Lowassa, umeamua kuwa na busara?

Lowassa, umeamua kuwa na busara?

Binafsi naamini mpaka sasa Lowassa ndio shujaa wa siasa za Tanzania kuanzia chama tawala mpaka upinzani.

Lowassa wakati anajiunga Chadema alijua kabisa hawezi kushinda Urais, sababu ya mizizi ya ccm Na katiba iliyopo kuwa madhaifu mengi.

Baada ya kuukosa urais kupitia ccm kilichobaki kwake ilikuwa ni kuamua kusafisha jina lake hasa kwenye siasa za upinzani.

Hasa wale waliomchafua miaka nane bila huruma, Lowassa alikuwa kama nembo ya ufisadi ccm.

Na amefanikiwa kwa asilimia kubwa sana kwenye hilo, Mbowe na Chadema wote wanamlamba miguu Lowassa, Kubenea na Mwanahalisi lake ndio vinara wa kumsafisha Lowassa.... Wakati wote tunakumbuka ilikuwa ni nadra kwa Mwanahalisi jumatano kutoka bila heading kuhusu Lowassa.

Hongera Lowassa umewafanya adui zako wakupigie magoti, na kufuta miguu yako kwa machozi yao huku wakikusujudu bila mwisho.!

Do you know the cost of it?
 
Wewe utakuwa Mkenya au msomalia,Mtanzania mwenye busara na hekima huweka maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi yake binafsi,na LOWASSA analifahamu hilo ametumia busara kuliepusha taifa na vurugu kisa tu madaraka.Hivyo hekima na busara ya mwanadamu ni nusu ya kufahamu mbingu.

Mbona hakuwa na busara kipindi anakatwa?
 
Mimi sii CDM wala CCM. CCM imeiba kura halafu ikajigeuza upinzani. Msiogope kwani mbio za sakafuni huishia ukingoni. Lowassa huyu huyu au ni mwingine unamzungumzia? Omba Mungu kwani Lowassa hakushindwa uraisi. CCM ndiyo ilishindwa angalia tu inavyojichanganya. Mara Zanzibar, mara rushwa, wizi, ubadhirifu, maigizo yasiyoisha. CCM haipo. Kilichopo ni upinzani. Inakuwaje wabunge walewale walikuwa wanapiga ndiyooo bungeni na mkuu wao wa msafara Ndugai (karibu amtoe mtu roho) sasa hivi wanashangilia hapanaaaa! Ni afadhali Lowassa alijinasua mapema kweupe. Waliobaki huko wanabugia matapishi yao huku wakipigania kumtukuza na kuziheshimu ahadi za Lowassa alizotoa wakati wa kampeni.

Mkuu ahadi gani? Zile za Elimu, Elimu, Elimu? Nawapenda bodaboda na mama ntile? Wake up buddy, you are loosing
 
kwakweli busara hasara..bora nisiwe nazo kama ni hizi za kuonewa na kukaa kimya..
 
Sio busara, jamaa ni dhaifu mno kimwili na kiakili,hapo alipo anapelekeshwa na Mbowe tu
 
Hivi si mlitangaza maandamano nchi nzima yaliishia wapi?????????????????????????????????????????????????????
 
Ndiyo ujuwe sasa kwanini mnaitwa nyumbu, huyu fisadi Lowasa hajaibiwa kura wala nini ameshindwa kihalali kabisa ila aliwaaminisha nyumbu kwamba kaibiwa kwa maana kama kweli angekuwa na ushahidi leo hii angeshauanika hapa lkn yuko kimya anajifanya busara, busara tangu lini fisadi kama Lowasa akawa na busara? hiyo busara mbona hakuitumia wakati anatuibia?

Acha uchizi fisadi wewe na roho yako mbaya
 
Lowassa alishindwa kihalali na anajua huu ndio mwisho wa ndoto zake za kuwa rais wa JMT. Pia anaelewa vurugu haziwezi kumfanya yeye atangazwe kuwa rais. Ndio maana kaamua kutulia ale pensheni zake X PM na alinde ka heshima kidogo kalikosalia
 
Jamani uchaguzi umekwisha na tulishasema kuna maisha baada ya uchaguzi, sasa hivi tufanyeni kazi huu umbwiga mnaoendekeza hauna tija.
 
The forsaken truth is just revernging now.Ndo basi tena.
 
Mh. Lowassa nimesikia tamko lako, Police wasipochukua hatua kwa wauaji wa kamanda Mawazo, Ukawa watachukua hatua. Angalau umerejea kwenye harakati. Lakini ulitakiwa uende mbali zaidi ya hapo, ungewapa police deadline, kama hawatachukua hatua ndani ya kipindi cha siku thelathini, kwa mfano.... hapo ungetisha zaidi. And you mean it...
 
tatizo wenye nchi hawakutaka lowasa awe rais ingawa wananchi walitaka awe rais wao...
 
