Lukuvi, Muhongo: REA Isimani ilijaa rushwa na ufisadi wa kutisha

Magulukwenda

New Member
Apr 26, 2016
1
0
Napaza sauti kuhusiana na hujuma na ufisadi uliofanyika wakati wa kusambaza umeme katika Jimbo la Isimani katika mradi wa umeme vijijini. Wakati mpango wa mradi wa umeme vijijini ukiletwa hapa Isimani, mbunge wetu mh. William Lukuvi alituhimiza kujenga nyumba bora na kutandaza nyaya ndani ya nyumba zetu ili tuweze kufungiwa umeme huo wa vijijini. Wananchi walihamasika sana kwa kujenga nyumba bora na kisha kufanya wiring katika nyumba zao tayari kwa kufungiwa umeme

Cha ajabu mradi ulipofika haukuwa vile kama tulivyotegemea. Mkandalasi aliyefanya kazi ile hakuifanya ipasavyo kwani baadhi ya maeneo hakusambaza nguzo ili wananchi wafungiwe umeme. Matokeo yake imekuwa hasara kwa wanavijiji kwani waliongia gharama za kufunga nyaya katika nyumba zao halafu hawakupelekewa umeme. Pamoja na kuwa wananchi walilipia, wale makandalazi hawakuwafungia umeme wanavijiji bila kupewa hongo ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/= mbali ya malipo halali wanavijiji waliyolipa Tanesco. Na kwakuwa ilikuwa kazi ya rushwa walikuwa wanawaunganishia wananchi waliootoa hiyo rushwa usiku kati ya saa3 hadi saa 4. Mbunge wetu na waziri wakitaka kuthibitisha haya wapite kuuliza wote waliofungiwa umeme hapa kata ya Kising’a kuanzia kijiji cha Igingilanyi hadi hapa Kising'a penyewe watawaambia ukweli kuwa bila hizo pesa walikuwa hawafungiwi umeme. Wale waliokataa kutoa, hawakufungiwa umeme hata kama nguzo ilikuwa mlangoni na wengine mpaka sasa hawajafungiwa. Baadhi ya maeneo ya vijiji hawakusambaza kabisa nguzo za kuunganisha umeme majumbani licha ya kuwa nguzo za line kubwa zimepitia meneo hayo

Tunamwomba mbunge wetu afuatilie hili suala kwani isije kuwa alikuwa anatumia kama kigezo cha sisi kumpigia kura na baada ya hapo ametusahau. Kama tungejua umeme utasambazwa kwa watu wachache sisi ambao hatukuletewa umeme tusingeingia gharama za kufanya wiringi badala yake pesa tulizotumia kwa shughuli hiyo tungezitumia kwa kilimo. Sasa tumebaki na manyaya tu ndani ya nyumba lakini bila umeme wakati huo huo katika kijiji hicho hicho wenzetu wanaumeme. Umeme ni maendeleo hivyo kutunyima umeme ni kuturudisha nyuma katika maendeleo

Tunaomba mbunge wetu na waziri wa wizara husika Suala la usambazaji umeme lifuatiliwe ili kila mwananchi aliyekidhi vigezo afungiwe na sio kwa mtindo wa rushwa kama ilivyofanyika na kusambaza baadhi ya maendeo na mengine kuyaacha. Vile vile tunaomba yule mkandalasi aliyekuwa anasambaza umeme hapa afuatiliwe na kutumbuliwa kwani aliwatia hasara sana wananchi kutokana na kuwadai pesa nje utaratibu unaotakiwa. Jingine ambalo tunamwomba ni kuhakikisha huduma hii inafika hata vijiji ambavyo viko mbali ya barabara kuu ya Iringa – Dodoma kama Itagutwa kwani kwa sasa huu umeme inaonekana kama ni kwa ajili ya vijiji na watu walio karibu na barabara kuu tu.
 
Back
Top Bottom