M pesa kuna tatizo gani ?

M pesa kuna tatizo gani ?

njugilo

Member
Joined
Feb 8, 2010
Posts
58
Reaction score
28
Wakuu toka tarehe 01/04/2013 kuna pesa nimezituma kwa ndugu lakini zijapata ripoti ya kuwa zimekwenda au kukwama lakini ndugu kasema hajazipata,na tarehe iliyofuatia niliongeza salio kwenye akaunti lakini taarifa mrejesho kwa wakala ikatoka kwangu sijapata.Nikatuma tena pesa kwa ndugu mwingine yeye kazipata lakini taarifa za mrejesho sijazipata.Nimejaribu kupiga namba hizi za huduma 15000 na 15366 (customer care) na haziiti muda wote "'Network busy"
Sasa kama kuna yeyote anayejua njia mbadala za kuweza kuwapata mnijuze tafadhari!
 
hawa voda wanatutia hasara hasa sisi mawakala kila siku shoti mana transaction znafail huku ushampa mteja fedha matokeo fedha inarudi kwa mteja.wiki ya pili sasa matatizo haya
 
ni vizuri tuwe na mazoea ya kuangalia salio kabla na baada ya muamala ili kuwa na uhakika kama muamala umefaulu au la.
hata kama message hujapata una kuwa na uhakika kwa kuangalia balance.
 
Piga 100 then fuata maelekezo..ni rahic sana..mimi nlikumbwa na tatizo km lako..namba zako hz itakuwa ngumu kuwapata
 
fuatilia kupitia namba hiyo uliyopewa (15366)
matatizo hayo wkt mwingine yanatokea.
ndio kazia ya DIGITAL ... pole sana
maana endapo ndio msaada wa fedha za dharura unahitajika (hali itakuwa mbaya)
 
Sawa wana JF nitaendelea kuwatafuta kwa namba 100 maana kama ilikuwa pesa ya kupeleka hosp kwa dharura basi majanga yangejitokeza
 
mie wakala cna hamu kabsa maana kaz hakuna ukijarbu matatzo wateja hawaelewi somo wala darasa,"Mteja anaambiwa waombe waangalie cm yao kwa makn"%-).2angalie nn wakat hamja tuma sms.TCRA HAIPO TZ. Au imepewa kitengo kingne SUBIRN AJE KIONGOZ ATAKAE WAWAJIBISHA.TUMESHAPATA NAULI.
 
ni vizuri tuwe na mazoea ya kuangalia salio kabla na baada ya muamala ili kuwa na uhakika kama muamala umefaulu au la.
hata kama message hujapata una kuwa na uhakika kwa kuangalia balance.

c kwel mkuu, hakikisha umepata sms ya udhitisho kuwa pokea au toa kiasi cha fedha kutoka kwa wakala au mteja kama hukupata hyo sms fedha ztarud kwenye a/c yako. Ile sms ni ndo risit namba yako.
 
Hiyo tisa kumi ni hii..mimi ni wakala wa Mpesa..jana kuna mtu kaja kutoa 350,000 sms ya Mpesa ikaingia na nikaangalia salio limeongezeka..nikampa pesa na nikaandika huo muhamala kwenye kitabu.. salio langu likawa ni 400000 maana kabla ya muhamala wa mwisho nilikua na 50000..nilipotoa hizo 350,000 nikawa na salio la 400,000.baada ya muda alipokuja mtu nimtumie 300000 nikashangaa naambiwa sina salio..kucheki salio nakuta ipo 50,000.nimewapigia voda wanasema hiyo no. Iliyotoa hela ilifungiwa isitoe hela toka siku nyingi na hawakua na kingine cha kuniambia..swali langu imekuaje no. Iliyofungiwa imeweza kutoa no. Na sms ya Mpesa kuja kwangu wakala??kuna mchezo hapa
 
Wana JF tuwe makini na mambo ya kiditali badala ya kuwa rahisi kwa kueka na kutoa fedha yanaweza kutughalimu na kuleta mahusiano mabaya kati yetu.Mie hatimae nimewapata kwa namba 15000 na kunipa ankara ya muamala wote nilioufanya na uko sahihi .JF ni tumaini jema tulitumie kwa makini,maana tatizo unalolipata usikumbatie.Kwako unaweza dhani ndio wa kwanza kumbe mwenzio kalitatua muda mfupi au alishapata muda fulani zamani na likaisha for just a single click.
 
