Wana JF,
Poleni na majukumu ya Ujenzi wa Taifa na Familia zenu,
Ningependa sana mwenye Hotuba ya Rais wetu aliyoisoma au kuitoa kwenye Sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwa CCM huko CCM Kirumba mjini aka jijini Mwanza, yameshasemwa Mengi sana kuhusu Hotuba yake, Kama; amewaambia Watanzania ni Malofa kwa kushinda kulipwa ujira mdogo na kulaghaiwa na Viongozi, Watanzania waache kuchagua watu wenye tuhuma za Rushwa, Chama kama hakina Idara ya Propaganda hakina nguvu, nimesikia na kusoma kuna mambo aka hoja kama 23 ameongelea.
My take: Nimeshindwa kuamini na kujua lipi la kweli au yote ni uzushi au yote ya kweli, mwenye hotuba tuwekeeni tuusome
Nawakilisha