha mazuri...

Najua wengi wanaoishi mabondeni wamepangishwa na waliolipwa fidia. Huwezi kuwa na akili timamu ukakubali kupanga bondeni

Hivi karibuni nitaelekeza wapi showroom za magari zinatakiwa ziwe jijini Dar. Nataka magari yote yauzwe eneo moja

Ninawashukuru wanasheria wetu 35 wanaotoa msaada na ushauri wa kisheria bure kwa wananchi wa jiji la Dar wasio na uwezo

Tumepewa eneo kubwa la kujenga kambi kwa ajili ya wahanga wa #DawazaKulevya. Hii itatusaidia kufuatilia mienendo yao

Hadi sasa tuna watu 11,854 jijini Dar waliokubali kuacha matumizi ya #DawaZaKulevya kwa hiari. Haya ni mafanikio makubwa

Wengine tukiwaita Kituo cha Polisi wanatumia Colgate na Chumvi ili wasigundulike ktk vipimo. Tuna mbinu mpya za kuwapima

Kuna wanaowatumia watoto wadogo kufanya uhalifu na kabla ya hapo wanawavutisha bangi. Tunawasaka na tutawakamata!

Wazee mlio jijini Dar mkikaa kwenye vijiwe vyenu msiache kutoa mafundisho ya zamani. Yanasaidia kujenga jamii.

Tumefanikiwa kukomesha biashara ya Shisha jijini. Wameungana kupiga kelele, kelele zao zinanitia moyo kuwa nafanya kazi.

Rais Magufuli ameziba mianya ya rushwa kuhakikisha tunarudi kwenye anga na kununua ndege. Je, huyu ni Rais wa kumpinga?Tumenyimwa chai maofisi, posho, safari ambazo tulikuwa tukiota vitambi.

index.jpeg
 
Wana JF Muda Huu Mkuu wa Mkoa P Makonda Yupo Live TBC, sijui kuna nini Kipya,
Ila ukiangalia kwa makini ni Kama kuna kisherehe Fulani hivi, ila kwa Wataalam waliosoma seminari vizuri, kuna kitu unaweza kukigungua ktk hafla hii, we Call Body Language

Yaani kuanzia watangazaji mpaka wahudhuriaji ni Kama wana wasi wasi fulani hivi. Duh, hatari
Wasiwasi wako tu...maana tayari una majibu kichwani na unayalazimisha
 
Nasikia anafanya hafla ya kutimiza mwaka mmoja kama mkuu wa mkoa wa Dar.

Sijui nani kakagharamia maandalizi ya hyo hafla wakati falsafa ya mteuzi wake ni kubana matumizi.

Ila kwa Bashite naona kubana matumizi hakumuhusu kwani anasafiri nje Mara kwa Mara na nadhani atakuwa anatumia tu kodi yetum
 
Mkuu wa mkoa wa Daresalam ahazimisha mwaka mmoja wa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar.Nia ni kueleza mafanikio na Changamoto alizokutana nazo akiwa kama mkuu wa mkoa wa Dar.
Nimatumaini yangu leo atavunja ukimya na kuonyesha vyeti
More updates to come
Source Azam two.
☆TID anaongea kuihasa jamii athari mbali za madawa ya kulevya na kusititiza watu wawaombee waathirika waache matumizi ya madawa ya kulevya. Anasema mtumiaji anapoteza uelekeo.anasema hakuna chama kitakachoruhusu mtumiaji wa madawa ya kulevya kujiunga na chama iwapo kitakua makini( anamponda wema)
☆Daktari anayehusika na madawa anaongea kwa kuelezea magonjwa yatokanayo na madawa ya kulevya. Halafu inaoneka mateja wengi wapo kwenye kikao. Daktari anasema mtu akiwa anatumia madawa ni vyepesi kupata maambukizi ya UKIMWI, ULAIBU, TB, MENO. Uharibifu wa mazingira kubaka uhalifu na hivyo kuliongezea taifa gharama za kuwahudumia
 
Back
Top Bottom