Lowassa turudishie maji yetu ya mto Themi

Lowassa turudishie maji yetu ya mto Themi

Unaongelea Arusha sehemu gani wanayotumia maji ya mavi maana mm binafsi mkazi wa Arusha na mboga nalima na wala sijawahi kumwagilia maji ya mavi na wala hakuna anayemwagilia maji ya mavi.

Acha upotoshaji, nenda kumtafuta Harmorapa mnaendana kutafuta kiki!!

Lemara bwawani
 
Mie nimekuja mbio nikijua kuna kampeni ya kumtaka don aturudishie pesa zetu za richmond!
 
Wewe acha kukurupuka mboga zote zinazouzwa soko kuu kutoka maeneo ya Daraja mbili, lemara na sinoni zinanjeshewa kwa kutumia maji ya mavi kutoka bwawa la maji machafu (mavi) na hata migomba inanyeshewa kwa hayo maji na hii yote imekuja baada ya Lowasa kupora maji ya wana Arusha na kupeleka kwa Monduli.
Acha uongo wako
 
Maji ya mto themi yalianza kukau katikati ya miaka ya sitini pamoja na chemchemi zote zilzokuwa kila mahali Arusha Township ya wakati huo
Pale Unga ltd Sunflag palikuwa ardhi oevu na tindiga kubwa sana,vijito vya Naura vilikuwa na samaki wakiwemo kaa
Hivi vote vimekauka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka sana kwa wakazi
Bomba lillilopeleka maji Monduli ni kwa ajili ya kambi mbili za jeshi zilizopo Monduli
Aidha Mamlaka ya maji ya jiji la Arusha limeanza kuchukua maji kwenye chanzo hicho
Lowassa anaingiaje hapo wakati miradi hii inaanza ama alikuwa shule au UVCCM?
 
Miaka ya sitini, sidhani kama ni kweli ila nijuavyo mimi kipindi nipo shule ya msingi Lemara na baadae nikahamia shule ya msingi Themi na hii ni mwishoni mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 mto huu ulikua umefurika maji mengi sana mpaka kufikia maji kuingia kwenye maeneo ya watu msimu wa mvua nasi tulikua tukiogelea kwenye mto huo na hata kuvua visamaki vidogodogo.
 
Ukikulia Arusha na ukawa wa hovyo lazima umekulia Ungalimited, maji kwako ni bora ya tririke mtoni kuliko kuwekwa kwenye bomba? Halafu kama umekulia Arusha hiyo mabomba imewekwa wapi maeneo gani?
 
Ukikulia Arusha na ukawa wa hovyo lazima umekulia Ungalimited, maji kwako ni bora ya tririke mtoni kuliko kuwekwa kwenye bomba? Halafu kama umekulia Arusha hiyo mabomba imewekwa wapi maeneo gani?
Kwahiyo wewe unaona ni sawa mto kukaushwa? Halafu acha kukariri maisha sio kila anaekaa Ungalimited ni muhuni wapo Maproffessor wapetokea maeneo hayo na inakubidi uwaombe radhi wakazi wa Ungalimited. Lowasa turudishie wakazi wa Arusha maji ya mto Themi.
 
Salaam!

Nikiwa kama kijana niliyekulia katika viunga vya jiji la Arusha, Jambo kubwa linalinikumbusha miaka ya nyuma hapa jijini Arusha ni kutiririka kwa maji safi ya mto Themi kutokea katika miinuko ya mlima Meru, hakika maji haya yalikua yakipendezesha jiji ikiwa ni pamoja pia na kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa hali ya chini. Kutoka mlima meru mtu huu ulikua ukitiririsha maji yake kupitia kata ya Sekei, Themi, Lemara na mwisho kumalizikia kata ya Engutoto.

Maji ya mto Themi yalikua na faida zifuatazo kwa wananchi wa jiji la Arusha:

· Kilimo cha umwagiliaji (hususani mbogamboga).

· Kunyweshea mifugo mbalimbali kwa jamii ya wafugaji.

· Matumizi mbambali ya nyumbani (kunywa, kupikia, kufulia n.k) kwa watu wa kipato cha chini.

· Burudani ya kuogolea kwa watoto na vijana.

· Matumizi mbalimbali ya kishule (Shule ya msingi Themi na Daraja mbili).

