Wadau, mimi ni wakala wa shughuli za M-Pesa na za kibenki, nimekuwa nikipata shida sana ninapopeleka pesa mbovu benki ambazo nimezipokea kutoka kwa wateja ambao wanakuja kupata huduma ofisini kwangu.
Watu wa benki wanasema pia wao wanahojiwa na BOT pesa mbovu wanazipata wapi? Wakati kiuhalisia pesa mbovu lazima zipo katika mzunguko.
Kwa jinsi ninavyojua Benki yoyote Tanzania ni kama Wakala wa BoT (act as ana agent of BoT) hivyo wateja wao wanapopeleka pesa mbovu inatakiwa wawahudumie. Wanapozikataa sasa wateja wazipeleke wapi? Hili limekuwa Kero sana kwa wateja.
Naomba kujua utaratibu upoje kuhusu hizi pesa mbovu ambazo mtoa huduma wa biashara za kawaida anapokea kutoka kwa wateja azipeleke wapi?