LUKUVI! Mbona statement yako haina logic kabisa?

LUKUVI! Mbona statement yako haina logic kabisa?

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
242
Ingekuwa Nape sawa, kwani yeye ni mtu wa propaganda. Lakini huyu waziri anayetoa kauli kny serikal? yaani anasema wananchi waliokusanyika pale mkutatoni waliomuona mtu aliyelenga kuwauwa halafu wakamkinga asikamatwe na polisi/

Jamani, jamani, mawaziri wetu kwa ulevi wa madaraka wamefikia kusema kauli za kijinga kama hiii, hata mtoto wa miaka kumi ukimwambia atakushangaa!

I'm flabbergasted. I really am! Nani mwenye logic angalau nzuri aliyebakia katika serikali ya JK?
 
Kama hii statement aliiandika yeye au aliipitia kabla ya kuisoma na akaenda kuisoma hivyo hivyo, basi inabidi akapimwe akili. Lakini nahisi aliisoma tu kwa ile tabia ya viongozi wengi kupenda kuandikiwa vitu na kuvisoma bila kuvipitia na kuona kama vina logic.
 
Walioinadika ndio hao walipanga huo ugaidi. Yaani mtu aue ndugu yako halafu umkinge asikamatwe. Mbona ni kinyume chake? Angekamatwa angekatwa vipisi vipisi. Lukuvi huu ni ujinga uliokithiri. Jua kwamba hakuna mtanzania aliyekubaliana na ujinga kama huu. So wewe ni Mjinga no. 1 Tz
 
Ingekuwa Nape sawa, kwani yeye ni mtu wa propaganda. Lakini huyu waziri anayetoa kauli kny serikal? yaani anasema wananchi waliokusanyika pale mkutatoni waliomuona mtu aliyelenga kuwauwa halafu wakamkinga asikamatwe na polisi/

Jamani, jamani, mawaziri wetu kwa ulevi wa madaraka wamefikia kusema kauli za kijinga kama hiii, hata mtoto wa miaka kumi ukimwambia atakushangaa!

I'm flabbergasted. I really am! Nani mwenye logic angalau nzuri aliyebakia katika serikali ya JK?

Lukuvi ni maskini sana,ananjaa alafu ni mwizi asipotamka hivyo atakosa ugali,ni maskini sana,ila kwa vile kalimbikiza mali za wizi anajihisi tajiri,anahofu sababu ni maskini,we mskilize fikra zake kwenye masula mazito,utakiri ni maskini na mwenye hofu kubwa
 
Ingekuwa Nape sawa, kwani yeye ni mtu wa propaganda. Lakini huyu waziri anayetoa kauli kny serikal? yaani anasema wananchi waliokusanyika pale mkutatoni waliomuona mtu aliyelenga kuwauwa halafu wakamkinga asikamatwe na polisi/

Jamani, jamani, mawaziri wetu kwa ulevi wa madaraka wamefikia kusema kauli za kijinga kama hiii, hata mtoto wa miaka kumi ukimwambia atakushangaa!

I'm flabbergasted. I really am! Nani mwenye logic angalau nzuri aliyebakia katika serikali ya JK?
Nape au Mwigulu
 
Ndugu yangu ULITEGEMEA LOGIC kutoka kwa waziri wa CCM??????!
 
yeye na wassira na Mwigulu ni majanga ya taifa.
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 
Ingekuwa Nape sawa, kwani yeye ni mtu wa propaganda. Lakini huyu waziri anayetoa kauli kny serikal? yaani anasema wananchi waliokusanyika pale mkutatoni waliomuona mtu aliyelenga kuwauwa halafu wakamkinga asikamatwe na polisi/

Jamani, jamani, mawaziri wetu kwa ulevi wa madaraka wamefikia kusema kauli za kijinga kama hiii, hata mtoto wa miaka kumi ukimwambia atakushangaa!

I'm flabbergasted. I really am! Nani mwenye logic angalau nzuri aliyebakia katika serikali ya JK?

Usishangae ndugu. Viongozi wa CCM wote saa imefika na wananena kwa lugha! Ni kama kama wale wadhalimu waliokuwa wanajenga mnara wa Babeli lengo wamfikie mungu. Hawataweza kuelewana asilani hata kama wakikaa na kuweka msimamo mmoja. Tanzania ni taifa la mungu ambalo lilipaswa kuwa shinning example kwa Afrika nzima. Tanzania ndio Moses wa Afrika na yale mambo yote aliyofanya Mwl. Nyerere na wenzake kulikomboa bara la Afrika toka makucha ya wanyonyaji haikuwa bahati mbaya wala ya kubahatisha. Mwl. na wenzake walikuwa ni "conduit" tu ya mpango mzima. Sasa kazi waliopewa na mungu wameinajisi kwa kuchonga sanamu ya dhahabu na kuifanya mungu wao. That is the bottomline!! Hawataelewana tena
 
mtu aliemwambia Mh.Rais ataenda kwa passport matokeo yake yy atapigwa exile.ushnd 22% tu duuu.aliponzwa kwel kwel
 
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
Peleka uchafu wako uliolishwa na CCM kwa mama yako kwanza, na sio kuja kutapika humu JF.
Tunajadili hoja wewe unaleta vioja, unataka nini?
Hizi posho za CCM zimekuharibu kabisa.
 
