Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Kwa huu utendaji kazi na uwajibikaji wako kama bado kuna kitu chama chako kinategemea toka kwako katika kulitetea jimbo ifikapo 2020 basi kimekwisha, umefeli.
Umekuwa "alama" kubwa sana ya kufeli kwa CDM na Ukawa kwa ujumla jimboni, umeshindwa kabisa kunyumbulika. Hata kuvaa viatu vya mtangulizi wako H. Kagasheki imekuwa mtihani mkubwa kwako, umekwisha na umefeli mheshimiwa.
Hizi ni miongoni mwa ahadi zako 2015; soko kuu, soko la kashai, stand ya mabasi n.k lakini hadi leo hii huna hata jiwe la msingi la mradi wowote kati ya hii, bado tu umebaki kwenye idea (how to start), umekwama. Take off itaanza lini, utamaliza lini, hivi havina majibu tena. Hata ile Bumdeco uliyoandaa hata ukawaita wadau waje wakusaidie kimawazo na ki mbinu nayo leo haikuamini tena, umekwisha, umefeli.
Ukiachia ahadi zako za miradi mikubwa, hata shughuri ndogo ndogo nazo za kijimbo na manispaa zimekushinda, umekwama. Barabara za mjini ni mashimo, mji hauna ruti za mjini, taa za barabarani hazipo, mitalo imeziba, kila kona ni tope na madimbwi mji mzima, n.k. umekwama, umefeli.
Mikutano iliyozuiwa ni ile ya kuongea katika eneo lisilo lako, wewe leo hata kuandaa ile ya jimbo lako ukaongea na wana jimbo wako imekushinda, imebaki ndoto. Sugu kule Mbeya kaongea na wanajimbo wake hivi juzi juzi tu, hivyo wewe kushindwa kuandaa mikutano isiwe tena eti imezuiwa ama unazuiwa bali ni udhaifu wako. Umekwama na umefeli mh.
Labda kuna jingine tusilolijua lakini kwetu sie, kwa vile ilo hatulijui basi tutabaki tunakuona hivyo, na tutaendelea kukuuliza vile vile. Kulikoni mheshimiwa, lile jimbo ambalo ni jimbo lako kwa kuchaguliwa, vipi umemkabidhi nani?