Ma-TO wawili katika mtihani mmoja Japhet S John na Aude G Kileo

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,160
2,000
LEO NGOJA NIKUMBUSHIE TUKIO ZURI SANA KUHUSU ELIMU

Ni muda mrefu sana sijaandika kuhusu Maswala ya ELIMU hivyo wengi wakanibatiza majina mara 'Mr Love ', 'KIBAMIA','Mwanaharati' na wengine wakaenda mbali nakuniita 'MZEE WA MISAMBWANDA '

Hahahaha me nafurahi tu kuona watu wakinichukuliwa tofauti na uhalisia wangu.

Sasa niweke wazi tu kuwa katika mambo ya 'elimu' nipo mstari wa mbele kabisa kusaidia mapambano hasa kwa watoto wa 'NDALICHAKO ' kufaulu mitihani yao.

Humu JF tumesoma shule katika zama tofauti kabisa,mfano mimi nilianza la kwanza kipindi cha MKAPA na nikamaliza 6 kipindi cha KIKWETE aka MZEE MAARUFU.

Katika elimu kwa kipindi hiki yalitokea matukio mengi sana ila leo nataka kuongelea moja tu ambalo linakuwa chachu ya kufaulu kwa wanafunzi wa sasa kama watasoma uzi huu.

TUANZIE MWAKA 2009
Kulikuwa na mwanafunzi anasoma Form 6 KIBAHA anaitwa 'AUDE KILEO'

Huyu mwanafunzi alikuwa ni best best na best of all pale kibaha kwa uwezo wake katika kombi ya PCM.
Huyu 'AUDE KILEO' Alikuwa mtu wa ajabu ajabu maana waliporipoti tu Kuanza kidato cha 5 akiwa ameshasoma huko vibanda umiza masomo yote ya PCM na mada zote zote.Yani jamaa kwa kifupi alienda shule akiwa amesoma mada zote za Physics,Chemistry na Mathematics kuanzia za form 5 mpaka za 6.Jamaa was very intelligent.

Nov 2008 kulikuwa na mitihani ya mock form 6 kanda ya kaskazini hivyo akaamua aende akajipime ubavu ILBORU yaani akaombe afanye mitihani ya kanda ya KASKAZINI baada ya kuona mitihani ya kanda yake KIBAHA hakuna mpinzani ambaye alimkaribia hata kwa mbali.

JAMAA akatimba ILBORU kufanya mitihani na wakanda hiyo. Sasa cha ajabu ni kuwa katika shule ya ILBORU alikuwepo kijana mmoja ambaye kwa wakati huo yeye alikuwa kidato cha 5 hivyo hatofanya mitihani ya FORM 6 maana hajafika huko. Kijana huyu alikuwa anaitwa 'JAPHET JOHN'.

Jamaa kaforce kuwa yupo tayari kulipia hela ili tu ajipime kwa uwezo wake aliofikia japo ni wa kidato cha chini.

UONGOZI wa shule ukaona 'MTOTO ' akililia wembe mpe umkate, hivyo kijana 'JAPHET JOHN ' akaruhusiwa kufanya mtihani huo wa kanda wa kidato cha 6 japo yeye ni kidato cha tano.

Hahahahahaha kitu ambacho wengi walikuwa hawajui ni kuwa mnyama 'AUDE KILEO ' atakuwa dimbani

SIKU YA MTIHANI IKAFIKA
Mtihani ukafanywa ambapo MTABE 'AUDE KILEO ' Kutoka MKOA wa PWANI(KIBAHA) akawa mwanafunzi bora kikanda na KIJANA aliyekuwa nyuma kidarasa JAPHET JOHN akawa wapili KIKANDA.

Wengi walishangaa kuona mwanafunzi wa kidato cha tano anawashinda kidato cha 6 WOTE kasoro mmoja tu tena sio wa kanda ile ila aliomba tu kushiriki.

