Lyatonga Mrema: Wanachama TLP waliokimbia sababu ya "ukata" sasa warudi chamani

Wanamalizana nae kwa utumishi wake uliotukuka ndani ya ccm! Yaliyotokea yote ni zuga na danganya toto! MREMA ni wao ataendelea kuwa wao! Hata JK alimpa pesa za kampeni ya Ubunge ili akiumwa atibiwe na Bunge! Hongera MREMA! Ukatende haki kwenye Parole! Isiwe tu kwa matajiri ndio wanapewa hizo Parole
Kama ambavyo Lowasa ni wao
 
Haha kwa anavyoongea tu inaonyesha ameathirika kisychologia kwa alivyokua juu mpaka sasa hawez kua sawa
 
Muwe mnakukumbuka hakuna kiongozi wa juu wa siasa ndani ya upinzani ambaye hakutokea CCM, Kuanzia enzi za Mtei, mpaka Maalim seif Zanzibar. Kama ni malipo ya utumishi ndani ya CCM basi tusubiri wenge walipwe pia
zitto na mbowe hawajawahi kuwa CCM
 
Mrema kachoka!!! Angepumzika tu mzee wa watu.
hahaha Mrema kachoka ?? mbona hamkumuona Lowasa, Sumaye au Kingunge na kuwaambia wamechoka wapumzike kwa muktadha huu. hata Kingunge alikuwa anasema ccm imeishiwa pumzi. hahahaha. siasa kweli si...asa. ni vitu vya kufikirika.nyani haoni kundule wajameni
 
Mtu akiendelea kuwa mwanachama wa chama cha upinzani kinaitwa TLP halafu akaniambia yuko timamu kiakili itabidi niende nikapimwe maana labda mie ndio siko timamu
unakumbuka maneno ya mchungaji Msigwa.?? "atakayemshabikia Lowasa inabidi akapimwe kama ana akili nzuri" kwa maana nyingine wote washabiki wake hawana akili timamu. sijui labda tumuulize Msigwa alimaanisha nini au alikuwa anatania tu. lazima tukumbuke statement kama hizi huwa zina uhai na valid wakati wowote katika maisha, hiyo ni kulingana na imani zetu. tamko huwa linaumba. linatengeneza ukweli kama lilivyotamkwa. tujihadharani sana na siasa za majitaka wajameni
 
View attachment 366884

Kwa mara ya kwanza baada ya Uteuzi wa kuwa Mwenyekiti wa Parole,Augustine Lyatonga Mrema ameongea na waandishi wa Habari.Mreama anasema ni wakati muafaka kwa wanachama wa TLP waliokimbia chama kwa sababu ya "ukata" wa Mwenyekiti wao,amewasihi wanachama kurudi na kukijenga chama kwani kwa sasa yeye kama mwenyekiti atakuwa na pesa hata za kumlipa "secretary".

Mrema anasema anamshukuru sana Rais kwa kumteuwa na kumpa kazi,kwani watu walishaanza kusema amefulia.Amenukuliwa akisema "Kuna watu wanaa sana,wanaleta unaa eti siwezi kutumikia chama na nafasi ya Uenyekiti wa Taifa wa Parole,mbona Mbowe ni mwenyekiti Chadema na mbunge wa Hai?Mbatia alikuwa Mwenyekiti wa NCCR na akapewa ubunge na Kikwete,hata Magufuli ni Rais,Amiri Jeshi mkuu,mkuu wa inji na lalaa laaaa laaa,mbona Rais ana vyeo vingi hamumuulizi mnanionea tu mimi?,kwani mi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Parole na TLP kuna shida gani?We mwandishi vipii bwana?acheni unaaa...Mimi nabeba vyeo vyote viwili,ntakuwa mwenyekiti wa TLP wa Taifa na wa Parole,si nimechaguliwa bwana!!!"

Mrema anasema kwanza Rais Magufuli kakionea huruma chama cha TLP na wanachama wake kwa kumpa yeye uenyekiti wa Parole,sababu TLP haikuwa na mbunge wala ruzuku,hivyo yeye kama mwenyekiti hakuwa na gari na hata posho;Kwa cheo hicho sasa Yeye kama Mrema anapata posho,nauli na hata gari,hivyo atapata pesa ya hata kumlipa karani wa kuchapa barua za ofisini.Amesisitiza kuwa cheo hicho hajapewa kama hongo,maana Rais Magufuli anajuwa utendaji wake na ndio maana kwenye kampeni za Ubunge Rais alisema watu wa Vunjo wamchague Mrema ili awe mbunge wao.Hivyo watu waache "unaaa" wa kumfuatilia fuatilia wakati yeye kateuliwa na Rais
Kwa hiyo ukata umeisha au wapi huko anapoenda kukwapua mihela? Au ameshapata wadhamini?
 
Hata aliyemteua akisikia haya kama ni ya kweli ataumia
 
Mtu akiendelea kuwa mwanachama wa chama cha upinzani kinaitwa TLP halafu akaniambia yuko timamu kiakili itabidi niende nikapimwe maana labda mie ndio siko timamu
Zamani tulikuwa tunasema hivyo kwa CUF.
Badae tukahamia ACT.
Hahahaaaaaaa
Msigwa yeye alisema hivyo kwa Lowassa.
TAIFA LA WANAFIKI.
 
Back
Top Bottom