LUKUVI! Mbona statement yako haina logic kabisa?

LUKUVI! Mbona statement yako haina logic kabisa?

WAUAJI WAWAJIBISHWE.
Lakini baada ya kipindi hiki cha maombolezo kwa mauaji kama haya na mauaji mengine ambayo yametokea muda mrefu katika taifa letu, ni lazima tufike hatua tuseme hapa imetosha. Ifike hatua tuseme, waliohusika na mauaji haya, si tu yaliyotokea Arusha Juni 15 mwaka huu, bali waliohusika na mauaji ya kuanzia yale ya Arusha Januari 5 2011, na mauaji yaliyofuatia baada ya hapo: mauaji ya Igunga Mwezi Oktoba 2011 ya Marehemu Mbwana Masoud, aliyekutwa ameuawa na kutupwa. Mauaji yaliyofuata Arumeru, alipochinjwa kiongozi wa Chadema Marehemu Mbwambo aliyechinjwa kwa msumeno, na baadaye askari Polisi wakadiriki kumtorosha mtuhumiwa huyo mahakamani na mpaka leo hajapatikana, na mauaji yote yaliyotokea baada ya hapo, ifike hatua tuseme sasa imetosha.

Ifike hatua tuiwajibishe serikali, ambayo baada ya kushindwa kubaki madarakani kwa kuwatumikia wananchi, baada ya kushindwa kubaki madarakani hata kwa kutumia ufisadi na rushwa, kutoa rushwa kwenye chaguzi, lakini wananchi bado wanakubali mabadiliko. Baada ya kushindwa kung'ang'ania madarakani kwa siasa za UONGO, SIASA CHAFU ZA PROPAGANDA ZA UDINI, UKABILA n.k., sasa wanafikiri kwamba wanaweza kung'ang'ania madarakani kwa UMWAGAJI WA DAMU.
Ukweli ndio utakaonusuru nchi hii. Tukiachia hila, uongo, rushwa, propaganda chafu ziwe ndio siasa, tumeshafika pabaya.
 
Nasubiri kwa Hamu Kideo ndani ya Youtube, Jamani CDM tuwekeeni kitu hiyo watu wahumbuke, Ila jamaa walivyo na roho ngumu wanaweza wakakana, Maana Ya mwangosi walibisha vilevile, Mpaka watu walipo weka picha zikionyesha tulio zima ndipo MACCM walipo shindwa kuendesha Propaganda zao.
 
Mungu iokoe Tanganyika na vita inayoinyemelea.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Tanzania tunahitaji mediator wa kuleta muafaka ndani ya nchi.

Bahati mbaya watawala watakuwa kwenye hali ya kukataa na ku criminalize wapinzani. Lakini tunakokwenda si pazuri hata kidogo.
 
Ingekuwa Nape sawa, kwani yeye ni mtu wa propaganda. Lakini huyu waziri anayetoa kauli kny serikal? yaani anasema wananchi waliokusanyika pale mkutatoni waliomuona mtu aliyelenga kuwauwa halafu wakamkinga asikamatwe na polisi/

Jamani, jamani, mawaziri wetu kwa ulevi wa madaraka wamefikia kusema kauli za kijinga kama hiii, hata mtoto wa miaka kumi ukimwambia atakushangaa!

I'm flabbergasted. I really am! Nani mwenye logic angalau nzuri aliyebakia katika serikali ya JK?

Sidhani kama lukuvi anaweza kukuelewa, sura pana kichwani hewa
 
Back
Top Bottom