Lukuvi anayumbisha serikali ya JK

Lukuvi anayumbisha serikali ya JK

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,073
Jamaa huyu amekuwa akitoa majibu ya kihuni bungeni kwa anavyodhani yeye na pia boss wake Pinda majibu hayo tabasaidia CCM kumbe ukweli ni yanaua chama.

Mtu wa haiba yake hakupaswa hata kuingia bungeni maana ni limbukeni kwa mtazamo wangu ambaye hana kifani. Ulimbikeni wake unatokana na kufikiri ana akili sana na hivyo kupotosha bunge, chama na serikali pia.

Tujiulize mara kadhaa ameamka bungeni na kusema serikali haitaji majina bado inafanya uchunguzi wa wauza unga, na sasa inafanya uchunguzi wa majangili wa wanyamapori.

Suala langu kwani wauza unga ni mtu mmoja au kikundi kimoja? kwani majangili ni mtu mmoja au kikundi kimoja? Kama jibu ni siyo basi Lukuvi ni bogus saana.

Kwani mzinzi mmoja hakamatwi au hatajwi mpaka wote wanaozini wajulikane harafu watajwe kwa pamoja? yaani majaji na mahakimu wala rushwa hawakamatwi mpaka wote wawe wamechunguzwa na kutangazwa kwa pamoja? kwani mwizi mmoja hakamatwi mpaka na wezi wengine wajulikane ndo wakamatwe kwa pamoja.

Lukuvi anadanganya bunge kila mara serikali haiwezi kutaja majina wakati bado uchunguzi unaendelea je hakuna mtu au kikundi cha wauza unga au majangili ambacho uchunguzi umekamilika??? kwanini hawa wasitajwe na kukamatwa??? kwa style hii serikali haitataja hata siku moja wauza unga wala majangili maana haiwezekani kuwapata wote kwa wakati mmoja eti ndo uwataje na waanze kushughulikiwa.

AIBU KWA LUKUVI na serikali yake, AIBU KUBWA KWA CCM. AIBU KUBWA KULIKO KWA RAIS wa nchi ambaye amempata hiyo dhamana.

TUNATAKA MTUTAJIE AMBAO UCHUNGUZI UMEKAMILIKA, vinginevyo mseme hakuna hata uchunguzi mmoja umekamilika ambayo ndo aibu yenyewe.

Nawasilisha
 
Kwani huyo aliyempa uwaziri hakuwa akijua kiwango chake cha elimu? Most likely imefanyika kwa makusudi ili iwe rahisi kutumika na kutoa majibu ya hovyo ambayo mwenye akili zake hawezi kusema. There is no single day huyu jamaa alitoa jibu la kuridhisha au lenye susbtance. This is pathetic. Hivi lile dau la 1m vipi? Each time this guy stands up in the parliament he makes me puke.
 
Kwani mzee wa kanuni ya 64 ameanza leo kudaganya na kutoa kauli za kejeli na hovyo hovyo ndani na nje ya bunge? Anafahamika (soma anasifika) kwa kufanya hivyo huku mara kadhaa akishangiliwa kwa makofi na wabunge wengi wa chama chake. Kwa mtazamo wangu, sio kwamba Lukuvi anayumbisha serikali ya JK, bali yale anayosema ndiyo msimamo wa serikali na chama chake. Kwa maneno mengine, kauli za mzee huyu zinaakisi tu serikali ya chama cha mapinduzi ambayo tayari inayumba.

Mwalimu JKN aliwahi kusema: "bila CCM imara nchi itayumba". Najua wanasisiemu wengi hupenda kunukuu kauli hii ili kutaka kuaminisha watanzania kuwa ccm lazima iendelee kutawala na kwamba vyama vya upinzani vitayumbisha (au tayari vinayumbisha?) nchi. Mimi huwa naiangalia kauli hii kwa mtazamo tofauti kwa kuangalia muktadha wa mazingira ya kisiasa ya wakati huo wakati mwalimu anatoa kauli hii.

Ni kweli wakati huo (mwaka 1994 au 95) kulikuwa na vuguvugu kubwa la upinzani, lakini pia kulikuwa na msigano mkubwa ndani ya ccm katika harakati za kuelekea uchaguzi wa 1995. Kwa kuzingatia kuwa ccm ilikuwa madarakani, na kwa kuona pia kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa ccm kushinda uchaguzi wa 1995 ilhali kuna mvurugano na mnyukano mkubwa ndani yake, yamkini ndiyo yaliyompelekea mwalimu kuona mbele na kutoa kauli hii.

