Lukuvi kuhamisha wahudumu wabovu maofisini ni suluhisho?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi kuhamisha wahudumu wabovu maofisini ni suluhisho??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 20, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Majuzi nimeshhangaa sana kuona watu walioua watoto wachanga si chini ya miamoja.watu wazima si chini ya hamsini jamani leo hii wameamishwa kutoka mwananymala kusambazwa hospital nyingine
  Bado najiuliza mh lukuvi hii ni suluhisho la kutokomeza uovu.....,uoni kamawalikuwa wauwaji wanazidi kuendelea kuua....kama wakatili unahisi wakienda mikoani wataacha ukatili
  hawa awakuwa tofauti na maharamia wa somalia jamani...serikali ni wanafiki ukiwona hivyo kuna mmohja wa ndugu wa KIONGOZI yamemkuta wakajifanya wameamua kuwabadilisha...
  Hili si soln ya KUMALIZA MATATIZO MAOFISINI.....
   
 2. M

  Msindima JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wala hiyo ya kuwahamisha sio solution,tabia ya mtu kubadilika inachukua muda sana,wakifika huko kwenye vituo vipya kwa muda wata-act kuwa ni wauguzi wazuri sana lakini wakishazoea mazingira tabia zao zitajionesha wazi kabisa.Wangetafuta solution nyingine lakini kwa hapo naona wamechemka tena sana.
   
 3. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Una ushahidi na hili au unabwabwaja tu?
  Kama una ushahidi nenda mahakamani haki itendeke
  Si vizuri kumuita mtu muuaji wakati huna ushahidi. Hivi watu mtakua lini?
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kwa hili la mauwaji yatokanayo na uzembe best kuna namna ya kuhakikisha kuwa limetokea kama ni kweli sheria ni vizuri ikachukua mkondo wake. Kuhusu kuhamisha watendaji wabovu in short term ni kutatua tatizo la mahali ila in long term siyo utatuzi wa tatizo bali ni kama kufukuza mbuzi shambani mwako na kuwaelekezea kwenye shamba la jirani yako!
   
 5. O

  Orkesumet Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ndo tatizo kubwa ambalo tumerithi toka kwa viongozi wetu, kuwa mfanyakazi wa umma anapoharibu basi hupewa uhamisho! Huku ni kukosa umakini kabisa na kutaendelea kuharibu na kuangamiza uweza wa taasisi mbalimbali katika kutekeleza majukumu ipasavyo. ukiangalia historia mashirika mengi yamezikwa kwa sababu ya utendaji mbovu wa viongozi na viongozi hao wabovu wamekuwa wakiahmishwa kutoka shirika moja hadi jingine na kupewa nyadhifa zenye kutoa maamuzi na utawala! kuna thread ya nyuma ambapo mwanaharakati alilalamika kuhusu mtendaji mkuu wa ATC kuhamishiwa shirika la bima (bila shaka kumbukumbu zangu ni sahihi) huku akiacha shirika hilo hoi bin taaban. Je huko alophamishwa ataweza kuleta ufanisi katika utendaji ikiwa alipotoka ameacha shirika katika hali mbaya? Kukosekana kwa mfumo wa kuwajibika and majukumu ya kazi yanayoeleweka yametoa mwanya kwa wanasiasa kuingilia majukumu yasiyo wahusu! katika hili bodi ya afya katika eneo husika imefanya nini? mganga mkuu amehusika vipi katika suala hili? Uamuzi wa lukuvi unaacha maswali mengi kuliko majibu! huu ni mtazamo wangu!!
   
Loading...