M/kiti wa CUF Kibaha auwawa

M/kiti wa Cuf kibaha ameuwawa ucku wa jana kwa kuvamia na watu wasiopungua kumi na tano wakitumia mapanga. Marehemu alihama ccm na kujiunga na cuf na kuwa mwiba mkali kwa ccm.Ijumaa iliyopita alimweleza jirani yake kuwa anawindwa kuuwawa na wapinzani wake kisiasa. source.mlimani tv.

Hee!? R.I.P
 
Ccm Oyeeeee. Jk safiii, malecela safi. Nape imaraaa? Ccm saafi?
 
Tunawapa pole wafiwa na lazima walihohusika wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria. Intejensia ya kuzuia maandamano ya wapinzani iko wapi katika hili?Ingekuwa maandamano yanataka kufanyika Kibaha wangesema Intelijensia ya polisi inaona maandamano hayatakuwa ya salama je kwa hili wanasemaje?. Mbona mie naona hakuna hatua zinazochukuliwa kuzuia hali kuendelea na je tusemeje chama tawala kinahusika? Mbona akiuliwa kiongozi wa CMM mbona wauaji wanakamatwa mapema? Je jeshi letu la polisi linalinda viongozi wa CMM tu na sio kulinda raia na mali zake? Naomba kutoa wito kwa wanaccm watoe maelezo nchi hii inakwenda wapi na wanataka nini juu ya usalama wa raia na mali zao na uhuru wa kujiunga na chama chochote cha siasa wao wanasemaje ili kupunguza vifo na waseme hadharani ili atakaye hama ajue kinachofuata ili mtu atoe maamuzi sahihi na sio kuviziana na kuleta vifo kwa nguvu kazi na watu wanaotegemewa na familia zao.
 
Jamani ifike wakati tuwaambie wana CCM imetosha haya mauaji hayavumiliki!!!ni wazi kwa sasa CCM ndiyo inayovunja amani katika nchi yetu
 
CCM wameamua kuwarestisha in piece wote wanaoirestisha in pieces
 
walianza kumuua m/kiti wa chadema kule arumeru baada uchaguzi na sasa huyu m/kiti wa cuf kibaha vijijini, tena wauaji walimwambia sababu ya kifo ni kitendo chake cha kuhama ccm. Jamani hizi chuki za kisiasa ktk nchi yetu zimefikia hapa?. Nadhani ipo haja kwa viongozi wa upinzani kuyatafutia dawa haya matukio.

kweli mkuu,nami nashangaa matukio haya kuanzia mwanza,arumeru,na sasa kibaha yako wazi kabisa kuwa ni kuna watu wameamua kuchinja ili kuua spirit ya watu kuhamia vyama vya upinzani kwa kasi kwa kutia hofu ya kifo.sasa kosa wanaolifanya viongozi wetu wa upinzani hasa cdm chama changu ni kukaa kipya bila kutoa kauli yeyote na msimamo wao si ule wa kukakaa na waandishi wachache na kutoa kauli ya uoga uoga.tuandamane kwa amani nchi nzima ili wananchi wote wajue na mpaka wa vijijini wasikie huko kwenye nguvu zao kwa sababu ya kuishi miaka ya 47 na mataifa nao wajue.viongozi wa upinzani wawatetee tetea wanyonge na wanachama wao wanaochinjwa kama kuku.wajue hili ni pigo kubwa kwa vyama vya upinzani, itauwa kabisa spirit ya watu kujiunga upinzani ikiwa wanachinjwa na viongozi wanakaa kimya.ukiwauliza eti wananchi tuwe watulivu jeshi la polisi lifanye kazi yake.kazi yake ipi?kwani kutoa kauli ya kulaani na kutia moyo wananchi na hata maandamano ya kulaani mauaji haya watakuwa wamechochea ghasia?wao wanajua kabisa sehemu kubwa ya wananchi hawana imani na jeshi la polisi kwani limeshapoteza legacy kwa wananchi,wananchi wataendeleaje kuviunga vyama vyama vya upinzani mkono wakijua wako salama eti kwasababu polisi itawalinda.viongozi wa upinzani toeni kauli kuwapa wananchi moyo wa kuendelea kuwaunga mkono.ukimya wenu unatuvunja nguvu.hatusemi muanzishe fujo bali muonyeshe mko imara kutetea haki za wanyonge.any way mungu ndio atakayetupigania nami nasema kama kipo chama kinafanya haya wakumbuke mungu anasema damu hii wanayoimwaga ataidai mikononi mwao and one day they will pay the price kama sio wao basi watoto wao au wajukuu na hata vitukuu.na laana hii itakuwa kwao wanatuibia na wanatuchinja ila watoto wao tunaona wameanza kula laana za baba zao wanaishia kulewa mapombe,madawa ya kulevya baadae ukimwi na kansa itawamalizia waalaniwe kwa matendo yao na wazazi wao.
 
