Lowassa: TANESCO jiandaeni kuwajibika

Lowassa: TANESCO jiandaeni kuwajibika

...huyu ndie anaeleweka akitoa kauli kama hiyo, na atawanyoosha kweli,sio yule bendera fuata upepo aliyewekwa bila kujitambua anajua push_up tu.
 
Anafkiri hatujui haya madhila Richmond inahusika, aache kutuhadaa.

Naona hujui unachosema: Kubuma kwa miradi ya MTERA, KIHANSI, KIDATU, PANGANI, BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU, HALE, KIWIRA, MBALIZI, JENERETA ZA UBUNGO, IPTL aka ESCROW, SONGAS, SYBION, KINYEREZI na mingine mingi ni Richmondi ihahusika?
 
Anafkiri hatujui haya madhila Richmond inahusika, aache kutuhadaa.

Tundu lissu alimtaja mhusika wa richmond,sasa unataka kuchokonoa ili sisi tumtaje tena?ng'o !hatujakariri vema vifungu vya sheria!
 
Umeme,Richmond,Lowasa,Kikwete........Magufuli kuwa Raisi utunyooshee hawa watu, nayeye analalamika umeme hivyo tu kweli Lowasa....zaidi ya miaka kumi ile miwili wewe si ulikua waziri mkuu, ukajiuzuru kwa kashfa ya Umeme, na bado hutaki kufafanua hilo, leo unajifanya kanakwamba hujui habari za Umeme nakati ndo kilicho kutoa madarakani......Sawa tu Lowasa hushatufanya sisi wajinga mpaka basi, unabunda tu na Raisi freand wako, hamtuelezi chochote.......Bora Magufuli kauli yake ile niyakweli sio hii ya Lowasa....
 
Mgawo wa umeme umekuwapo nchini tangu mwaka 1992. Siwezi hapa kusisitiza adhari za kukosekana umeme wa uhakika kiuchumi na kijamii. Swali la kujiuliza ni je, hili tatizo litaendelea hadi lini? Jibu la swali hili lipo katika nukuu ya Mwanafizikia na Mwanafalsafa nguli wa karne ya 20 katika nukuu yake hii: "We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them". Tafsiri isiyo rasmi ni "Huwezi kutatua tatizo kwa kutumia akili hiyo hiyo iliyosababisha hilo tatizo liwepo". Maana yake ni kuwa chama hicho hicho kilichokuwa madarakani; mfumo huo huo; na sera hizo hizo vilivosababisha tatizo la mgawo wa umeme havitaweza kamwe kuliondoa.

Maana yake sio chama hicho hicho...... Ni fikra zilezile na huyo Lowassa alikuwa sehemu za fikra zilizooongoza nchi tangia maika ya tisini... Unataka kuja kutuambia nini sasa hapa
 
Mzee wa maamuzi magumu na sahihi ambaye ni mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa Ndg. Edward Lowassa kasema kuanzia tarehe 27 baada ya matokeo kutangazwa TANESCO waanze kuwajibika wenyewe kama hawatashughulikia hali ya umeme ipasavyo.

Lowassa kaonyeshwa kukerwa na mgao usiokoma kwa miaka zaidi ya 10, "kila siku ni mgao, mgao, huu mgao utaisha lini? TANESCO inalalamika, serikali yenyewe inalalamika. Sasa kama serikali na Tanesco wanalalamika na kukosa majibu mnategemea wananchi wakimbilie wapi?...alisema

Ni muda mrefu sasa nchi imekubwa na mgao wa umeme, na mbaya zaidi wananchi hawajui hali hii itakoma lini. Waathirika wakubwa wamekuwa wakina mama wajasiariamali, wafugaji wa kuku, vijana wanaojihangaisha kwa kupata ujira mdogo kama vinyozi wa saloon, vijana wenye ajira za kubangaiza viwandani, mama ntilie n.k

Ni jambo la kushangaza sana kuna mgombea ambaye ni waziri mwandamizi katika serikali hii lakini amekuwa akihaidi viwanda kila wilaya sasa sijui hivyo viwanda vitatumia power bank au?...

NB: Ninapoandika huu uzi tayari umeme ushakatwa..... Kwa hakika nchi inamuhitaji Lowassa kuondoa kero kama hizi....

Lowasa la umeme angekaa kimya tu hii janja ya kupanik usoni moyoni anachekelea na fusadi wenzie tumeishukia
 
hana lolote kazoea kupiga deal, safari hii kapigwa yeye na kina mbowe

Kwanin Unapingana Na Ukweli? Hata Sisi Tanesco Wametuboa Wanakata Umeme Hadi Siku Za Mitihani Kwa Wanafunzi, Tena Ajabu Wanakata Usiku Hata Hatuna "Light Torch",
 
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema iwapo atachaguliwa katika nafasi hiyo, atahakikisha kwamba serikali yake inawafutia mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu waliowahi kukopeshwa kwa ajili ya masomo ya vyuo vikuu.Lowassa anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro jana.---Alisisitiza kuwa serikali yake atakayoiunda, itatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu na kwa wale ambao tayari wanadaiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, watafutiwa kiasi chote wanachodaiwa.

"Serikali yangu itatoa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu bure na wanaodaiwa na Bodi, tutawafutia mikopo yao,"-alisisitiza Lowassa.Kuhusu- tatizo- la- umeme- kukatika- mara- kwa- mara, Lowassa alitoa onyo kwa watendaji wa Tanesco kuwa akiingia madarakani wajiandae kutafuta kazi nyingine kwa kuwa umeme umekuwa ni kero kwa wananchi kutokana na kukatika mara kwa mara pasipo sababu za msingi."Uchumi unasimama kwa kukosekana umeme wa uhakika, uwezo upo lakini viongozi wetu wameshindwa kulitatua,"alisema Lowassa- na- kuongeza:"Ninawaambia Tanesco wajipange baadhi ya watendaji watafute kazi nyingine."--Alisema bila kufanyika uamuzi wa haraka kutatua tatizo la umeme nchini mambo mengi yanakwama na uzalishaji viwandani unadorora na gharama za bidhaa kupanda hivyo kumuumiza mwananchi wa kawaida.

Aidha, akiwa katika Wilaya ya Mwanga ,mkoani Kilimanjaro, Lowassa alisema serikali yake itahakikisha huduma ya maji inapatikana wilayani humo kwa asilimia 100.Alisema anashangaa kuona wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la maji kwa miaka mingi, lakini yeye atalimaliza katika uongozi wake.Wakati huo huo, Lowassa jana alitembelea kaburi la aliyekuwa muasisi wa Tanu na baadaye CCM, marehemu Peter Kisumo.Kisumo alifariki dunia Agosti 3, mwaka huu na kuzikwa kijijini kwao Usangi wilayani Mwanga ambapo wakati wa mazishi, Lowassa hakuhudhuria kwenye mazishi ya Kisumo baada ya msafara wake kuzuiwa na polisi.

Lowassa, ambaye aliongozana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, mgombea wa Vunjo, James Mbatia na mgombea wa Mwanga, Henry Kileo, walipokelewa na kaka wa marehemu, Daniel Mchangila.

Mpekuzi blog
 
Back
Top Bottom