Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Naomba tujaribu kuchangia hapa!
Nilitaka kujua tu M PESA inafanyaje kazi.
Kwanza nilitafuta sheria yetu inasemaje. Kwamba kila taasisi inayojishughulisha na fedha lazima iwe imepata leseni toka Benki kuu ya Tanzania. Kufanya kinyume na haya ni kuvunja sheria za nchi kwa mujibu wa THE BANKING AND FINANCIAL INSTITUTIONS ACT 2006. Nimepitia kote, FINANCIAL INSTITUTIONS, COMMERCIAL BANKS na hata REGIONAL UNIT BANKS hakuna pahala Vodacom, Tigo wala Airtel wamesajiliwa kufanya biashara ya fedha! Kwa hili linanituma kusema kuwa hawafanyi biashara kihalali na hii inaweza kuliingizia hasara kubwa Taifa hili.
Wataalamu wa VODACOM wanasema kuwa ukitumia huduma ya M PESA lazima transaction zako lazima ziende Uingereza then zirudi kwenye mitambo ya Vodacom Tanzania. Ina maana kuwa Benki Kuu ya Tanzania haihusiki ku- monitor chochote kwenye hizi huduma.
Kama ni kweli BOT hawana muingiliano na hizi taasisi je ikitokea siku moja Voda ama Airtel ama Tigo wakasema database yao imecrush itakuwaje?
Je ina maana kuwa BOT (T) hawajui hilo ama wanafumba macho kwa personal interest za watu wengine?
Kuna pia fununu nimeisikia kuwa VODACOM walifanya party pale Dodoma kwa ajili ya waheshimiwa na kila mtu akaondoka na kibahasha kinono ili kuwafumba macho ( sina uhakika sana ila kama kweli watatuambia humu).
Naomba kuwasilsha
EM