Ludewa kujengewa maktaba 45 kwa shule za msingi

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671

Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imefaidika na mpango madhubuti wa maktaba za shule unaoanza katika shule za msingi 45 wilayani humo kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa vitabu na vifaa vya kujifunzia vinavyolingana na mtaala mpya wa Taifa.


Your browser is not able to display this video.

Mkurugenzi Mtendaji wa Uwezo Tanzania, Baraka Mgohamwende

Mpango huo inaoitwa “Kijiji Changu” unaotekelezwa kwa na shirila la Uwezo Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania, unalenga vitabu vya hadithi na rasilimali za kielimu zilizobuniwa ili kuimarisha elimu msingi, kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika madarasa na jamii kwa ujumla.


Your browser is not able to display this video.

Meneja Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano, Benki ya Stanbic Tanzania, Dickson Senzi

Akizungumzia leo Februari 18 wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Uwezo Tanzania, Baraka Mgohamwende wanaunga mkono mkono maktaba za jamii kwa kuimarisha elimu msingi kwa watoto kwa kutoa vitabu vinavyoendana na mtaala wa taifa.

“Tukio hili la kukabidhi vitabu linaendana na Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo ya Elimu wa KKK uliozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Januari29, 2026 kwa kuboresha upatikanaji wa vitabu na vifaa vya kujifunzia,” amesema.

Meneja Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano, Benki ya Stanbic Tanzania, Dickson Senzi Mpango amesema ufadhili huo utasaidia ununuzi wa vitabu vinavyoendana na mtaala pamoja na vitahu vya ziada, ambapo inatarajiwa kufaidisha takribani watoto 33.619 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 10 hadi 20.

"Ushirikiano huu unaakisi namna Benki ya Stanbic mavyotekeleza uwekezaji wake wa kijamii, kwa kuzingatia miradi yenye manufaa ya moja kwa moja na inayoweza kupimwa matokeo yake. Kama ilivyo kwa programu zetu zilizopita katika sekta ya elimu na maendeleo ya jamii, mpango huu unatuwezesha kukidhi mahitaji halisi ya jamii zetu, na inaendana na kauli mbiu yetu kuwa Tanzania ni nyumbani, na tunachochea ukuaji wake," amesema.


Your browser is not able to display this video.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa Mkoa wa Njombe, Sunday Deogratius.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…