LumumbarDAR iyo ndo hal harisi mkuu,si kaul za viongoz wa CDM au walikuwa wanatania tu.
 
Nilisha sema tatizo la CCM na Serikali ni kuwa wapuuzi wote ndio wamewekwa mstari wa mbele kukisemea chama na serikali. Hebu angalia: Nape, Mwigulu, Wassira, Lukuvi, Kuna kitu hapo? Wakifungua midomo tu ndio utajua mkosi ulioipata CCM na serikali yake! Ni vigumu kuamini kama hawa wana ubongo wa kufikiri kabla ya kusema! Hiyo ni reflection ya akili na uwezo alio nao aliyewaamini na kuwaweka kwenye nafasi hizo!
 
Walioinadika ndio hao walipanga huo ugaidi. Yaani mtu aue ndugu yako halafu umkinge asikamatwe. Mbona ni kinyume chake? Angekamatwa angekatwa vipisi vipisi. Lukuvi huu ni ujinga uliokithiri. Jua kwamba hakuna mtanzania aliyekubaliana na ujinga kama huu. So wewe ni Mjinga no. 1 Tz

mkuu kamzidi na mzee wa tanzania ni Muungano wa Zimbabwe na zanzibar!?
 
Mh. Mnyika anasema kuwa:

1. Lukuvi amesema uongo huku akijua ukweli
2. Polisi ndio waliotupa Bomu na kumtorosha mhalifu.
3. Hao wanaotetea Polisi ndio wanaowatumia Polisi kufanya mauaji.
4. Wakati wa maombolezo CCM wanafanya Propaganda kama vile waliokufa kwenye mkutano wa Chadema si Watanzania.
5. Tamko hili limelazimika kutolewa sasa kukanusha UONGO ambao kukiachwa utaonekana ni ukweli.
6. Wauaji wawajibishwe
7. Hakuna Serikali inayoendelea kudumu madarakani kwa kumwaga damu
8. Chadema tuendelee kutetea Amani huku tukiendelea kudai haki.


Sehemu ya Tamko la Mh. Mnyika Juu ya Propaganda za CCM wakati wa Maombolezo - Tukio la Bomu Arusha.

a. UZITO WA KAULI YA LUKUVI.
Mwenyekiti Mbowe alizungumza jana, na wakati anaeleza ushahidi uliopo, na ushuhuda uliopo juu ya tukio hili, ameeleza vilevile kushangazwa na kauli za Waziri Lukuvi. Kwa hiyo katika nukta hii, tuongeze tu baadhi ya mambo ya msingi, ikizingatiwa kuwa waziri Lukuvi ni Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge. Kauli yake, akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, inamaanisha ni Ofisi ya Waziri Mkuu imezungumza Bungeni.

b. LUKUVI AMESEMA UONGO HUKU AKIJUA UKWELI
Kauli ya Lukuvi inapaswa kubebwa kwa uzito mkubwa, na kwa kauli hiyo imedhihirika kwamba ni sera ya serikali kusema uongo, huku ikijua ukweli. Kauli yake imedhihirisha kwamba, jambo hili la kutaka kulidanganya Taifa, lina uratibu wa serikali kwa ujumla wake. Kama Waziri wa Uratibu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu ndiye Mkuu wa shughuli za serikali bungeni) anaweza kutoa uongo wa namna hiyo, maana yake kauli hizi zimeratibiwa, na hivyo serikali bungeni imepoteza uhalali wa kimaadili (moral authority) wa kuzungumza, kwa sababu imeratibu uongo wa moja kwa moja.

c. ASKARI WA FFU ALITUPA BOMU NA ALITOROSHWA NA ASKARI WENZAKE
Kauli ya Waziri huyu iturudishe nyuma tu. Wakati anazungumza kwamba polisi walishindwakumkamata mhalifu kwa sababu eti wananchi wamechochewa muda mrefu na hivyo kulichukia jeshi la polisi kwa kiwangu cha polisi kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kumkamata mhalifu, wakati ukweli wa mikanda tuliyo nayo unaonyesha kuwa polisi ndio ambao waliamua kumtorosha mhalifu.

Sio tu kumtorosha kwa magari, bali kwa matumizi ya bunduki na bastola kuwapiga risasi wananchi waliokuwa wanafanya ulinzi shirikishi wa kuelekea kumkamata mhalifu waliyemwona, kwa sababu tu mhalifu huyo amevaa mavazi ya FFU, kwa sababu tu mhalifu huyo ni mwenzao. Polisi hawa wakatekeleza uhalifu mwingine wa kupiga raia risasi ili kulinda uhalifu. Jeshi la namna hii haliwezi kutetewa.

d. WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye ndani ya jimbo lake alituhumiwa bungeni kulitumia vibaya jeshi la polisi, kumtumia vibaya Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda. Lakini Lukuvi aliposimama akaenda mbele zaidi, sio tu ndani ya jimbo lake, akafikia hata hatua ya kumkingia kifua Michael Kamuhanda, ambaye ripoti ya tume ya haki za binadamu na utawala bora inamhusisha moja kwa moja na kusimamia opereshein iliyosababisha mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi.

