M/kiti wa CUF Kibaha auwawa

Goheki

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
448
387
M/kiti wa Cuf kibaha ameuwawa ucku wa jana kwa kuvamia na watu wasiopungua kumi na tano wakitumia mapanga. Marehemu alihama ccm na kujiunga na cuf na kuwa mwiba mkali kwa ccm.Ijumaa iliyopita alimweleza jirani yake kuwa anawindwa kuuwawa na wapinzani wake kisiasa. source.mlimani tv.
 
Tanzania nchi yenye "amani," na "democrasia" inayosifika. R.I.P ndugu yetu
 
Ni kweli tukio hilo limetokea huko kibaha vikuge njia ya kuelekea soga kwa msabaha
 
nimeshangazwa kuona tena m/kiti wa CUF kibaha vijijini amezikwa leo na kifo chake kuhusishwa na siasa, kwani alivamiwa na watu wasiojulikana. jamanii wapi tunaelekea au ndio ukombozi unakalibia, au nini tatizo...

SOURCE; ITV NEW
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahalapema pepo Amina.Ila hawa wanaofanya haya mauwaji wajue nao ipo siku yao wema na ubaya hulipwa hapa hapa duniani.Arusha wameuwa,mwanza walitaka kuuwa wakajeruhi kwa kuwakata kata na mapanga, sasaivi wameuwa kibaha.
 
Walianza kumuua m/kiti wa CHADEMA kule Arumeru baada uchaguzi na sasa huyu m/kiti wa CUF KIBAHA Vijijini, tena wauaji walimwambia sababu ya kifo ni kitendo chake cha kuhama CCM. Jamani hizi chuki za kisiasa ktk nchi yetu zimefikia hapa?. Nadhani ipo haja kwa viongozi wa Upinzani kuyatafutia dawa haya matukio.
 
Kama kweli chanzo cha mauaji haya ni siasa basi sisi kama Taifa tumefika pabaya na tunaelekea pabaya zaidi. RIP Kiongozi
 
Back
Top Bottom