Maabara ya DNA yaniletea bifu zito kitaa.

Maabara ya DNA yaniletea bifu zito kitaa.

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,643
Reaction score
4,184
Wakuu,

Nina rafiki yangu yupo Hongkong,
Katika mazungumzo yetu ya hapa na pale mwanzoni mwa mwaka nilimpa wazo langu la kutaka kuanzisha maabara ya kupima DNA ili kusaidia uboreshaji wa ile takwimu yetu ya asilimia za mkemia mkuu ile.

Sasa rafiki yangu alikuwa analifanyia kazi taratibu,
Na kanipa ripoti kuwa keshapata mashine mitambo yote muhimu ya upimaji,Wakuu,

Nina rafiki yangu yupo Hongkong,
Katika mazungumzo yetu ya hapa na pale nikampa wazo langu la kutaka kuanzisha maabara ya kupima DNA ili kusaidia uboreshaji wa ile takwimu yetu ya mkemia mkuu ile.

Yule rafiki yangu kanipa ripoti kuwa keshapata mashine na mitambo yote muhimu ya upimaji wa DNA,
Hivyo kaniambie tufuate taratibu za uanzishaji wa maabara yetu ya kipekee,
Kisha aisafirishe mitambo ili tuanze kupiga kazi.

--------------
Kumbe ubuyu juu ya uanzishwaji wa maabara ushavuma,

Nimeshangaa kuona tangu majuzi wazee wengi hapa kitaa wanakuja kuniulizia bei ya kufanya vipimo vya kugundua uhalali wa watoto-

Sasa wazee wengi wamekuwa wakinipa BigUp kinoumah baada ya kuwaambia kuwa nataka kufanya bure kwa miezi 6 ya mwanzo,
Na wamenisisitiza nifungue haraka sana hiyo maabara pendwa.

-----------------------
Sasa kinyume chake,
Wanawake wengi hasa waliopo ndoani wameanza kunichukia ghafla bin vuuuuuuuu,

Tena kwa chuki ya Wazi.

Kuna kikundi cha akina mama kama 9 hivi,
Miongoni mwao ni wafanyabiashara, watumishi & wake wa wazito
wamenifuata na kuniambia

" Seneta Wa Mtwiz,
Tunajua kuwa we' ni kijana na unatafuta riziki,
Ila tafuta biashara ingine sisi tutakusaidia kwa nguvu zote,
Na sio hiyo project yako ya kuwaharibia wengine mishemishe na kuvuruga ndoa na familia za watu hapa mjini-

Tukunaomba uwe tayari mwisho wa mwezi tukupatie kama M. 8 tu za kuanzia ili ukafanye mambo mengine.
Achana kabisa na hayo mambo ya Kupima watu DNA
Vinginevyo kitakachokukuta-
Utatamani urudi Mtwara kwa miguu.

Have a great care,
The World is not fair."
---------
Na pia nikapigiwa simu kama 21 hivi za onyo kali kutoka kwa wanawake tofauti juu ya huu Mradi wangu Tarajali wa Kupima DNA.

WAKUU,

KWANI HAWA WANAWAKE WASIWASI WAO NINI??

NA VIPI
HII MAABARA PENDWA NIIANZISHE AU VINGINEVYO??

MAANA'KE MIMI SIO MTU WA MCHEZO MCHEZO,
NA HUWA SIJARIBIWI KABISA MIMI!
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Kama machine zenyewe zatoka China hata Mimi napata wasiwasi
 
Basi wanachoogoopa ni ukweli kujulikana maana watoto si wa waume zao.. au ni viruka njia sana.. sasa wanahofia majibu.
 
Fungua tu ila anza kupima wewe na dingi yako ulete majibu hapa
 
Hamna kiumbe nisichokiogopa na ninachokidharau kupitiliza kama *mwanamke asojielew*.

Sasa mkuuu iyo million 8 nikitu gan ???? Umefikilia garama za mashine za DNA na Faida yake baada ya miaka mwaka mmoja tu ???

Kama utasimamisha project yako kisa washenzi basi wee naye niwakupimwa mkojo.
 
Back
Top Bottom