Binafsi, nafikiri alichomaanisha mwalimu ni kuwa serikali imara inatokana na chama imara. Udhaifu na ulegelege wa ccm ya sasa ndio uliozaa serikali dhaifu inayokumbatia wauza unga, majangili, mafisadi, wala rushwa n.k. Nani wa kumfunga paka kengele wakati hao hao ndio walifadhili uchaguzi ndani ya chama. Kama washiriki wa semina elekezi ya chama tawala wanaweza kupewa 'air time' ya laki 2 kila mmoja tena kwa uwazi kabisa sio hata kwa kificho, na mwenyekiti wa chama taifa anajua na amewaambia washiriki hadharani, lakini akaishia na yeye kulalamika badala ya kuchukua hatua, unategemea nini????
 
Lukuvi ubunge wake na uwaziri ni wa waganga wa kienyeji! Maana elimu yake ni ya msingi std 7
huyu ni mbunge wetu kule ismani Iringa vijijini na anaongoza wat mbumbu anfikir wa2 wote watakua kama waleee
 
Zamani waziri akisema au jibu swali unapata taabu sana kupata jibu mbdala. Lakni leo ni kichekecho, utazani tumekabishi nchi kwa wala unga au wapiga debe?? TUNATAKA wale ambao uchunguzi umekamilika watajwe. Tuache ujinga ujinga kwa nchi ya baba na mama yangu. sio nchi ya CCM, CUF au CDM hii ni ya watanzania.
 
Namkubali saana plato........philosopher kings should rule.............. Makanjanja mhhhhhh
 
Can uwakika ila nilishawai kuskia kuwa huyo jamaa amemaliza 4m 4 then akawa mwalim wa primary ndy akachaguliw kuwa mkuu wa mkoa had xaxa kawa mbunge had now ni wazir......... me cpo!
 
Sijaona ukweli wa hoja yako zaidi ya ushabiki na kutawaliwa na hisia za kisiasa tu.
 
Hawezi kubaki salama. Historia itamhukumu. Haiwezekeni watu wasio n hatia wapigwe mabomu na jeshi la polis Arusha na afanye majigambo bungeni. Uongo ambao ameusimamia kwa kiburi bungeni ndo rahana yake yeye na kizazi chake.
 
Kwa nini bungeni kila mbunge akisimama anasema majangili wanajulikana halafu anataka wengine wataje badala ya yeye kutaja kama kweli anawajua.
 
Ni aibu sana kuwa na mawaziri wa aina ya Likuvi,wasira,mulugo,kawambwa na sophia simba!
 
Yote haya yanatokea kwa sabubu Lukuvi ni sawa na AKILI NDOGO inayojitahidi KUONGOZA AKILI KUBWA hata siku moja hawezi kuwa sahihi. Nakumbuka wakati ule wa ghorofa lilipoanguka alitoa amri lile ghorofa lingine liwe limebomolewa ndani ya siku 30 la sivyo mmiliki atashitakiwa, leo hii imepita zaidi ya miezi 3 tukimuuliza amechukua hatua gani atabaki kubwabwaja tu.
 
Unajua nchi yetu ina vituko saana...... Viongozi wamejitenga na watu......madudu ya ujangili wanafanya wao na wadau wao...
 
Unajua nchi yetu ina vituko saana...... Viongozi wamejitenga na watu......madudu ya ujangili wanafanya wao na wadau wao... Then wahanga wananchi...
 
Sijaona ukweli wa hoja yako zaidi ya ushabiki na kutawaliwa na hisia za kisiasa tu.

Wakati mwingine unapoona hoja zimetolewa hapa ambazo zina ukweli kwa kinachotokea ni vizuri ukasoma na kupitiliza si lazima uandike vitu vya kijinga. unapinga kitu ni vizuri ukaweka ukweli unaoujua la sivyo utabaki kuwa mpumb-avu.
 
Elimu ya darasa la 7 is not a crime na kama amekuwa waziri na elimu yake ndogo na capacity yake inauwezo wa kusimama ndani ya bunge na kutoa hoja tatizo liko wapi?
 
Kwani huyo aliyempa uwaziri hakuwa akijua kiwango chake cha elimu? Most likely imefanyika kwa makusudi ili iwe rahisi kutumika na kutoa majibu ya hovyo ambayo mwenye akili zake hawezi kusema. There is no single day huyu jamaa alitoa jibu la kuridhisha au lenye susbtance. This is pathetic. Hivi lile dau la 1m vipi? Each time this guy stands up in the parliament he makes me puke.


Ukiwa CCM hata kama unadegree kumi unaziweka mfukoni kwanza ndio unaweza kufanyakazi. Si mnamwona Prof. Mwongo anavyo ongea
 
Jamani ni juzi tu huyu jamaa katibu wake ameshutumiwa kwa ujangili, it means na yeye ni jangili, wewe unafikiri agetoa majibu gani, Tembo wataisha kama Ivory coast,
 
Back
Top Bottom