M/Kiti wa UVCCM mkoa wa Ruvuma jela miaka 36 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M/Kiti wa UVCCM mkoa wa Ruvuma jela miaka 36

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 26, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma, imemhukumu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, John Komba, kutumikia kifungo cha miaka 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh 80 milioni.

  Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Baptista Mhelela, alisema jana alipokuwa akisoma hukumu hiyo kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 24 kwamba, Benedict Ngwenya, alitenda kosa hilo la kuiibia Kampuni ya DAE Ltd.

  Kwa mujibu wa Hakimu Mhelela, Mahakama hiyo bila shaka yoyote, imeridhika na ushahidi huo na kwamba imemtia hatiani mshitakiwa Ngwenya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mpepai katika Wilaya ya Mbinga.

  Alifafanua kwamba mshitakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa 13, lakini kosa moja kati ya hayo ambalo ni la kughushi kwa maandishi alishinda. Alisema ametiwa hatiani kwa makosa mengine 12 yaliyobaki.

  Awali, Mwanasheria wa Serikali, Mwegole Shabani, alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Ngwenya alitenda makosa hayo mwaka 2008 kwa nyakati tofauti akiwa anafanya kazi kama mhasibu katika kampuni hiyo ya DAE LtD.

  Shabani alisema mshitakiwa alizichukua fedha hizo kwa lengo la kwenda kugawa kwenye mitambo inayokoboa kahawa mbichi ambapo hata hivyo, hakuzifikisha sehemu husika.

  Alisema baada ya kutenda kosa hilo, aliacha kazi bila kukabidhi ofisi kwa mwajiri wake, jambo ambalo lilimfanya mwajiri huyo kumtilia shaka na kumtaka mkaguzi wa mahesabu wa ndani kufanya ukaguzi ndipo alipobaini upotevu wa fedha hizo
   
 2. e

  erneus kyambo Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana mimi nasema kijana ambaye yuko ccm lazima atakuwa anamaslah ambayo atakuwa anayalinda kwa kutumia mgongo wa chama, haya sasa yamemkuta huyoo ambaye alikimbilia ccm ili imkingie uovu wake, results ni 36yrs in jail! Hongera hakimu
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndivyo ilivyo kila aliyepo huko ni gamba.wengi wao unakuta aliiba,anatarajia kuiba au sabab ya njaa kuna gamba linalomlisha hivyo yupo tayr hata kutembea uchi! Nawaonea huruma ndugu zetu vjjn wanaokiamini chama wakitegemea kitawakomboa!
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yaani ma CCM kuanzia watoto hadi wazee ni wakwapuaji tu .Tanzania hii ni siasa za CCM .Komba atakata rufaa ngojeeni mtasikia na hakimu huyo atakamatwa na rushwa karibuni zengwe lao hawa jamaa .Tegeni masikio .
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Magamba bwana!
   
 6. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  chadema wakachukue kiti cha udiwani., Magamba watajivua na wengine watavuliwa kwa sheria hadi 2015 tutachukua viti vingi sana
   
 7. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wasomi nnaokimbilia CCM kama nia zenu ni hzi basi kitawanukia tu .
   
 8. s

  smz JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa tunavyowajua ccm subiri tu utasikia huyo hakimu hana kazi na ana kesi mbaya ya rushwa. Kama amefikia umri wa kustaafu naomba afanye hivyo haraka. Kama bado naomba afanye mpango aende hata kusoma tena hata miaka miwili ili akute soo limepoa. Vinginevyo 2012 hawezi kuiona.
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tusishangilie hili; hivi Liyumba alifungwa miaka mingapi vile? Yaani aliyeiba milioni 80 anafungwa miaka 36; aliyeiba bilioni 80 anafungwa miaka 2!!!
   
 10. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nilikuwa napita nikaona nikusalimie.
   
 11. MANI

  MANI Platinum Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ndio Tanzania chochote kinawezekana hapa!
   
Loading...