Lukuvi anayumbisha serikali ya JK

Lukuvi anayumbisha serikali ya JK

Kwani mzee wa kanuni ya 64 ameanza leo kudaganya na kutoa kauli za kejeli na hovyo hovyo ndani na nje ya bunge? Anafahamika (soma anasifika) kwa kufanya hivyo huku mara kadhaa akishangiliwa kwa makofi na wabunge wengi wa chama chake. Kwa mtazamo wangu, sio kwamba Lukuvi anayumbisha serikali ya JK, bali yale anayosema ndiyo msimamo wa serikali na chama chake. Kwa maneno mengine, kauli za mzee huyu zinaakisi tu serikali ya chama cha mapinduzi ambayo tayari inayumba.

Mwalimu JKN aliwahi kusema: "bila CCM imara nchi itayumba". Najua wanasisiemu wengi hupenda kunukuu kauli hii ili kutaka kuaminisha watanzania kuwa ccm lazima iendelee kutawala na kwamba vyama vya upinzani vitayumbisha (au tayari vinayumbisha?) nchi. Mimi huwa naiangalia kauli hii kwa mtazamo tofauti kwa kuangalia muktadha wa mazingira ya kisiasa ya wakati huo wakati mwalimu anatoa kauli hii.

Ni kweli wakati huo (mwaka 1994 au 95) kulikuwa na vuguvugu kubwa la upinzani, lakini pia kulikuwa na msigano mkubwa ndani ya ccm katika harakati za kuelekea uchaguzi wa 1995. Kwa kuzingatia kuwa ccm ilikuwa madarakani, na kwa kuona pia kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa ccm kushinda uchaguzi wa 1995 ilhali kuna mvurugano na mnyukano mkubwa ndani yake, yamkini ndiyo yaliyompelekea mwalimu kuona mbele na kutoa kauli hii.

Binafsi, nafikiri alichomaanisha mwalimu ni kuwa serikali imara inatokana na chama imara. Udhaifu na ulegelege wa ccm ya sasa ndio uliozaa serikali dhaifu inayokumbatia wauza unga, majangili, mafisadi, wala rushwa n.k. Nani wa kumfunga paka kengele wakati hao hao ndio walifadhili uchaguzi ndani ya chama. Kama washiriki wa semina elekezi ya chama tawala wanaweza kupewa 'air time' ya laki 2 kila mmoja tena kwa uwazi kabisa sio hata kwa kificho, na mwenyekiti wa chama taifa anajua na amewaambia washiriki hadharani, lakini akaishia na yeye kulalamika badala ya kuchukua hatua, unategemea nini????

.
.
.
.
.
.
.
.
.
hata kwa muktadha wa sasa mkuu iko plain tu,nchi inayumba mara tembo mara udini,mara gesi,mara kung'oana kucha,mara viwango vya ufaulu....huku nako mara iyena iyena mara gamba mara balozi mchina mara
.
.
.
.
.
bila ccm imara nchi itayumba
.
.
bila ccm imara=na ccm legelege/dhaifu
.
.
badili neno bila ccm imara na 'na ccm legelege/dhaifu'
.
.
.
.
ingekuwa leo angesema kama ifuatavyo
.
.
.
ccm legelege inayumbisha nchi.
 
Si kweli. Lukuvi ni waziri makini sana. Acheni figisu.
 
Si kweli. Lukuvi ni waziri makini sana. Acheni figisu.

Tunajua mnafikri kwa kutumia ma------, pengine ni vile tumbo kwanza ukweli na haki baadae. Inavyotumia kichwa chake WL ni dhahiri kunatatizo na anachangia kuyumbisha serikali. Majibu mapesi na ya mzaha kwenye masuala nyeti nao ni ujinga au tusema ujanja dhaifu sana maana ndo lugha zenu, hata kama hatupendi.
 
anasema wapinzani au vyama kwenda ikulu ni courtesy tu, mambo yao huwa yanajadili wana task force ya ikulu. ni nilizadhi pale nondo hutolewa hararfu task force hu ipo kuchukua point na kuandaa ripoti kamili?? kwa hiyo rais huwa anawaita ili wauze sura tu? mambo huwa yamekwisha fanya??? nitoeni tongnotongo jamani, hili la LUKUVI.
 
Anasema wapinzani au vyama kwenda ikulu ni courtesy tu, mambo yao huwa yanajadili wana task force ya ikulu. ni nilizadhi pale nondo hutolewa hararfu task force hu ipo kuchukua point na kuandaa ripoti kamili?? kwa hiyo rais huwa anawaita ili wauze sura tu? mambo huwa yamekwisha fanywa??? nitoeni tongotongo jamani, hili la LUKUVI.
 
Lukuvi kasema jana BUNGENI walaumiwe waTZ kwa kuchagua WABUNGE WENGI WA CCM, Ismania mmesikia????
 
Back
Top Bottom