M4C Mtwara, Mikakati,wakati na Maeneo ni wapi?

Nikumbushe hivi bwawa la nabwada liko mdenga namadi au pale idara ya maji??
Hoja nimeipenda na nimeongea na zito plan ziko underway kuja mtwara kupiga kambi. so wakuu tukae mkao wa kula kamanda anakuja na full skwad
 
Utawala na madaraka katika nchi ni nyanja yenye upana mkubwa tofauti na wengi tunavyoangalia kwa upeo mwepesi. M4C ni mkakati imara na bora zaidi katika kuleta mapinduzi ya kweli. Kadiri siku zinavyosonga mbele, ndivyo idadi ya wapiga kura vijana inavyoongezeka nchi nzima. Upinzani nao unazidi kupata mtaji wa wanachama kutoka vijana hasa waliozaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi. Hawa hawakusikia propaganda ya vitisho kabla ya mfumo wa vyama vingi kuwa, vyama hivi vitaleta vita na umwagaji wa damu, kauli ambazo zilifanya mbumbumbu wengi kuwa waoga wa kutupwa. Sasa basi, leo tumebuni mkakati M4C ili kuendelea kuleta ushawishi kuyafikia mabadiliko, lakini tunawaandaa vipi watu wetu kuupokea utawala mpya siku upinzani hasa CDM ikishika madaraka? Kuna kipindi kifupi kijacho kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Nchi nzima tuna wakuu wa mikoa ambao ni makada wa CCM. Wakuu wa wilaya ni makada wa CCM. hali kadhalika na waambata wao hivyohivyo. Leo Mbowe, au Slaa au Zitto, akiwa rais atatawala vipi wakati mfumo CCM ndiyo umekalia mishipa yote ya fahamu ya nchi hii? Nashauri! Wakati M4C Inafanyika, iendane na uteuzi wa viongozi vizuli katika mikoa na wilaya zetu kama ilivyo bungeni. M4C Ijiongezee jukumu la kuhakikisha kila mkoa unakuwa na mkuu wa mkoa kivuli. Wilaya vilevile, nao washirikiane na wananchi tangu sasa katika hamasa ya kuleta mabadiliko. Bila ya kuwa na mkakati wa kweli tangu mapema. CDM inaweza kujikuta inashika hatamu ya uongozi ikiwa na rais na wabunge bila ya watendaji makini katika serikali. Hiyo itakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Mkuu umenena sawa hilo ndo tatizo watakalo kutana nalo Chadema kama watafanikiwa kushika Nchi na matokeo yake kwa kuwa watakuwa hawana watu wakushika hatamu hizo walewale waliokuwa CCM watajiunga na Chadema na watapewa madaraka na kwa vile Chadema itakuwa haina muda wa kuwachunguza manbo yatarudia yaleyale ndipo Watanzania watakapohisi kuwa wamedanganywa na Chadema kuwa maisha yatakuwa mazuri kumbe siyo na Vurugu ndozitaanzia hapo!
 
nyie kusini hamna kitu. mtu anaharibu lasrimali ya nguvu za kuja huko halafu kwenye mikutano hamtokei. nyie subilini mtakombolewa na watanzania wenzenu wa kanda ya ziwa, mbeya, ruvuma, kilimanjaro na msoma.
 
Mkuu Nabwada, habari za Nabwada..., sisi huku Chuno tumesha jikabidhi kabandari ketu. Angalizo kwa CDM: Mh Lipumba kesho atarindima Viwanja vya Mashujaa, hawa jamaa wa CUF wanazidi kujenga mizizi huku kusini. Kimsingi CUF itafanikiwa katika hili kwa sababu wananchi wa Mtwara hawana chaguo m'badala, lkn CDM wakitia mkazo huku mjue majimbo ni yetu.
mkuu upo chuno mimi nipo hapa Coco beach nafanya uhamasishaji kwa vijana wa hapa. Pia watu mtwara kuna vitu vya kijinga kama kutoa uchawi ndio wanavpa kipaumbele, kwanza itabidi wabadili mind set zao.
 
Back
Top Bottom