Lukuvi: Ni kosa kisheria shamba kulikata na kuligeuza viwanja

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,058
23,510
Habari ndio hiyo /
Chanika,Mbezi,Kigamboni,Mkuranga na kwingineko!
-hili lisipozingatiwa upo uwezekano wa kujenga tandale nyingi kila kona ya nchi.
 
Hii pia haiwezekani,mamilioni ya watu wananunua mashamba kisha ndo wanajenga,sasa sijui watabomoa au
 
Habari ndio hiyo /
Chanika,mbezi,kigamboni,mkuranga na kwingineko!
Umegusa ndipo,hayo maeneo aisee ndio mchezo uliofanyika.
Ila kuna utaratibu wa kuhaulisha Ardhi kwenye matumisi,kutoka Commercial Plots kuwa Residential Plots ni kitu cha kawaida na kipo kisheria.
Nahisi mleta uzi umeleta juu,lazima atakuwa ametoa ufafanuzi,hawezi kuweka juu juu namna hiyo.
 
lakini inabidi aangalie na idadi ya watu wanavyozidi kuongezeka. kama planning haiko vzuri watu tutaishi wapi? yeye anaangalia mashamba lakini haangalii population ya watu hasa kwenye miji mikubwa tanzania kama dar es salaam. zamani huko mbezi kote kulikua mashamba. ata tabata kulikua mashamba zamani yote yalikatwa vipande watu wanaishi.
 
Sidhani kama kuna tatizo kwa hao wanaokata na kufanya viwanja ikiwa wamepitia Ardhi na kufata utaratibu wote mpaka kupewa HATI, Mana wengi wao hukata na kuvitafutia hati na kuuza, hawa nadhani watakuwa salama mana ardhi hawatoi hati kwa eneo lenye plan tofauti na ramani ya mjini, kama sharia imefatwa wako salama(TUKIACHA WALE WALA RUSHWA WANAOJITOLEA OVYO HATI) ila pole kwa wale walokatiwa kwa serikali ya kijiji halafu kajenga hata kwenda ardhi kucheki eneo ni vipi hakwenda.
 
Habari ndio hiyo /
Chanika,mbezi,kigamboni,mkuranga na kwingineko!

Umepata kusikia Miradi ya Plots 20.000/= Kigamboni -Kisota na Kibada?
Unajua kuna watu bado wana Kesi na Wizira/Halmashauri kwa kutoafikiana malipo kwenye uwekezaji walioufanya kwenye maeneo waliyokuwa wanamiliki kama mashamba na kugeuzwa kuwa Plots?

Ni eneo gani Tanganyika hii ambayo siyo shamba na linawakaazi?

Ebu weka hiyo vizuri hiyo habari yako tumweewe Lukuvi vizuri !


Mjimpya wa Kigamboni chini ya Wizara yake ummeishiwa wapi?


Uanzishwaji wa mji mpya wa kigamboni star tv live
31 Dec 2015
 
Umegusa ndipo,hayo maeneo aisee ndio mchezo uliofanyika.
Ila kuna utaratibu wa kuhaulisha Ardhi kwenye matumisi,kutoka Commercial Plots kuwa Residential Plots ni kitu cha kawaida na kipo kisheria.
Nahisi mleta uzi umeleta juu,lazima atakuwa ametoa ufafanuzi,hawezi kuweka juu juu namna hiyo.
Nilivyoelewa suala hapa ni kugeuza shamba na kulikatakata vipande na kupata viwanja kienyeji na kisha kuvitumia viwanja hivyo au kuwauzia watu wengine. Hii ipo sana maeneo mengi ambapo wamiliki au wajasiriamali wengi wamekuwa wakinunua mashamba na kisha kupima viwanja vidogo vidogo kienyeji kama vya 20sqm kwa 20sqm n.k. kwa kutumia kamba na pengine kuweka vijibarabara vya uongo na kweli. Kwa kufanya hivyo watu hawa wamekuwa wakivuna mapesa mengi kwa wahitaji wa viwanja vya kujenga pasipo kuhusisha watu wa mipango miji na ardhi katika halmashauri husika ili kuweza kujua mipango hasa iliyopo ya matumizi ya ardhi katika sehemu hiyo.

Hii ni tofauti na uliyosema ya kubadili matumizi ya commercial plots (kama PLOTS) kuwa residential plots.
 
Nilivyoelewa suala hapa ni kugeuza shamba na kulikatakata vipande na kupata viwanja kienyeji na kisha kuvitumia viwanja hivyo au kuwauzia watu wengine. Hii ipo sana maeneo mengi ambapo wamiliki au wajasiriamali wengi wamekuwa wakinunua mashamba na kisha kupima viwanja vidogo vidogo kienyeji kama vya 20sqm kwa 20sqm n.k. kwa kutumia kamba na pengine kuweka vijibarabara vya uongo na kweli. Kwa kufanya hivyo watu hawa wamekuwa wakivuna mapesa mengi kwa wahitaji wa viwanja vya kujenga pasipo kuhusisha watu wa mipango mingi na ardhi katika halmashauri husika ili kuweza kujua mipango hasa iliyopo ya matumizi ya ardhi katika sehemu hiyo.

Hii ni tofauti na uliyosema ya kubadili matumizi ya commercial plots (kama PLOTS) kuwa residential plots.
***
upo sahihi ndicho alichomaanisha.
 
Serikali za mitaa zingepima na kuuzia hivyo viwanja Kwa bei nafuu naamini kila mtu angenipa Na angejenga
 
Hata Hapo Uliposimama Mtoa Uzi Zamani Palikuwa Shamba Lakn Leo Ni Makazi.
Ebu Rudi Tena Na Uzi Wako Tukuelewe Maana Idadi Ya Watu Ikiongezeka Ardhi Itahitajika Lakn Sehemu Yenye Maliasili Au Vyanzo Vya Maji Ndipo Ambapo Hawataruhusiwa Kujenga.
 
Back
Top Bottom