M - Gas biashara imewashinda. TBS futieni leseni hawa wapuuzi

Ruble

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
621
1,040
Kama kichwa kinavyojieleza. Wiki ya 3 inakwenda mteja nafanya kubembeleza mfanyabiashara. Natumia gesi ya hawa wapuuzi baada ya kushawishiwa na sijui wakala wao baada ya kutuunga kwenye group watu wengi. Nikauliza group la nini ndio kujua habari za M gas.

Kazi iko hapa > betri imeisha, mtungi una gas ya pesa takribani elfu 30. Napiga customer care walete technician kurekebisha wanajibu yuko njiani. Juzi nikapiga kuwatukana. Wakajibu ndugu mteja tunasikitika lakini mafundi wanashughulikia taarifa yako.

Nimeazimia kutafuta fundi anayejua kuyafungua haya majiko yao aje afungue anitolee hii takataka ninunue mtungi mwingine wa kawaida.
 
Ni huduma nzuri mnoo ya kisasa, inaondoa kazi ya kubebana na mitungi na unanunua muda wowote hata usiku wa manane
 
Hapana mkuu hakuna bomba.

Siwezi kueleza kitaalama gas inavyoingia but ikiisha unanunua kupitia namba maalum imebandikwa kwenye mtungi na kuna ka keyboard chao juu...ndio maana mdau amesema betri yake inayowasha keyboard imekufa.

Ukinunua tu inastant unaanza kutumia papo hapo.

Sijui gas inarushwaje..
Nakuitia

Meneja Wa Makampuni ni mmoja wa wadau, wauzaji, ma agent wao
Kwahio M gas wanakuletea mtungi wao wenye gas halafu ukinunua ndio unapata access ya kutumia gas?
 
Hapana mkuu hakuna bomba.

Siwezi kueleza kitaalama gas inavyoingia but ikiisha unanunua kupitia namba maalum imebandikwa kwenye mtungi na kuna ka keyboard chao juu...ndio maana mdau amesema betri yake inayowasha keyboard imekufa.

Ukinunua tu inastant unaanza kutumia papo hapo.

Sijui gas inarushwaje..
Nakuitia

Meneja Wa Makampuni ni mmoja wa wadau, wauzaji, ma agent wao
Japo sifahamu inafanyaje kazi. Lazini naweza kufikiri kwamba unapewa amtungi wenye Gesi ya kutosha ila kutumia gesi hiyo ndio inabidi ulipe upewe pass code kama Vote za LUKU.

Haiwezekani Utumie Gesi from nowhere.

Gesi ni Matter, material thing it occupies space and volume.
 
Okay Asante, bado nipo analog. Sasa gas unapataje? Kuna mabomba kama ule mradi wa TPDC?
Jamaa anazingua huyo uliyemuuliza, ipo hivi.

Hao jamaa kuna kiasi unalipa na wanakupa mtungi wao wenye connection ya mtandao, so wewe unanunua gas kulingana na pesa yako na hiyo gas ni ile uliyopewa siku unaletewa mtungi.

Kadiri unavyotumia na wao wanajua kiasi kilichobaki na ikionekana gas inakaribia kuisha kwenye mtungi wanakuja siku yoyote kabla haijaisha na kubadirisha mwingine uliojaa, ipo hivyo.

Ni wanasema "lipa kadiri ya matumizi yako"
 
Back
Top Bottom