Huu umati wa watu unanifanya nitamani nilie,kama ikiwa hawa wote wanaiunga mkono CCM au ni wanachama wa CCM...japo najua hapo kuna watu waliotolewa mikoa mingine hasa ya kanda ya ziwa.Lakini pia,hali hii inauzunisha sana wakuu.Kama watu wanakufa kwasababu ya mgomo wa madaktari uliosababishwa na CCM na watu wake bado kuna watu waniunga mkono CCM? Kama mfumuko wa bei sasa ni 20% bado kuna mtu anaiunga mkono CCM? Kama nchi ina ombwe la uongozi na si ajabu kumsikia Spika akiongea tofauti na Raisi kuna watu bado wanaiunga mkono CCM? siamini.Umati huu wa watu unanifanya nitoe machozi.