Lugha hii na mafanikio katika biashara

Msimbo Pau

Member
Aug 2, 2012
24
8
Heshima kwenu WADAU:

WADAU kimsingi tunajifunza kutokana na kusikia hasa pale tunapouliza.

Kuna hili jibu ambalo kila mfanyabiashara akiulizwa analitoa-Popote pale:-luninga,ktk biashara, hata akitoka kuamka,n.k- ''BIASHARA NGUMU/HAILIPI'' siku akijitahidi saana anasema ''Aah hivyohivyo tu tunaenda/Inshaallah M.Mungu anasaidia tu''-huku ameinamisha kichwa chini au kuangalia pembeni, lakini ndo huyohuyo anabadilisha magari, anajenga nyumba nzuri, watoto wanasoma shule nzuri, anakula vizuri, n.k.

Sio hao tu hata wale ambao huoni mafanikio jibu ni hilohilo.

Hebu jaribu kwa rafiki zako wafanyabiashara halafu uje useme neno hapa. Ni nini basi nguvu ya haya majibu katika biashara? Na je yana ukweli ndani yake? Kama wewe ni mfanyabiashara pia funguka.

**End of part 1**
 
interesting....na kuna wale anasema nimejenga 'kibanda changu'..
unakwenda na kukuta bonge la house la ghorofa lol
 
interesting....na kuna wale anasema nimejenga 'kibanda changu'..
unakwenda na kukuta bonge la house la ghorofa lol

Umeonaee... Mi bado nawaangalia tu, ndo nauliza nguvu yake nini na ina ukweli WADAU? ANZA NA RAFIKI ZAKO TU AU WW MWENYEWE KAMA UNABIASHARA.
 
Back
Top Bottom