mwakajilae
Member
- Mar 11, 2011
- 58
- 46
Mbunge mpambanaji Cecilia Pareso aliye apishwa hivi karibuni katika bunge lililopita huko Dodoma,leo ameandaliwa mapokezi makubwa wilayani Karatu,yanayoratibiwa na Baraza la Vijana la Chadema Karatu ikiwa ni hitimisho la kiapo chake cha mwisho kwa wananchi, katika safari ya kuwatumikia na kuwawakilisha.Maandamano hayo makubwa yanaambatana na msururu mkubwa wa piki piki takribani miamoja kuanzia Mto wa Mbu kuelekea Karatu kijijini aliko zaliwa.Msafara wake umeambatana na uongozi mzima wa Chama mkoa wa Arusha.Kutafanyika mkutano mkubwa wa hadhara kijijijini hapo.
Matarajio ya wakazi wa Karatu ni makubwa kutokana na ujasiri,msimamo na uzalendo ambao mara nyingi alikuwa anausimamia akiwa diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Nifaraja ndani ya Chama cha Chadema kumpata mbunge machachari anaye kwenda kuungana na Mh Halima Mdee na wengine wengi katika wabunge wa kike wanaowasha taa ya mapambano ya kuonesha uongozi pasipo kujali jinsia yao iliyokolezwa na tamaduni za mfumo dume.
Kitaaluma Mh Cecilia Paresso ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza.
Tutegemee makubwa kutoka kwa mwanaharakati huyu hivi karibuni.