Ghafla miaka kama ya 2005 au 2006 mto huu ulikauka ikawa hauna maji kabisa isipolkua kipindi cha mvua. Wananchi walifuatilia jambo hili na wakaambiwa kwamba aliyekua Mbunge wa Monduli miaka hiyo (Lowasa) alienda kutega mabomba kwenye chanzo cha maji hayo na kisha maji hayo kuelekezwa kwa wananchi wake Monduli.

Sasa namwambia Muheshimiwa Lowasa umetuachia majanga makubwa sisi wakazi wa Arusha kiasi kwamba watu wanamwagilia mbogamboga kwa kutumia maji ya mavi kutoka kwenye bwawa la maji machafu. Kwa hiyo tunaomba uturudishie maji yetu.
katika udadisi wangu niliwahi kuelezwa na mtu wa monduli kwamba source ya maji ya monduli ni visima virefu vilivyochimbwa arusha. mto kukauka mbona sio themi tu. mito yote iliyokua inatiririsha maji katikati ya arusha kwenye miaka 70 na 80 mbona imekauka.
 
Salaam!

Nikiwa kama kijana niliyekulia katika viunga vya jiji la Arusha, Jambo kubwa linalinikumbusha miaka ya nyuma hapa jijini Arusha ni kutiririka kwa maji safi ya mto Themi kutokea katika miinuko ya mlima Meru, hakika maji haya yalikua yakipendezesha jiji ikiwa ni pamoja pia na kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa hali ya chini. Kutoka mlima meru mtu huu ulikua ukitiririsha maji yake kupitia kata ya Sekei, Themi, Lemara na mwisho kumalizikia kata ya Engutoto.

Maji ya mto Themi yalikua na faida zifuatazo kwa wananchi wa jiji la Arusha:

· Kilimo cha umwagiliaji (hususani mbogamboga).

· Kunyweshea mifugo mbalimbali kwa jamii ya wafugaji.

· Matumizi mbambali ya nyumbani (kunywa, kupikia, kufulia n.k) kwa watu wa kipato cha chini.

· Burudani ya kuogolea kwa watoto na vijana.

· Matumizi mbalimbali ya kishule (Shule ya msingi Themi na Daraja mbili).

Ghafla miaka kama ya 2005 au 2006 mto huu ulikauka ikawa hauna maji kabisa isipolkua kipindi cha mvua. Wananchi walifuatilia jambo hili na wakaambiwa kwamba aliyekua Mbunge wa Monduli miaka hiyo (Lowasa) alienda kutega mabomba kwenye chanzo cha maji hayo na kisha maji hayo kuelekezwa kwa wananchi wake Monduli.

Sasa namwambia Muheshimiwa Lowasa umetuachia majanga makubwa sisi wakazi wa Arusha kiasi kwamba watu wanamwagilia mbogamboga kwa kutumia maji ya mavi kutoka kwenye bwawa la maji machafu. Kwa hiyo tunaomba uturudishie maji yetu.
Duu hayo maji yenu au ya watanzania wote? Dhahabu zikiuzwa wa Mwanza au Mara hawasemi hiyo hela itumike Mwanza na Mara tu. Hivi nyie watanzania nani kawaroga? Watalii wakija Arusha kwani pesa ya utalii hubaki Arusha? Gesi ya Mtwara imebaki Mtwara? Tuacheni mambo ya ajabu. Leo his Ziwa Victoria lina supply maji hadi Egypt chanzo cha maji ni nchi tatu tu na wala hazifaidi sana
 
wew ni selfish wenzako wa monduli walikuwa hawana hata maji ya kunywa ndo maana wakapelekewa sasa wew unataka kuogelea njoo dar au nenda ziwa duluti
 
Wakati Mbunge Lowassa "anafanya" hayo, serikali ilikuwa wapi?
 
Kwahiyo wewe unaona ni sawa mto kukaushwa? Halafu acha kukariri maisha sio kila anaekaa Ungalimited ni muhuni wapo Maproffessor wapetokea maeneo hayo na inakubidi uwaombe radhi wakazi wa Ungalimited. Lowasa turudishie wakazi wa Arusha maji ya mto Themi.
Professor atoke wapi huko ambako hakuna anaemaliza shule. Hayo maji yanayoenda kwa Lowassa yanachukuliwa sehemu gani?
 
Back
Top Bottom