Inamaana hawa sisem wamevunja amri ya kuiba na sasa wanavunja na amri ya kuua! Mi nadhani na wao sisiem wameanzisha movement yao inayoitwa" MOVEMENT 4 KILLING ( M4K) kweli tutafika jamani kwa hali hii?
Mungu wa israel awasamehe sisiem.
 
Jamani hakuna maisha bila kifo,magamba acheni kuuwa watu.Mda wa kila m2 kufa utafika na wote hapa duniani tunapita.Tusiwahishane kufa wengine hatujajiandaa kusimama kizimbani kwenye mahakama kuu na ya haki iliyopo MBINGUNI.
 
Hivi jeshi la polis mnasubiri auwawe mwenyekiti wa ccm taifa ndo mtoe matamko iko wapi ile intelijensia yenu tuliyoishuhudia kule arusha na dodoma? mlaaniwe wote jeshi la polisi na ccm yenu
 
CCM wameshashindwa Siasa za kistaarabu sasa wanataka kila mtu ashike upanga wake ili wahepuke aibu ya kuondolewa kistaarabu wasingizie kwamba waliondolewa kwa nguvu
 
Walianza kumuua m/kiti wa CHADEMA kule Arumeru baada uchaguzi na sasa huyu m/kiti wa CUF KIBAHA Vijijini, tena wauaji walimwambia sababu ya kifo ni kitendo chake cha kuhama CCM. Jamani hizi chuki za kisiasa ktk nchi yetu zimefikia hapa?. Nadhani ipo haja kwa viongozi wa Upinzani kuyatafutia dawa haya matukio.

Inasikitisha sana,nchi hii imefika pabaya sana
 
R.I.P Mwkt. Wadau hebu tujadili hatua sahihi zanazopaswa kuchukuliwa dhidi ya ukatili huu
 
M/Mungu awalaze pema wote waliouawa, Aliyehama CCM na kuhamia CDM Arusha kauawa, Mwanza ni manusura, huko wameua..Eee Mwenye Enzi, usiyelala wala kusinzia unayaona haya yote, na hakika hutanyamaza. Uwalipe sawasawa na waliyoyatenda.:sad:
 
Hata Diwani na mwenyekiti wa CCM Tabora vijijini aliuwawa juzijuzi pia hata kule maeneo ya mkoa wa Mbeya mwenyekiti wa CCm aliuwawa. Maswala kama haya yanahitaji uchunguzi wa kina kabla tya kujaji.
Walianza kumuua m/kiti wa CHADEMA kule Arumeru baada uchaguzi na sasa huyu m/kiti wa CUF KIBAHA Vijijini, tena wauaji walimwambia sababu ya kifo ni kitendo chake cha kuhama CCM. Jamani hizi chuki za kisiasa ktk nchi yetu zimefikia hapa?. Nadhani ipo haja kwa viongozi wa Upinzani kuyatafutia dawa haya matukio.
 
Back
Top Bottom