Lusinde (CCM-Mtera) apendekeza watwangane kwanza Bungeni


sidhani kama kweli walimchagua yule jamaa...inawezekana ccm waliamua kumumaliza mzee wa watu baada ya kumtumia na kumchoka!!! anaongea matapishi kwa kweli!!!
 
Kazi tunayo mwaka huu! Kama CCM ina wabunge wa aina hii wengi basi nchi itaendelea kuwa chini ya mafisadi kwa miaka mitano
 
Kazi tunayo mwaka huu! Kama CCM ina wabunge wa aina hii wengi basi nchi itaendelea kuwa chini ya mafisadi kwa miaka mitano

kazi iliyobaki ni kufanya mazpinduzi kwa kutumia nguvu ya umma tu!!! tuungane tuweke mikakati!!!!!!
 
hawa c ndio wale wabunge makuwadi wa EL. Walikuwa 123, wameingia bungeni 61
 
Nawaonea huruma wananchi wa mtera na nyuma zao za udongo na nyasi zilizoshindiliwa na udongo. Ni bora wangemwacha mzee malecela aendelee kuwa mbunge wao kuliko huyu *****... Hivi hawa jamaa wanaenda bungeni kuwakilisha wananchi wao au kuwakilisha serikali!!!??? Nadhani bado hawajui wajibu wao kama wabunge na wanaenda sababu hawana njia nyingine ya kupata kipato kizuri zaidi ya ubunge...

***** lusinde mtera ndio chanzo cha umeme lakini umeme unapatikana pale mtera tanesco station tu, chipogoro, champipuru etc kote ni giza na hazizidi hata kilomita 30 toka power station but kwako sio issue!!??

Shame on you...
 

Napendekeza kutokana na hoja ya huyu mheshimiwa moja ya sifa za kuwa mbunge sasa itakuwa lazima mtu awe amepitia self defence. Hawa ndio wa wakilishi wa chama kikongwe na tunachokitegemea kitupe muongozo wa nchi, kazi kwelikweli. Mtu anajipendekeza kwa mtu mpaka anamuona mnafiki na kumdharau.
 

ulitegemea la ziada kutoka kwa mhitimu wa darasa la saba.... hapo bado yule wa Sumbawanga hajaongea na Lakairo....
 
Haya Mbunge wa darasa la saba huyo... sasa watanzania tumemchague tunatarajia awe na upeo kuliko darasa la saba la UPE? Waingereza wanamsemo, Nguruwe ni nguruwe tu hata umpake vipi lipstik atabaki nguruwe tu!
 
Nashangaa Mh. Spika Mama Makinda kwa nini hakutoa adhabu kwa huyu Mbunge wa CCM Bw. Lusinde!

Hivi kanuni za bunge zinasemaje kuhusu matamshi ya namna hii bungeni?
 
Cdm nawashauri wasimamishe mgombea jimbo la mtera mwk 2015 kwan watu hawampendi, mara nyingi ccm huwanunua wagombea wa ubunge ili wasigombee. Mm ni mkazi wa huko, hata anadaiwa kuwa malecela alikuwa ananunua wagombea wengne na kujitoa ktk hatua za mwisho? Ccm hata dodoma wamewachoka, mm napita
 
Jamani jamani!! Mkamateni huyo kiazi mumpeleke hapo Milembe akatibiwe maana inaonesha akiwahiwa anaweza kupona.
 
Kule kwetu jimbo la Mbozi East tunaye mdai posho Zambi G. Hata hajuwi kama kwenye tarafa yake ya Igamba kuna mgodi wa makaa ya mawe maana hata hajawahi kukaa angalau na wananchi wanaouzunguka mgodi wajuwe wanafurusa gani za kuwasaidia kutokana na kuwepo kwa ule mgodi. Weupe wanaishia kubeba mchanga na kutokomea nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…