Maadhimisho ya miaka miwili ya awamu ya pili ya uraisi wa J. M. Kikwete

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Ndugu wanajamvi, kama mnavyojua ni takribani miezi miwili imebaki kukamilisha miaka miwili ya awamu ya pili (ya miaka mitano) ya raisi wa JMT, Mh J. M Kikwete.
Kwa maoni yangu ni jambo la busara tukikumbushana mambo makubwa ambayo yametokea katika uongozi wa raisi huyu katika miaka miwili iliyopita. Hii itasaidia kutathmini tunakoenda kwa kuangalia tulikotoka.
Kisiasa, kiuchumi, kijamii na kadhalika, ni mambo gani ungependa kuyaorodhesha ambayo kwako yalikuwa makubwa katika kipindi hiki cha miaka miwili ya awamu ya pili ya Kikwete?

Mi kwa kuanzia tu, nakumbuka mambo yafuatayo
1. Kikwete aliridhia na kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya
2. Kikwete alikubali kw kiasi kikubwa kuwasikiliza na kujumuisha mapendekezo ya CHADEMA katika sheria ya kuandika katiba
3. Serikali ya Kikwete ilichafuliwa kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasio na hatia kule Arusha, Songea, na Morogoro kupitia jeshi la polisi kwa kisingizio cha vurugu za kisiasa, na hivi karibuni kumuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi
4. Kwa mara ya kwanza katika uongozi wake, Kikwete alikumbana na changamoto ya kukataliwa kwa bajeti ya nishati na madini na bunge, hadi ilipofanyiwa marekebisho
5. Kwa shinikizo la wananchi, Kikwete alilazimika kuvunja na kuunda upya baraza la mawaziri.
6. Serikali ya Kikwete ilikumbana na changamoto ya maandamano ya kundi la UAMSHO kule Zanzibar, na kutokea kwa vurugu zilizochochewa na askari.
7. Serikali ya Kikwete ilifanikiwa kuendesha zoezi la sensa, ambalo nalo lilikumbwa na changamoto ya kugomewa na baadhi ya taasisi za kiislamu na makundi mengine ya watu


Naomba tuongeze matukio, katika kuyapa uzito maadhimisho haya.

Pia naomba uchambuzi, je kwa tunavyoona utendaji wa serikali hii, nini kitarajiwe kwa miaka mitatu ijayo?
 
Tukio jingine nililolikumbuka punde ni kutokea kwa mgomo wa madaktari nchi nzima, ambao pamoja na mambo mengine ulipelekea kutekwa, kuteswa na kudhalilishwa kwa Kiongozi wao, Dr Steven Ulimboka
 
huu uzi mzuri sana, namna hii ndio jf inavyotakiwa iwe.
Ktk nayokumbuka,
9. jk amefanikiwa kuanzisha rasmi vitambulisho vya urai zoezi ambalo mchakato wake uianza miaka mingi nadhani tokea awamu ya pili.
10 nchi imeingia katika mgogoro na jirani zetu wa malawi, suala ambalo bado jk na serekali yake wanalishuhulikia.
 
Kumbe JK bado hata hajamaliza miaka miwili ya utawala?
Looh...watanzania tuna kazi kwelikweli!
 
11. Kubwa zaidi JK kaipandisha umashuhuri na umaarufu CHADEMA kwa udhaifu na ulegelege wake wa kutofatilia mambo ya msingi mpaka ikaonekana kama nchi sasa inaongozwa kwa maelekezo na matakwa ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom