M4C Mtwara, Mikakati,wakati na Maeneo ni wapi?

Nabwada

Senior Member
Apr 5, 2012
124
33
Wana bodi naomba kujua ile ratiba ya Wakombozi wa Nchi yetu lini CHADEMA watakuja Mtwara?,kuna watu humu jamvini wanatufikiria sisi watu wa huku ni wale ambao wao waliwaacha kile kipindi walipoletwa huku kama adhabu,siyo.
 
Kitu kitakacho nifanya nirudishe kadi ya CDM ni hili, mwaka ukiisha hawaja fika kanda ya kusini najivua gwanda.
 
Waje watoe Elimu ya Uraia ya kutosha hapa.Tumechukia sana tuliposikia Bandari imeuzwa.Kama ni kulipa deni kwanini wasiiuze ya Dar au yaTanga kwa Nundu?,
 
Nimefarijika kuona jirani zangu na nyinyi mnaanza kuitikia mwito, watu wakusini tunakazi kubwa yakufanya kuwaelimisha maskini wa Lindi na Mtwara waitikie mwito wa M4C, kama mnakumbuka uchaguzi liopita kuna watu waliwapotosha watu kwamba CDM ni chama cha wakristo sasa hii ni fikra potofu watu wanalenga kuikomboa nchi na si vinginevyo. walio elimika tuungane kuwaelimisha ambao hawajaelimika. kamata wezi meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen!
 
Wakuu M4C itafika kila mahali
subirini ngoma itatia timu huko
 
Nimekuwa nikikutana na neno m4c bila kujua maana yako,tafsiri yangu ya haraka inanituma ni movement for changes. Naomba maana wadau wangu wa jf.
 
Ndg.zangu wana JF umasikini uliopo mkoa wa Lindi cjui nisemeje!na M4C isipo ikomboa kusini inabidi tuanze mchakato wakudai jamuhuri ya watu wakusin.
 
Waje watoe Elimu ya Uraia ya kutosha hapa.Tumechukia sana tuliposikia Bandari imeuzwa.Kama ni kulipa deni kwanini wasiiuze ya Dar au yaTanga kwa Nundu?,
Mkuu Nabwada, habari za Nabwada..., sisi huku Chuno tumesha jikabidhi kabandari ketu. Angalizo kwa CDM: Mh Lipumba kesho atarindima Viwanja vya Mashujaa, hawa jamaa wa CUF wanazidi kujenga mizizi huku kusini. Kimsingi CUF itafanikiwa katika hili kwa sababu wananchi wa Mtwara hawana chaguo m'badala, lkn CDM wakitia mkazo huku mjue majimbo ni yetu.
 
Ninakumbuka baada ya kukataliwa kwa hoja binafsi ya Mh.Zitto kuhusu mashamba ya Mkonge,Mh.Zitto,Mh.Mnyika na makamanda wengine walifanya ziara Mkoa wa Tanga kutoa elimu kwa wananchi na kuelezea kile ambacho wabunge wao wamekipinga Bungen.Sasa kama vile mlivyotoa elimu kwa watu wa Tanga,tunaomba Makamanda mje huku Mtwara nasi hatuko nyuma katika harakati hizi za ukombozi wa kweli.Mh.zitto njoo tueleze Mpango mzima wa Magamba kutoa Bandari yetu kama fidia kwa deni linalotokana na mikataba yao ya kilaghai.Katika hili ni lazima tutawahoji na hawa wawakilishi wetu kwani bilashaka wanafaham mpango huu na wameshindwa kulisemea hili.Wananchi sasa wanaichukia sana CCM na serikali yake hasa kwa jinsi walivyo chakachua Malipo ya korosho na kusababisha matatizo mengi katika familia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kupeleka sekondari watoto wao.Wapo waliokuwa wameweka matumaini yao CUF kuwu wangekuwa watetezi wao lakini kwa sasa wengi wanaelewa kuwa CUF imepoteza mwelekeo kwani hata katika uchaguzi mkuu uliopita ilipoteza viti vya udiwani katika kata ambazo zilikuwa chini yake kabla ya uchaguzi.Mfano ni pale(Mkuti)Masasi.Tunaomba M4C iwe kwa wa TZ wote bila kutubagua watu wa Mtwara.
 
Wana bodi naomba kujua ile ratiba ya Wakombozi wa Nchi yetu lini CHADEMA watakuja Mtwara?,kuna watu humu jamvini wanatufikiria sisi watu wa huku ni wale ambao wao waliwaacha kile kipindi walipoletwa huku kama adhabu,siyo.

