Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,629
Unamtetea mnyonge mmoja kwa kumsababishia mnyonge mwingine mshtuko wa moyo!.
Vipi kama huyu aliyepatwa na mshtuko wa moyo akipoteza maisha?, hao wanyonge wengine wanaomtegemea, nani atawapatia hudumu muhimu za kimaisha pale nyumbani?.
Kuna watu wanafunga biashara zao kwa sababu tu ya kutozwa kodi ambazo haziingi akilini.
Mtu anamiliki stationery yenye thamani ya shilingi milioni tatu, jamaa wa kodi wanamtaka alipe shilingi milioni kumi, tena kwa kutengeneza mazingira mepesi kabisa ya kutaka kupata hela ya bure.!!
Mtu huyu akifunga biashara yake, kuna siku mkusanya kodi hatakuwa na maana ya kuendelea kuwepo!!. Hii ndio waingereza wanaiita sadism.
Kuondokana na hulka za kubembelezana iliyokuwa imejengeka, kuna mipaka yake, ikishavukwa basi uhalisia wa mambo unakuwa ni maisha ya sadism.
Ile hali ya mtu mmoja kupata raha pindi amuonapo mwingine akiumia kwa mateso.
Kuumia na kuteseka kwa mmoja hakumnyimi usingizi mtu mwingine, na wakati mwingine hujisikia raha sana.
Maisha hayabaki kama yalivyo, huenda yakibadilika kadri siku zikipita. Itakapofika siku ya malipo kwa wote wenye kuishiriki hii sadism, basi majuto na unyonge vitakuwa ni vitu maarufu ndani ya jamii.