Maaada: Naomba faida za kuchanja chale mwilini.

MuganyiziMushiMwaipopo

JF-Expert Member
Oct 14, 2018
359
691
Naomba kujua faida za kutoboa toboa mwili kwa kuuchanja chale mwilini hii ni baada ya kutembea Mikoa hasa ya Kigoma, Shinyanga, Rukwa pamoja na Tabora.
Kwa utafiti wangu wa muda mfupi kwenye mikoa hii unakutana na watu wengi hasa wazawa wana chale mwilini.
Unakuta mtoto mdogo ana chale usoni, mgongoni, Kifuani hadi miguuni kila niliyejaribu kumuuliza faida zake wengi hawajui wengine wanadai walikuta washachanjwa toka wakiwa wadogo, Wengine wanasema ni kinga na wengine wanadai ni urithi wa kikabila dah!!!
Wana JF wanaojua haya mambo naombeni ushauri wenu na faida za kuwa na chale mwilini maana imefika hatua ya kuogopa watu wenye chale mwilini nikihisi ni Wachawi.
Nawasilisha...
 
Kuna zile zilizochanjwa kwenye uso pembezoni kidogo kwa mwacho zilichanjwa ili kuondoa au kupunguza makengeza.

Chale za miguuni huchanjwa watoto ambao ni wazito kutembea, mfano mtoto ana miaka 2½ hatembei. Akichanjwa hizo chale anapakwa dawa na anatembea.

Chale za usoni hasa katika paji la uso, zipo zilizochanjwa au zinachanjwa kwaajili ya tiba ya maumivu ya kichwa( kiponda uso).

Zipo zinazochanjwa sehemu mbalimbali za mwili, hizi huwa ni za tiba. Mfano, kufa gazi, maumivu ya miguu/magoti na viungo vya mwili, kupooza, matibabu ya bandama n.k.
 
Kuna zile zilizochanjwa kwenye uso pembezoni kidogo kwa mwacho zilichanjwa ili kuondoa au kupunguza makengeza.

Chale za miguuni huchanjwa watoto ambao ni wazito kutembea, mfano mtoto ana miaka 2½ hatembei. Akichanjwa hizo chale anapakwa dawa na anatembea.

Chale za usoni hasa katika paji la uso, zipo zilizochanjwa au zinachanjwa kwaajili ya tiba ya maumivu ya kichwa( kiponda uso).
Asante mkuu kwa ufafanuzi wazungu wakija hapa watakwambia in mambo ya kizamani
Cc Yericko Nyerere
 
Back
Top Bottom