Hii huduma nilishaichukia toka zamani, yaani ni full ubabaishaji makato ndo usiseme!!
 
Hiyo tisa kumi ni hii..mimi ni wakala wa Mpesa..jana kuna mtu kaja kutoa 350,000 sms ya Mpesa ikaingia na nikaangalia salio limeongezeka..nikampa pesa na nikaandika huo muhamala kwenye kitabu.. salio langu likawa ni 400000 maana kabla ya muhamala wa mwisho nilikua na 50000..nilipotoa hizo 350,000 nikawa na salio la 400,000.baada ya muda alipokuja mtu nimtumie 300000 nikashangaa naambiwa sina salio..kucheki salio nakuta ipo 50,000.nimewapigia voda wanasema hiyo no. Iliyotoa hela ilifungiwa isitoe hela toka siku nyingi na hawakua na kingine cha kuniambia..swali langu imekuaje no. Iliyofungiwa imeweza kutoa no. Na sms ya Mpesa kuja kwangu wakala??kuna mchezo hapa

Uko wizi wa chinichini mpesa.mi nilipewa namba isiyo sahihi na wakala wakati natoa fedha.badala yake kiasi cha sh.60,000/= nilichotoa kikaenda kwa wakala mwingine.nimewataarifu vodacom (15366) muda uleule tukio lilipotokea yaani 15/02/2013...!wananizungusha tuuuu.mara wanasema wakala hapokei simu.mara wakala hana hela. mara nisubiri tatizo langu linashughulikiwa,mara tunalipeleka tatizo lako kwenye idara husika...!!!??..,mwezi wa pili sasa !!,mpaka leo wananizungusha tu :nono:.Hivi malalamiko yetu wateja/walaji tuyapeleke wapi?.Kwanini hawa voda wanaendelea kuimba kwenye matangazo yao kuwa m-pesa ni salama,wakati matukio ya wizi/utapeli yanaendelea kutokea??:A S-confused1:.Je kuna taasisi za usimamizi wa biashara za fedha(digital money)?,je zinajua haya???.Hivi kama vodacom wakiamua kuiba shilling 1,kwa kila mpesa account kwa siku,mamlaka hizo zinaweza kugundua??? ...mmh,tunahitaji kuchukua hatua.
 
Hawa jamaa nami wameniliza wiki hii, kuna jamaa alinitumia 20000 kwenye line yangu ya tigo, nikaenda mara 3 kuzitoa lakini imeshindikana sababu ya mtandao, juzi wamenitumia msg kuwa pesa zimerudishwa zilipotoka, nimewasiliana na aliyenitumia kasema kwake hazijarudi mpaka sasa inamaang nimechezeshewa cheusi na chekundu.
 
Wote wako likzo ufahar unaonesha kwa wagen wakija lakn kusimamia majukumu ni 0 per qbc
 
Njooni Airtel money.Yaani kitu imetulia ile mbaya. Hakuna longo longo!
 
Njooni Airtel money.Yaani kitu imetulia ile mbaya. Hakuna longo longo!

Hapo ndo nitaharibu kabisa maana money transfer inachukua week nzima ,ukiingia majanga lazima yakukute,lakini inategemea na mahali ulipo.
 
c kwel mkuu, hakikisha umepata sms ya udhitisho kuwa pokea au toa kiasi cha fedha kutoka kwa wakala au mteja kama hukupata hyo sms fedha ztarud kwenye a/c yako. Ile sms ni ndo risit namba yako.

mkuu kwa kuangalia sms tu, haita hakikisha asilimia 100. kuna matapeli sikuizi wana uwezo wakukutumia message kwa mfano anajifanya anaenda ku cash out kwa wakala, halafu anatuma message(kama ni kwa wakala wa tigopesa) message inakuwa kama imetoka tigopesa, kwaiyo kama usipo kuwa mwangalifu, unaweza kulizwa pia.

halafu nimesema tujenge mazoea ya kuangalia salio pia. sio njia rasmi ya kuthibitisha, la hasha, inasaidia kuhakikisha kama hela kweli imeingia.
 
inawezekana imerudishwa, tigopesa usipotoa hela ndani ya siku saba kama hujajisajili inarudi kwa mtumaji.
mtumaji wako inawezekana hajaangalia vizuri
 
Back
Top Bottom