Kama ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na serikali ni wazi yamepangwa na serikali.

e. SERIKALI, CCM WANAFANYA PROPAGANDA BADALA YA KUTOA NAFASI YA MAOMBOLEZO .
Sote tuna majonzi, sote tunaomboleza. Ni bahati mbaya kuwa serikali, CCM na bunge, badala ya kutoa nafasi kwa maombolezo, wakati ambapo hatujawazika wenzetu, wakati ambapo tuko katika kipindi cha maombolezo, wao badala ya kuomboleza wanafanya propaganda.

f. TAMKO HILI LINAKUJA SASA KUKANUSHA UONGO.
Tumelazimika kuzungumza jambo hili badala ya kuzungumzia majeruhi, ambao wapo hospitali na tunaendelea kuwahudumia mpaka sasa, badala ya kuzungumzia marehemu, ambao lewa wanapewa heshima, wengine watapewa heshima kesho, tumelazimika kuyazungumzia haya kwa sababu UONGO UKIACHIWA, UKASEMWA, UKASEMWA, UKASEMWA, watu wanaweza kuamini kwamba ni ukweli. Lakini ni wazi, UKWELI UKISEMWA WATU WACHACHE WANAWEZA KUDANGANYIKA KWA MUDA MFUPI SANA, LAKINI SIO WATU WOTE KWA WAKATI WOTE.

Watanzania tusikubali kudanganyika, kwa pamoja tuungane katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tuendelee kusimamia UKWELI, kuueleza UKWELI.

g. WAUAJI WAWAJIBISHWE.
Lakini baada ya kipindi hiki cha maombolezo kwa mauaji kama haya na mauaji mengine ambayo yametokea muda mrefu katika taifa letu, ni lazima tufike hatua tuseme hapa imetosha. Ifike hatua tuseme, waliohusika na mauaji haya, si tu yaliyotokea Arusha Juni 15 mwaka huu, bali waliohusika na mauaji ya kuanzia yale ya Arusha Januari 5 2011, na mauaji yaliyofuatia baada ya hapo: mauaji ya Igunga Mwezi Oktoba 2011 ya Marehemu Mbwana Masoud, aliyekutwa ameuawa na kutupwa. Mauaji yaliyofuata Arumeru, alipochinjwa kiongozi wa Chadema Marehemu Mbwambo aliyechinjwa kwa msumeno, na baadaye askari Polisi wakadiriki kumtorosha mtuhumiwa huyo mahakamani na mpaka leo hajapatikana, na mauaji yote yaliyotokea baada ya hapo, ifike hatua tuseme sasa imetosha.

Ifike hatua tuiwajibishe serikali, ambayo baada ya kushindwa kubaki madarakani kwa kuwatumikia wananchi, baada ya kushindwa kubaki madarakani hata kwa kutumia ufisadi na rushwa, kutoa rushwa kwenye chaguzi, lakini wananchi bado wanakubali mabadiliko. Baada ya kushindwa kung'ang'ania madarakani kwa siasa za UONGO, SIASA CHAFU ZA PROPAGANDA ZA UDINI, UKABILA n.k., sasa wanafikiri kwamba wanaweza kung'ang'ania madarakani kwa UMWAGAJI WA DAMU.

h. HAKUNA DOLA ILIYODUMU KWA KUMWAGA DAMU YA RAIA WAKE.
Historia ya dunia inaonesha kuwa hakuna dola iliyokataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, kwa nguvu ya umma, ikafanikiwa kubaki madarakani kwa kutumia askari, kwa kutumia umwagaji damu. Tanzania tunapita njia hiyo. Tusielekee huko.

i. CHADEMA TUTETEE AMANI HUKU TUKIDAI HAKI.
Sisi Chadema tunapenda amani ya nchi yetu, tutaendelea kutetea amani ya nchi yetu. Lakini hatutarudi nyuma katika kudai haki. Haki za sisi tunaoishi, haki za waliokufa na haki za watakaokufa. Hatutaacha, kwa sababu tukifanya hivyo itakuwa ni usaliti kwa imani kubwa ambayo wananchi wameipa Chadema.

(Vichwa vya habari ni mimi nimeweka kwa kurahisisha kusoma tamko).
 
Last edited by a moderator:
WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye ndani ya jimbo lake alituhumiwa bungeni kulitumia vibaya jeshi la polisi, kumtumia vibaya Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda. Lakini Lukuvi aliposimama akaenda mbele zaidi, sio tu ndani ya jimbo lake, akafikia hata hatua ya kumkingia kifua Michael Kamuhanda, ambaye ripoti ya tume ya haki za binadamu na utawala bora inamhusisha moja kwa moja na kusimamia opereshein iliyosababisha mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi.

Kama ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na serikali ni wazi yamepangwa na serikali.
Haya maneno yanahitaji majibu. Kwa nini yanakwepwa?
 
Back
Top Bottom