Ngoyayi Lowassa, nini kimekupata? Kwanini umekuwa mtu wa busara tena? Busara itakurejeshea heshima yako au ndiyo itamalizia hata hiyo chembe ya heshima iliyobaki?

Kulikuwa na maana gani ya kutoka CCM kama ulijua kwamba utapoteza uchaguzi na usisabishe homa?

CCM walikudhalilisha kwa kiasi kisichomithilika. Wakakutwisha zigo la Richmond ukahiari kulibeba. Ukapigana kiume hadi Ukashinda hila zao kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM lakini wakaamua kukuchinjia baharini. Uliishiwa na subira, hukuwa na uvumilivu, above all, hukuwa na busara tena. Ulimua kujiengua ccm, liwalo na liwe. Come what may!

Watu wengi sana ndani ya CCM walikusihi usihame CCM. Uwe na busara. Uonyeshe ukomavu. Lakini wewe uliwajibu "There is life out of CCM. .. CCM sio mama yangu..." Ulikuwa ni uamuzi wa kijasiri. Na kweli ulikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo. Kwa sababu, at this point (a point of no return) you had nothing to lose. Ulipoteza uwaziri mkuu, ukapoteza heshima ndani ya chama, ukaitwa gamba. Ukapoteza nafasi ya kuwa mgombea urais wa ccm. Bila kusahau Ulipoteza mali nyingi sana.

Uamuzi wako wa kujiunga na UKAWA niliutafasiri kwamba ulikuwa ni muda wako wa kupambana hadi tone la mwisho la damu. I knew that was your dying point. Maisha yana maana gani kwako kuendelea kuishi nchini Tanzania huku ukiwa dhalili, a loser of everything?A loner? Wakati wako wa kufa kwa heshima kama Kamanda Mawazo, naona unaisha. Utakuja kufa kifo cha aibu, kama ambavyo waoga wote hufa. Wewe ni Shujaa tangu ujana, na ulikuwa na fursa ya kufa kishujaa,umeichezea hiyo opportunity.

Angalia sasa hivi mili yetu inapoa. Ujasiri unatuyeyuka. Hasira zinashuka. Na huyu jamaa anajua. Ndiyo maana anafanya uliyotarajia kuyafanya wewe. Kila sehemu anatulenga. Hatuna budi kupoa. Sisi tuna nafasi ya kugeuza shingo, tukawa washabiki wa upande wa pili. Wewe unayo hiyo nafasi tena? Sumaye anayo? Je babu?

Kwa nini ulizembea? Ukaendekeza ustaraabu wa kikondoo wakati ulikuwa ukipambana na genge la Mafia? You were supposed to take action accordingly on the spot. Live in prison or simply die.

Busara ni nini? Busara ni uamuzi wa kusitisha kuchukua maamuzi magumu stahiki. Kwa maneno mengine ni uoga. Kwa mfano, unamfuma mke wako kitandani mwako akiliwa uroda na jamaa. Hatua stahiki ni nini hapa? Watu wenye busara(waoga) watasema ni kusamehe. Kwa sababu wanaogopa kumtimua mke. Kwa sababu wanaogopa kumwajibisha mgoni. Wanajiuliza swali la kioga "What will happen if... "

Mimi nawachukia watu wenye busara. Hawawezi kutamka kauli ya mashujaa, "Come what may=Liwalo na liwe"

Title ya thread hii nilitaka iwe, "Mh Lowassa, umeamua kuwa na busara?" Ndiyo maana mimi niliandika "NITACHUKUA KADI YA CCM October 30th"

Nawaza kwa sauti.

si uende sasa! na kwanini usubiri hadi hiyo oktober 30 mwakani. kachukue hiyo kadi ya ccm leo uone kama iko chama unahama kitazoofika. ninachojua hatupungukiwi ubunifu hata siku moja huku! vijikosa vipo ndiyo; kuna binadamu aliyekamilika?
 
hivi mh.lowassa huwa anaingia humu?natamani azione comments za humu maana hili jambo linaniumiza sana najihisi km mtoto nilietelekezwa porini!!!!
 
Jawabu la upole hugeuza hasira,bali Neno liumizalo huchochea hasira.

Mtu wa hasira huchochea ugonvi,Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano,na Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyo jibu...bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.

Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa,Hata mpumbavu akinyamaza huhesabiwa hekima,akifumba midomo yake huhesabiwa UFAHAMU..soon Tanzania itabadilika tena bila kupigana vikumbo na police ccm...chamsingi ni uvumilivu tu ili Amani ya KIMUNGU iamue HATMA ya Watanzania.

Nimeupenda ujumbe wako mtumishi. ubarikiwe
 
Back
Top Bottom