Mkuu hivi bwawa la nabwada bado lipo hai?. Nakuunga mkono mkuu CDM waje ili ukombozi upatikane kwetu huku. CCM wanazidi kuuangamiza mkoa wetu wakati tuna rasilimali za kuweza kuufanya mkoa wenye maendeleo makubwa. Hivi kama yule mhindi anafanya nini bungeni jambazi kama yule??? Ona type yenyewe kama akina Ng'ange, Sinani na huyu mdosi yaani hakuna kitu. Halafu nimeona tuko wengi humu hivi hatuwezi kuanzisha group letu humu?
 
Mkuu hivi bwawa la nabwada bado lipo hai?. Nakuunga mkono mkuu CDM waje ili ukombozi upatikane kwetu huku. CCM wanazidi kuuangamiza mkoa wetu wakati tuna rasilimali za kuweza kuufanya mkoa wenye maendeleo makubwa. Hivi kama yule mhindi anafanya nini bungeni jambazi kama yule??? Ona type yenyewe kama akina Ng'ange, Sinani na huyu mdosi yaani hakuna kitu. Halafu nimeona tuko wengi humu hivi hatuwezi kuanzisha group letu humu?

inasikitisha sana kwa watu wa mtwara kuendelea kuchagua hawa vibaka. Panapo majaaliwa 2015 Lazima nije kupiga kura ya hasira hapo Mtwara mana naumizwa sana na huu umasikini wa kutupwa wa Lindi na mtwara. God bless south Tz
 
Wana bodi naomba kujua ile ratiba ya Wakombozi wa Nchi yetu lini CHADEMA watakuja Mtwara?,kuna watu humu jamvini wanatufikiria sisi watu wa huku ni wale ambao wao waliwaacha kile kipindi walipoletwa huku kama adhabu,siyo.

Muda si kitambo makamanda watatia timu huko! vuta subira mkuu wamalize kanda ya ziwa!
 
Nimegundua mtwara ni maji bardi
,
Yaani bandari yenu imegawiwa walebanoni kama kuwapoza na nyie mpo mpo tu, hivi ngoja niwaulize muindi wenu murji alisaini karatasi ya zitto?

Mji wa mtwara upo upo tu, barabara vumbi tupu hali ni mbaya,
Mmekaa na nyie mnasema mna mbunge,

Huko tandahimba nako eti nao wanasema wana mbunge?
Masasi eti mbunge wao anaitwa dastan mkapa, yaani mlichagua jina?
hivi ikiletwa hoja ya kufuta marupurupu kwa marais wastaafu wasiojiheshimu kwa kumtukana baba wa
taifa huyu atapiga?
 
Utawala na madaraka katika nchi ni nyanja yenye upana mkubwa tofauti na wengi tunavyoangalia kwa upeo mwepesi. M4C ni mkakati imara na bora zaidi katika kuleta mapinduzi ya kweli. Kadiri siku zinavyosonga mbele, ndivyo idadi ya wapiga kura vijana inavyoongezeka nchi nzima. Upinzani nao unazidi kupata mtaji wa wanachama kutoka vijana hasa waliozaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi. Hawa hawakusikia propaganda ya vitisho kabla ya mfumo wa vyama vingi kuwa, vyama hivi vitaleta vita na umwagaji wa damu, kauli ambazo zilifanya mbumbumbu wengi kuwa waoga wa kutupwa. Sasa basi, leo tumebuni mkakati M4C ili kuendelea kuleta ushawishi kuyafikia mabadiliko, lakini tunawaandaa vipi watu wetu kuupokea utawala mpya siku upinzani hasa CDM ikishika madaraka? Kuna kipindi kifupi kijacho kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Nchi nzima tuna wakuu wa mikoa ambao ni makada wa CCM. Wakuu wa wilaya ni makada wa CCM. hali kadhalika na waambata wao hivyohivyo. Leo Mbowe, au Slaa au Zitto, akiwa rais atatawala vipi wakati mfumo CCM ndiyo umekalia mishipa yote ya fahamu ya nchi hii? Nashauri! Wakati M4C Inafanyika, iendane na uteuzi wa viongozi vizuli katika mikoa na wilaya zetu kama ilivyo bungeni. M4C Ijiongezee jukumu la kuhakikisha kila mkoa unakuwa na mkuu wa mkoa kivuli. Wilaya vilevile, nao washirikiane na wananchi tangu sasa katika hamasa ya kuleta mabadiliko. Bila ya kuwa na mkakati wa kweli tangu mapema. CDM inaweza kujikuta inashika hatamu ya uongozi ikiwa na rais na wabunge bila ya watendaji makini katika serikali. Hiyo itakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Chadema ikichukua nchi watendaji wa serikali ni watumishi walioko serikalini sasa.
 
Back
Top Bottom