M4c na chopa 4 huku makatibu na wenyeviti wa wilaya na mikoa njaa kali

Yeye anachotaka ni uwiano katika malipo na akidokeza kuwa kuwa, kama katibu mkuu wa chama analipwa zaidi ya milioni saba kwa mwezi, kwa nini basi usiwepo utaratibu wa kuwalipa hata kidogo watumishi wa chini wa chama.

Yeye mwenyewe shahidi akaunti hazina ki2, asa mishahara itatoka wapi?
 
Hiki Chama kimeanza miaka 20 iliyopita. Hatukuwa na ruzuku. Ruzuku imeanza kuja kwa kiwango kizuri mwaka 2010 baada ya kupata kura za kutosha. Sasa tungekuwa tunategemea ruzuku tungefikaje 2010?
Kwa mawazo ya mleta uzi Chadema ingekuwa imeshajifia kwa sababu haina posho. Posho ukiweka mbele ndani ya Chadema hutakaa hata mwaka moja. Hii ni kwa sababu hata pesa kidogo zipo kwa uzoefu wangu hatulipani posho.
Binafsi nilikuwa mkiti wa jimbo la Ubungo lakini hatukuwa na posho ya vikao hata nauli mara nyingi tunajitolea. Ruzuku ina kazi za muhimu kuliko posho.
Hili wimbi la watu wanaokuja kwa kasi kutoka ccm na kujiunga na chadema wanakuja na uzoefu ambao unaweza ukatupa tabu kwa Muda lakini naamini mbele ya Safari tutaelewana.

Safi sana Kamanda lazima tuwaeleweshe hawa Magamba,Wateka nyara sie hatuna utamaduni wa kulipana chai lengo letu ni moja tu kukomboa nchi kutoka kwa hawa wakoloni weusi kima Ccm Magamba,si wanaona chama Makini na watu/viongozi wao wanajitolea kwa hali na mali ndio maana roho zinawauma.Peoples Power hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom