zimwilachi
Member
- Oct 22, 2016
- 40
- 23
Salaam!
Nikiwa kama kijana niliyekulia katika viunga vya jiji la Arusha, Jambo kubwa linalinikumbusha miaka ya nyuma hapa jijini Arusha ni kutiririka kwa maji safi ya mto Themi kutokea katika miinuko ya mlima Meru, hakika maji haya yalikua yakipendezesha jiji ikiwa ni pamoja pia na kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa hali ya chini. Kutoka mlima meru mtu huu ulikua ukitiririsha maji yake kupitia kata ya Sekei, Themi, Lemara na mwisho kumalizikia kata ya Engutoto.
Maji ya mto Themi yalikua na faida zifuatazo kwa wananchi wa jiji la Arusha:
· Kilimo cha umwagiliaji (hususani mbogamboga).
· Kunyweshea mifugo mbalimbali kwa jamii ya wafugaji.
· Matumizi mbambali ya nyumbani (kunywa, kupikia, kufulia n.k) kwa watu wa kipato cha chini.
· Burudani ya kuogolea kwa watoto na vijana.
· Matumizi mbalimbali ya kishule (Shule ya msingi Themi na Daraja mbili).
Ghafla miaka kama ya 2005 au 2006 mto huu ulikauka ikawa hauna maji kabisa isipolkua kipindi cha mvua. Wananchi walifuatilia jambo hili na wakaambiwa kwamba aliyekua Mbunge wa Monduli miaka hiyo (Lowasa) alienda kutega mabomba kwenye chanzo cha maji hayo na kisha maji hayo kuelekezwa kwa wananchi wake Monduli.
Sasa namwambia Muheshimiwa Lowasa umetuachia majanga makubwa sisi wakazi wa Arusha kiasi kwamba watu wanamwagilia mbogamboga kwa kutumia maji ya mavi kutoka kwenye bwawa la maji machafu. Kwa hiyo tunaomba uturudishie maji yetu.