Lwakatare na Ubunge what is the connection ?

Lwakatare na Ubunge what is the connection ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,919
Wadau naomba msaada wa kueleweshwa .

Lwakatare ametokea kuhubiri Mbezi sijui Mikocheni .Sikuwahi msikia katika harakati za kutetetea ana kupinga lolote .Niliwahi msikia katia biashara tu na hasa mashule na biashara za kanisa lake.

Ghafla akawa Mbunge kwa ticket ya CCM kwa kuteuliwa .Sijajua ndugu Rais alitumia kigezo gani japokuwa ni maamuzi yake yeye anaye wateua.

Nikaanza kushagaa sasa Siasa na Dini inakuwaje .Ghafla huyu mama amekuwa na tuhuma yingi katika jamii .Kuwadhurumu mishahara watumishi wake , kuiba umeme , na sasa anatajwa katika madawa ya kulevya .

Huyu mama bado najiuliza ilikuwaje hadi akawa mbunge na akaamua kuwatumikia ma bwana wa 2 yaani Bunge pesa za walala hoi na Kanisa anakokusanya zaidi pesa za walio kata tamaa?
 
Ndege wafananao mabawa ndio warukao pamoja!Ndugu mbona unaumiza mgongo wako bure kuangalia ya uvungunguni ili hali yapo wazi sebuleni?
 
Umesahau kwamba mafisadi na wauza unga wote wako CCM?, umeshajiuliza Mh. Rais alishapewa majina ya wauza unga lakini hadi leo kimya! Jiulize mtu kama Ndesamburo angekuwa anafanya biashara ya unga au hata tuhuma kama angekuwa bado yuko salama. Huyo Lwakatare ni mmoja kati ya wengi tu ambao wako CCM na wanafanya biashara hizo haramu na hawaguswi na wana nafasi kubwa, kumbuka meno ya tembo, kusafirisha wanyama hai, EPA n.k, sasa ukiwanyima nafasi wote hao CCM si itakufa?
 
Wadau naomba msaada wa kueleweshwa .Naomba walio serious pekee ambao wanaweza kujadili ndiyo tujadili .Natoa angalizo baada ya JF kuvamiwa na LT badala ta GT .Lower thinkers wameongezeka sana na kuhabaribu mijadili mingi .Lwakatare ametokea kuhubiri Mbezi sijui Mikocheni .Sikuwahi msikia katika harakati za kutetetea ana kupinga lolote .Niliwahi msikia katia biashara tu na hasa mashule na biashara za kanisa lake .Ghafla akawa Mbunge kwa ticket ya CCM kwa kuteuliwa .Sijajua ndugu Rais alitumia kigezo gani japokuwa ni maamuzi yake yeye anaye wateua.Nikaanza kushagaa sasa Siasa na Dini inakuwaje .Ghafla huyu mama amekuwa na tuhuma yingi katika jamii
.Kuwadhurumu mishahara watumishi wake , kuiba umeme , na sasa anatajwa katika madawa ya kulevya .Huyu mama
bado najiuliza ilikuwaje hadi akawa mbunge na akaamua kuwatumikia ma bwana wa 2 yaani Bunge pesa za walala hoi na
Kanisa anakokusanya zaidi pesa za walio kata tamaa?

Siku hizi kuna watu wengi wenye tamaa ya pesa za haraka bila kujali kama zinapatikana kihalali au la. Watu hao wamevamia siasa na makanisani kama kinga ya uovu wao. Kwa wale wanaokimbilia makanisani utawasikia wakijiita mitume, manabii,askofu n.k. Makanisa yanayomilikiwa na watu binafsi (Si taasisi) yanazidi kushamiri.Sadaka zinazotolewa na waumini wanaorubumiwa huingia kwenye mifuko ya watu binafsi. pia wengi wao wameenda mbali hadi kufanya utapeli ili kuwarubuni waumini wao waonekane wana uwezo wa kuponya na kufufua wafu. rejea ishu ya misukule, mchungaji aliyeumbuliwa na changudoa nchini Kenya na visa vingi vya utapeli. Biashara haramu ya dawa ya kulevya inafanyika na watu hawa kwa kinga ya siasa na dini. Ili kukomesha tabia hii inayoharibu jamii yetu, ni lazima wananchi wawe wa zalendo na kushiriki vita hii kwa kuwataja watu wote hadharani wanaojihusisha na matukio haya maovu.
 
Mama rwakatale ni mbunge wa viti maalum sio wa kuteuliwa,na alianza kuingia bungeni nadhani baada ya kifo cha amina chifupa (naweza kusahihishwa) yeye ndo alim replace

Kuhusu connection nadhani watu wa aina yake wapo wengi tu ndani ya CCM
 
Wadau naomba msaada wa kueleweshwa .Naomba walio serious pekee ambao wanaweza kujadili ndiyo tujadili .Natoa angalizo baada ya JF kuvamiwa na LT badala ta GT .Lower thinkers wameongezeka sana na kuhabaribu mijadili mingi .Lwakatare ametokea kuhubiri Mbezi sijui Mikocheni .Sikuwahi msikia katika harakati za kutetetea ana kupinga lolote .Niliwahi msikia katia biashara tu na hasa mashule na biashara za kanisa lake .Ghafla akawa Mbunge kwa ticket ya CCM kwa kuteuliwa .Sijajua ndugu Rais alitumia kigezo gani japokuwa ni maamuzi yake yeye anaye wateua.Nikaanza kushagaa sasa Siasa na Dini inakuwaje .Ghafla huyu mama amekuwa na tuhuma yingi katika jamii .Kuwadhurumu mishahara watumishi wake , kuiba umeme , na sasa anatajwa katika madawa ya kulevya .Huyu mama bado najiuliza ilikuwaje hadi akawa mbunge na akaamua kuwatumikia ma bwana wa 2 yaani Bunge pesa za walala hoi na Kanisa anakokusanya zaidi pesa za walio kata tamaa?

Kuna mambo mengi ambayo yananisababisha niwe na tashwishwi kuhusu huyu mama, haswa baada ya chama chake kuanza kutumia shortcut ya kutishia watu kwa kulipuwa watu mikutanoni, lakini suala la kuteuliwa yeye hakuteuliwwa na raisi, alipitia katika mchakato wa kawaida wa uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika chama chake!
 
Ni Rwakatare sio Lwakatare.
Rwakatare-CCM
Lwakatare-CHADEMA

Yaani kakosea jina halafu anajiita GT na kuomba sijui nini bila kujicheki.

embu peleke u GT huko, wengi wasio ma GT ndio wanajiita hivyo kulalamba kumbe ni ma xxxxxxxl LT.
 
Wadau naomba msaada wa kueleweshwa .Naomba walio serious pekee ambao wanaweza kujadili ndiyo tujadili .Natoa angalizo baada ya JF kuvamiwa na LT badala ta GT .Lower thinkers wameongezeka sana na kuhabaribu mijadili mingi .Lwakatare ametokea kuhubiri Mbezi sijui Mikocheni .Sikuwahi msikia katika harakati za kutetetea ana kupinga lolote .Niliwahi msikia katia biashara tu na hasa mashule na biashara za kanisa lake .Ghafla akawa Mbunge kwa ticket ya CCM kwa kuteuliwa .Sijajua ndugu Rais alitumia kigezo gani japokuwa ni maamuzi yake yeye anaye wateua.Nikaanza kushagaa sasa Siasa na Dini inakuwaje .Ghafla huyu mama amekuwa na tuhuma yingi katika jamii .Kuwadhurumu mishahara watumishi wake , kuiba umeme , na sasa anatajwa katika madawa ya kulevya .Huyu mama bado najiuliza ilikuwaje hadi akawa mbunge na akaamua kuwatumikia ma bwana wa 2 yaani Bunge pesa za walala hoi na Kanisa anakokusanya zaidi pesa za walio kata tamaa?

Ndugu Lunyungu,

Uongozi una mambo mengi. Ukitaka kuwa na mafanikio katika uongozi kuna mbinu nyingi za kufanya, kutegemea na aina ya mafanikio unayotaka. Nitakupa machache:

1.Kama unakusudia kuwa salama na unaogopa challenges utakimbilia kujaza maswahiba wakuzunguke ili wale unaowaogopa wasikukaribie kwa urahisi. Daima utawapa maswahiba kile roho zao zinapenda ili wakutetee hata kama unachemka.

2. Kama unajua kuna jamaa wanaweza kugeuka maadui zako, utajitahidi siku zote wawe rafiki zako. siyo kwa kuwa unajilazimisha kuwapenda ila kwa kuwa inakuwa ni rahisi kuwa monitor.

3.Kama unajua kuna mtu/kundi linakupinga na huna uwezo wa kushinda vita, utakimbilia kuomba muafaka kwa kjiunga nao hata kama mambo yao yanakukereketa ndani. Kwa wajanja hiyo huwa ni nafasi ya kujipanga na kufanya shambulizi la kushtukiza kwa ndani wakati ukiwa na nguvu za kutosha. Ila ukiwa poyoyo huwa ndo umejizika rasmi.

4.Ukiwa Kiongozi bora utaanza kujenga uongozi wa kujiamini na kuwa na wasaidizi wa haja bila kujali ni maadui au marafiki, kigezo ni kuwa wanaweza kutekeleza majukumu na malengo wanayowekewa na wanayojiwekea. Kiongozi wa aina hii haogopi changamoto za ndani wala nje kwani hataleta jambo lisilo na maslahi kwa jamii yake na hivyo upinzani atakaopata utakuwa ni katika kuboresha kile alichokianza. kwa hiyo kwa kuwa lengo lake huwa ni ustawi wa jamii yake atafurahi kila anapokutana na challenge itakayopelekea kuboresha hoja kwa maendeleo ya jamii.

Ndugu Lunyungu, Ukiangalia serikali yetu, matokeo yake kiutendaji na hasa ukijikita kwenye hii hali ya viongozi kuboronga hadharani( kama Waziri Nchimbi, IGP, DPP, Waziri wa elimu na Rais mwenyewe) utagundua kuwa serikali hii imejaa marafiki wa karibu wa rais, ukiongelea wizara na idara nyeti. Marafiki ambao wengine wamekuwa ni tatizo la wazi na kwa kuwa ni marafiki ameshindwa kuchukua hatua yoyote. Uteuzi wa wengine waliobaki umekuwa ni wa kujaza wenzetu zaidi. Eitha wale ambao walitusaidia kwa hali na mali na tumekosa nafasi ya kuwapa kama kulipa fadhila, ama kwa kuwa ni watu ambao tunajua hawajui kujitegemea kimawazo hivyo itakuwa rahisi kuwaendesha tunavyotaka.

Tatizo kubwa ni pale kiongozi anapokubali sapoti ya watu waovu na akakubali kulipa fadhila kwa watu hao! Matokeo yake ni kununuliwa na kukosa uamuzi, hasa inapokuja kutolea uamuzi jambo litakaloingilia maslahi ya hao jamaa. Na hilo pamoja na mengine ni kati ya matatizo ya kuwa na serikali ambazo ni zao la corruption.

Kutoka hapo nadhani unaweza kuona ni kwa nini mchungaji gani ameteuliwa kuwa nani, au ni kwa nini kina nani wamekuwa nani pamoja na kuwa hawawezi kazi na hawafanywi lolote na yeyote!
 
Kuna mambo mengi ambayo yananisababisha niwe na tashwishwi kuhusu huyu mama, haswa baada ya chama chake kuanza kutumia shortcut ya kutishia watu kwa kulipuwa watu mikutanoni, lakini suala la kuteuliwa yeye hakuteuliwwa na raisi, alipitia katika mchakato wa kawaida wa uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika chama chake!

Mchakato wa kawaida katika chama?.... hivi kuna mchakato wa aina gani ndani ya chama kinachoongoza kwa rushwa mpaka ya mchana? Mchakato huo unakuwa ni wa aina gani unaoleta viongozi wasio na sauti ya kukemea ufisadi? Mchakato huo unazingatia nini kama wanaozaliwa katika mchakato huo ni wabovu wote na wale wachache wanaotokea kugeuka na kuwa waadilifu kama wa Bukoba wanapigwa vita na viongozi wote mpaka mwenyekiti wa taifa? Mchakato?

Nadhani tukubaliane tu kuwa michakato yote itafeva kuwa na watu wa aina moja. Hivyo kama Mwenyekiti ameruhusu ubovu watakuwa wabovu wote. Kama Rais ameteua timu Fisadi, wote chini yake wataimba wimbo wake. Sidhani kama unadhani kuwepo na mchakato ndani ya CCM kwa sasa kunalenga kuwa na uadilifu wowote. Kwangu mchakato wa aina yoyote ndani ya system corrupt unalenga kuchuja wale tusiowataka na kuweka wanofanana na mambo yetu! Sasa wewe tafakari mwenyewe "mambo yetu" ndani ya CCM ni mambo ya aina gani.
 
Ndege wafananao mabawa ndio warukao pamoja!Ndugu mbona unaumiza mgongo wako bure kuangalia ya uvungunguni ili hali yapo wazi sebuleni?

Haaaaaah haaaaah birds of same feathers always fly together, Mkuu nae anabiashara hizo hizo ndo mana anashindwa ku take action kwa idd azzan,pole tz,watz tubadilike 2015 tuweke cdm maovu mengi yatafichuliwa
 
Mama rwakatale ni mbunge wa viti maalum sio wa kuteuliwa,na alianza kuingia bungeni nadhani baada ya kifo cha amina chifupa (naweza kusahihishwa) yeye ndo alim replace

Kuhusu connection nadhani watu wa aina yake wapo wengi tu ndani ya CCM

Alimreplace yule naibu waziri aliefia Ruvuma, jina sikumbuki! Na huyu mama alianza harakati zake za siasa Morogoro wakamwaga chini kwenye kura za maoni! Baada ya hapo JK akamteua
 
Yeye ndio mchungaji wa kwanza kutangaza jk ni chaguo la Mungu 2005.

ukitaka mambo yako yanyooke sifia ccm hata kama jambazi utaitwa mheshimiwa.!!
 
Alimreplace yule naibu waziri aliefia Ruvuma, jina sikumbuki! Na huyu mama alianza harakati zake za siasa Morogoro wakamwaga chini kwenye kura za maoni! Baada ya hapo JK akamteua

Salome Joseph Mbatia (27 Desemba 1952 – 24 Oktoba 2007) - Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
 
Back
Top Bottom