Lugha Kikwazo cha Penzi?

Lugha Kikwazo cha Penzi?

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,731
Kuna watu hata tujifunze vipi Kiingereza kinatupa shida tu. Kinatunyima raha. Kinatuondolea uhuru wa kujieleza.

Sasa inakuwaje ukioa mtu asiyeweza kujua Kiswahili? Si inakuwa vigumu kumueleza yaliyo moyoni? Si penzi litakwaza na lugha?
 
Kuna lugha ya picha pia.
Halafu wanasemaje? Matendo huongea zaidi ya maneno!
 
Tumia kiswahili
 
Kuna lugha ya picha pia.
Halafu wanasemaje? Matendo huongea zaidi ya maneno!

Wapenzi wanatumia muda mwingi katika maongezi - kuelezana yaliyo ndani kabisa ya mioyo yao, hayo hayawezi kuelezwa kwa matendo, hata lile tendo kuu haliwezi kueleza kila kilicho kwenye uvungu wa moyo wa mtu.
 
Halafu wanasemaje? Matendo huongea zaidi ya maneno!

"Kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake" - Mathayo 12: 34

"Mtu hunena yale yaliyojaa moyoni mwake" - Luka 6: 45

Sasa utanenaje yaliyojaa moyoni kama Inglishi izi noti Richabo!
 
Hilo si la kuuliza si ukasomeee? kuna matangazo kibao cha kuongea wiki 6 au wengine cha kuongea wiki 3 au 2 nenda kasome ili upate kunena ya kunena jamani!
 
Back
Top Bottom