Lwakatare kugombea tena ubunge bukoba mjini 2015?

Lwakatare kugombea tena ubunge bukoba mjini 2015?

je wewe ni mwana bukoba? Tusubili wenyeji waseme wenyewe

kwani thread ni kwa ajili ya wanabukoba tu ! Angetanaibisha basi kwenye kichwa cha habari kwamba usichangie kama si mwanabukoba
 
Kwani umeambiwa jela ndio makazi yake ya milele?kiwango chako cha kufikiri ni kidogo sana pole sana.

Wewe mwenye kiwango kikubwa umenizidi nini fal... Watu wanakula life wewe unakesha na keyboard
 
Kimsingi Lwakatare hana jipya
tena na ushawishi wake umepungua sana kwa wapiga kura wa
Bukoba,,,,,rejea moja ya mikutano alipokuwa Lwamishenye alipotoa kauli
ya kukata tamaa na kusema watu wa Bukoba ni wanafiki kuwa walionyesha
kumuunga mkono kwenye mikutano na kura wakampa Kagasheki.

Anayetajwa tajwa kuwa mbadala wa Lwakatare ni Gration Mukoba ingawa bado
yuko kimya

kuna diwani machachari wa CUF anaitwa Bigambo, huyu jamaa anakubalika sana kwasasa! Kwa wanaomjua Bigambo ndo alikuwa meneja mkuu wa kampeni wa Lwakatare na ndiye aliyemweka Lwakatare juu kisiasa
 
Lwakatare ameshachafuka mno. Hayo mambo ya ubunge inabidi aachane nayo tu...

kwani amechakuliwa ni kipi? Je umemwagia tope lipi? Mbona kama ni tope la Ugaidi tayari imeshalifuta sasa una tope lingine limeandaliwa na Lumumba? Kazi mnayo hapo Lumumba
 
Lwakatare ameshachafuka mno. Hayo mambo ya ubunge inabidi aachane nayo tu...

mkulu ndio amechafuka zaidi imefikia hatua hata ya kuhongwa suti?ingelikuwa mtu makinia meshaachia ngazi lakini anavyoonekana anauchu wa madaraka hata kufikiria hilo hana,yy anahongwa suti unafikiri wenggine watahongwa nini?
 
Entare, Engaju , etc Wilfred Muganyizi Lwakatare ambaye ni kipenzi cha wana Bukoba mjini na Kagera kwa ujumla anaaswa na wenyeji wa mji huo kusimamisha tena jina lake katika uchaguzi mkuu ujao.

Lwakatare ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa usalama CHADEMA Taifa na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera , amepanda chati gafla na kukua zaidi kisiasa baada ya kuzushiwa kesi zisizo na tija. Jambo hilo liliwaumza sana wana Bukoba na wengi wao wameapa kumrudisha Bungeni kwa gharama yoyote ile.

"Lwakatare bado yupo Lupango Segerea lakini kwa kudra za mwenyezi Mungu tunatarajia kuwa atatoka tu" haya ni maneno ya afisa mwandamizi katika halmashauri ya manispaa Bukoba mjini. Watu wameumia sana kuteswa kwa Lwakatare, na sisi kama watu wake wa Karibu tunamuomba kwa heshima zote akubali kurudisha jina lake na tunaahidi kumrejesha Bungeni.

Swali, Je? Lwakatare atakua tayari kugombea tena ubunge katika jimbo hili la Bukoba Mjini? Je nafsi yake bado inamsukuma kusimamisha jina tena pamoja na mateso anayoyaata huko Segerea?

Its just the matter of time, lets wait and see.
akiweka jina lazima atashinda ubunge maana Lwakatare ni kama Lema kwa Arusha
 
Kaa kimya kuliko kuchangia utumbo kama kawaida yako!
Mkuu, hoja yako uliyoileta hapa jamvini ni nzuri tu, ila lingekuwa ni jambo la busara kujenga hoja zenye nguvu kuliko kutumia nguvu nyingi kulazimisha mtizamo wako uwe ndiyo the best, ya nini unaweweseka? Umeleta mada hapa JF tujadili, kwa lengo la kubadilishana mawazo tena yenye kujenga! Now you are forcing people to speak what is within your mind! Unadiriki kumwambia mtu akae kimya ili wana Bukoba waongee? So, you mean huu uzi umeuleta kwa wana Bukoba pekee? Ama kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake...! Pole sana kwa mawazo yako chakavu!-
 
Mimi ni kiongozi wa chama wilaya jirani, tunamuandalia mapokezi yatakayowapukutisha magamba! lakini suala la kugombea bado muda upo tutalichukulia kwa umakini mkubwa pamoja na kuwa dalili zote zinaonyesha jimbo hilo haliwezi kurudi Ccm. Siasa za Bukoba ni ngumu sana wasiozijua wanaziona kawaida. Sisi wenyeji tuna vipimo vyake na kwa sasa vinaonyesha jimbo hilo kurudi Ccm ni sawa na jua kuwaka usiku ingawa muda bado upo na mambo yanaweza kubadilika.
 

kwani thread ni kwa ajili ya wanabukoba tu ! Angetanaibisha basi kwenye kichwa cha habari kwamba usichangie kama si mwanabukoba
Mleta mada hii awali niliona ana mantiki nzuri tu! Ila kwa huu upuuzi alioanza kuuingiza, sidhani! Ina maana tusiokuwa wana Bukoba tusichangie? Sasa mbona hakutanabaisha before? Hii mijitu ya namna hii sijui tutaibadilije! Ni tatizo.
 
Back
Top Bottom