AUDE KILEO alirejea KIBAHA SEC na KUWAABMIA WENZIE KUWA 'MIMI MWAKA HUU NITAKUWA TO ILA MWAKANI TO ATAKUWA JAPHET JOHN WA ILBORU'.Akawapa sifa zake

Kweli matokeo ya form 6 kitaifa mwaka 2009 AUDE KILEO alikuwa mwanafunzi wa kwanza KITAIFA kama alivyotegemea na MATOKEO YA FORM 6 MWAKA ULIOFUATA WA KWANZA ALIKUWA NI YULE YULE 'JAPHET JOHN ' wa ILBORU

Hii tunaita 'Kuwa TO kunahitaji mandalizi ya kutosha'
upload_2017-12-13_2-32-3.png


upload_2018-1-2_3-28-43.png

(Japhet john pia alikuwa TO FORM 4 akitokea shule ndogo kabisa ya ARUSHA DAY)

upload_2017-12-13_2-35-47.pngNOTE:Mtihani wa mock ambao JAPHET JOHN alifanya na AUDE KILEO ulihusisha MA-TO wawili hivyo lazima mmoja awe wa kwanza na mwingine awe wa pili.(FAHARI WAWILI HAWAKAI ZIZI MOJA )

UPDATE
=========
AUDEN KILEO akiwa Kibaha hajawahi kumpita RAYMOND AIDAN.Watu wote Kibaha walijua RAYMOND AIDAN ndio atakuwa T.O baada ya kuchukua Magamba yote Kuanzia Physics,Chemistry Mpaka Mathematics Huku AUDEN KILEO akiwa mtazamaji tu yaani alikuwa amekaa kwenye kiti chake siku ya graduation akimpigia RAYMOND AIDAN makofi na vigelegele anavyochukua 'ZAWADI' kama mfalme na T.O mtarajiwa atakayeiwakilisha KIBAHA SPECIAL SCHOOL .Mungu sio Deadbody Watu wote walibaki wanashangaa baada ya AUDEN KUIBUKIA 'MOCK' na mwisho kwa mshangao huo huo AUDEN anaeeelekea kuwa T.O huku T.O wa KIBAHA(Raymond Aidan) akishika nafasi ya PILI KITAIFA.

Waliosoma Kibaha PCM 2007-2009 wanasema ilipofika mitihani ya nje ya shule walikuwa WANAMWANGALIA 'AUDEN KILEO'.

NOTE:Ukiangalia TOP 10 Ya mwaka 2009 utaona wa kwanza na wa pili kitaifa walitoka KIBAHA


Deadbody
 

monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,187
2,000
Mi naomba kuwauliza hapa jamaa tutawaitaje?

Coz kwa upeo wangu wamesoma shule bora na wamekuwa bora kabisa tangu mwanzo...
sasa mi nakupa mifano tofauti kidogo wa jitihada bila Msaada.

Kuna jamaa mmoja alisoma kigonsera PCB Akapata Division 2 point 11.

Tena jamaa alinyimwa matokeo sababu ya kutolipa ada ya wakati ule 40,000.

Jamaa alikuwa kwao hawana uwezo kabisa acha tuu na alikuwa shuleni anaenda kwa kuvizia vizia six pale 2002 Kigonsera waliosoma pale wanaweza mkumbuka.Darasani walikuwa hakuna walimu wa Physics na chemistry.alikuwa anategemea sana waliosoma tuisheni waliotoka Mjini DSM.

jamaa akapata nafasi shule Mzumbe University,(MU)
2004,
Bsc.Production&Operations management,akamaliza 2007.GPA 4.9 Akawa Assistant lecture. MZUMBE UNIVERSITY

AKAENDA KUSOMA Msc.Engineering Management-udsm,wakawa wanamuambia Ohhh wewe hujasoma hapa Udsm,hujasoma sijui Ma engineering utakoma,jamaa akawa anawacheki tuu UE Kaibuka 4.6 GPA
UNAWEZA ONA Jitihada ya jamaa

Alikuwa anajiita "Son of Peasant"
Sasa hivi anasoma Phd tangu mwaka jana.
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,960
2,000
Life is not fair, pamoja na mbu, na kufunua karatasi zote za library, mwisho wa Siku ndio anakuja kuajiliwa na muuza karanga wa Tandale.
Nilikuwa na waza tu.
kusoma na kutoboa maisha ni vitu viwili tofauti. hebu nitajie ma T.O ambao wako kwenye top ten za matajiri Tanzania, East Africa, Africa Au duniani unao wafahamu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom