Tatizo mnashindwa kuielewa CUF ,CUF demukrasia ipo na jambo zuri kuwa hawapapatikii viongozi ,wala hakuna anaebembelezwa ,wanakuja wanaondoka ,ila Chama wanakiacha pale pale ,hebu jiulizeni wangapi wamebwaga manyanga na bado CUF inapeta ,haijatetereka wanachokidai CUF ni uchaguzi wa haki hakuna jingine ,wanachokidai CUF ni Katiba Mpya ,wanachokidai CUF ni Tume mpya ya Uchaguzi ,wanachokidai CUF ni mahakama Huru ,wanachokidai CUF ni viongozi kutokuwepo juu ya sheria.
Hili linapatikana katika Katiba mpya ,sasa tukubalini kuwa CUF iendelee na viongozi wenye busara ila siku ikipata kiongozi mvuta bangi basi mjue amani itatoweka nchi hii na kuwa kumbukumbu na wafuasi wa Sultani CCM watatafuta pa kujificha lakini wakuwa smoked out popote watakapokimbilia.Huwakuti CUF kupigia makelele hujuma za ufisadi kwani wanajua kwa hapa tulipo itakuwa tunapoteza nguvu zetu na hakuna ambalo litamuathiri mtawala CCM zaidi ya kubadilisha na kuweka uoza mwengine. Hayo mambu yakikubalika kubadilishwa ndipo hapo kuwanadi mafisadi kutapata nguvu za kisheria na sheria kufuatwa na wahusika kuwajibishwa kisheria sio mtu anajiuzulu ndio habari kwisha.
Nchi imetulia na kuvumilia mengi yafanywayo kibabe na Sultani CCM ,CUF hadi hivi sasa au leo ni Chama kinachoshikilia wananchi wengi na kimeweza kuwaweka chini ya control yake ,nasema tena siku akitokea kiongozi wa CUF na kuamua kuanzisha mapambano na serikali basi yatakuwa mapambano ya kweli sio mchezo na hilo CCM wanalielewa ,wanajuwa kuwa CUF ni Chama hatari kwa ufisadi wao ,maana ukishakuwa na wananchi wanaokusikiliza na waliotayari kwa lolote basi wewe ni wa kusikilizwa na kuheshimiwa na kama hufanyiwi hivyo iko siku utafungulia wananchi wapambane na serikali iliyopo madarakani ,hilo sio jambo la mchezo ni roho kwa roho,kutakuwa hakuna usalama wala jeshi ni mapambano tu,ambush kila kona ,maana itakuwa sio piga tajame bali ni piga ni kupige.
Hawa viongozi hawatakuwa na uhuru tena wa kutembea na mashati na tai ,maana uvumilivu wa wananchi utakuwa haupo tena anytime anaweza kujitolea mwananchi na kufanya kweli tumeona ndogondogo ambazo zimetokea mbele ya mtu anelindwa na mabunduki na walinzi kanzu mmoja kavamiwa miguu tukio la pili kalambwa mtu kibao ,sasa hatujui tukio la tatu litakuwaje ,we wacha wafuasi wa sultani wacheze na amani wakiambiwa badilisheni hiki ,hatutaki wakiambiwa tunataka hiki hawataki basi walitakalo limeanza kuonekana kidogokidogo nalo ni kwa wananchi kushindwa kuvumilia na hapo inakuwa rahisi kuwaamuru kwa lolote lile.Ikiwa wafuasi wa CCM wanachukua chao mapema naona zamu ya wananchi nao kuwahi kulinda chao imekaribia.