Lukuvi Kwenye Ibada ya Mazishi ya Ndesamburo na Magari Mawili Ya Polisi Wenye Silaha: Tafsiri

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,273
21,455
Bado kichwa kinanizunguka. Hivi lile tamko la Magufuli kuwa vyama vya upinzani ni maadui linapelekwa mbali kiasi cha Lukuvi kwenda kwenye ibada ya mazishi ya Ndesamburo na magari mawili yaliyojaa askari wenye silaha? Alikuwa anaenda msibani au vitani?

Ukweli ni kwamba nyie watu mnaojiita viongozi wa nchi hii mnatupeleka kubaya sana. Hivi Watanzania tumefikia mahali ambapo waziri anahitaji magari mawili ya polisi wenye silaha kwenda kwenye msiba wa Mtanzania mwenzetu katika nchi yetu wenyewe?

Sijawahi kuona uongozi uliokosa busara kama huu uliopo sasa hivi - manifestation of the highest degree in lacking common sense, foresight and intellectual rationality.

Ndio maana siku zote nasema changamoto kubwa zinazotukabili hapa Tanzania kwa sasa ni mfumo wa vyama vingi vya siasa kupoteza amani yetu, na nyingi ya akili ndogo kuwa na mamlaka makubwa

Waziri Lukuvi azua taharuki mazishi ya Ndesamburo
 
upload_2017-6-7_12-22-25.jpeg

Katika hali isiyo ya kawaida Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi jana alizua taharuki baada ya kuwasili katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini Philemon Ndesamburo akiwa ameongozana na magari mawili ya polisi waliobeba silaha.

Ibada hiyo ilifanyika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Kiboriloni mjini Moshi jana.

Hali hiyo ilisababisha hofu kwa wananchi wengi waliokuwa nje ya kanisa hilo na baadhi wakishindwa kuingia kanisani katika ibada iliyokuwa inaendelea ndani.

Hata hivyo ni kawaida kwa waziri kuongozwa na vyombo vya usalama wakati wa msongamano wa watu.

Chanzo: Mwananchi
 
View attachment 520650

Unaendaje na askari wenye silaha kwenye msiba?
 
Aisee lengo akasaini tu kile kitabu cha rambirambi, ili aingie kwenye kumbukumbu
 
Haina shida sana hali mradi askari wale hawakuwabughudhi wananchi na mambo yote yalienda sawa kabisa, maana ulinzi kwa viongozi una nafasi yake kiitifaki hivyo siyo wa kupuuzia younever know.
 
Unauhakika gani hao polisi walikwenda kisa Lukuvi na sio kuhakikisha usala unakuwepo eneo hilo kwa ujumla? Kwanini Kiki hadi misibani nyie watu!! Huu upuzi wenu hamuoni hata aibu? Mnaishiwa vibaya sana
Mjinga wewe, kipofu unaeongozwa na vipofu usiyejua kutumia akili yako kuelewa mambo. Kama suala lilikuwa kulinda usalama kwa nini Polisi waingie na Lukuvi na wasiwepo hata kabla Lukuvi hajafika?
 
Hivi inakuaje waziri anakuja kanisani na polisi magari mawali hii nini maana yake Tanzania utajafikia hatua hii waziri amekosea hii sio sawa
 
Ndipo tumefika na kibaya zaidi inapitiliza kuelekea huko kwa kasi ...madaraja yanavunjwa na kuta zinaimarishwa!
 
... ni kama una yako wewe na haupendi usalama wa viongozi wetu.

Usalama wa viongozi wetu? Hata kama nina nia mbaya na viongozi wa nchi hii, kum-liquidate mtu kama Lukuvi itasaidia nini? Kutoa nafasi nyingine ya kutumia michango ya rambirambi kwa ajili ya hospitali ya Mkoa Iringa anakotoka? Kuwapo au kutokuwapo kwa Lukuvi kama waziri hakutikisi taifa hili, so hahitaji kulindwa na magari mawili ya polisi wenye silaha. Hata Somalia na South Sudan mawaziri hawalindwi namna hii.

Sasa kama nchi hii imefikia uoga wa namna hii, Magufuli atasafri akiandamana na brigedia mbili za JWTZ basi, wakiwa na mizinga na vifaru. Au ndio maana hakwenda Arusha kwenye mazishi ya watoto? Hali hii mmeileta wenyewe kwa kukosa busara na hekima za uongozi. Shame on you.
 
Back
Top Bottom