PreGE2025 Maabara za kuchukua wanafunzi 1000 kujengwa MuCE

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
MAABARA ZA KUCHUKUA WANAFUNZI 1000 KUJENGWA MuCE

Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), inaendelea kuwekeza katika miundombinu mipya katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MuCE).

Ujenzi wa miundombinu hiyo mipya unalenga kuongeza nafasi za udahili wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Miundombinu hiyo ni pamoja na Jengo la Multimedia na jengo la sayansi, ambayo yatahusisha madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na maabara zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 950 hadi 1000 kwa wakati mmoja.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hosteli za wanafunzi zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 152 huku Jengo jipya la maabara za Fizikia litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 240.

Miradi yote ya ujenzi imegharimu takribani shilingi bilioni 14 na Uwekezaji huu utachangia moja kwa moja maendeleo ya kitaaluma na kiuchumi.

haya ndio maendeleo ya watu pamoja na vitu sasa 💪👊
 
Back
Top Bottom