Lowassa, Sumaye waivuruga CHADEMA, Washindana kuunda mitandao ya 2020

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Makada wawili wa chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye, wameanza kutifuana na kuwekeana visasi vya chinichini vya kisiasa, TAZAMA Tanzania limeelezwa.

Mtifuanao huo mpya wa kisiasa wa makada hao, ambao wote walihamia ndani ya chama hicho cha kikuu cha nupinzani mwaka wa jana baada ya majina yao kutupwa nje ya mchakato wa teuzi wa urais kwa tiketi ya CCM, umeelezwa unatokana na mbio zao za urais wa 2020.

Kwa mujibu wa habari hizo, Lowassa na Sumaye, wote wanautaka urais wa 2020, hivyo kila mmoja amekuwa akiendesha kampeni za chini kwa chini na siri kubwa, kuunda mtandao wa utakaorahisisha uteuzi na hatimaye kuwa mgombea urais wa chadema.

Haikuweza kufahamika ni kwanini Sumaye nayeameamua kujitosa kushiriki mbio hizo za urais ujao, ingawa kwa Lowassa ilikuwa inafahamika tangu awali kuwa atajaribu tena bahati yake baada ya kushindwa mwaka wa jana.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya duru za kisiasa chadema, zinasema, safari hii Sumaye ameamua kusaka urais mwenyewe katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020, badala ya kuwa mpiga debe kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita.

Sumaye ametajwa kuwa na mtandao mkubwa tayari wa urais, unaodaiwa kuungwa mkono na baadhi ya vigogo wa makao makuu ya chadema pamoja na viongozi wa kanda tatu zinazoundwa na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtawara, Morogoro, Dodoma na Singida.

“Vita ile ya zamani ya urais kati ya Lowassa na Suamaye ndani CCM, ndiyo imehamia Chadema. Sina uhakika kama Lowassa na kambi yake wanalifahamu hili, lakini nakuhakikishia kwamba Suamaye anaungwa mkono na baadhi ya vigogo wa mtaa a ufipa, kinasema chanzo kimoja cha uhakika cha habari hizi “. Mtaa wa Ufipa, maana yake makao makuu ya chadema, Kinondoni, Dare salaam

Akaongeza “ Mbali nan a vigogo wengi kumuunga mkonoSumaye katika nia yake hiyo, mtandao wake umefanikisha kuwanasa pia viongozi wa kanda tatu muhimu zinazounda mikoa minne ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtawara, Morogoro, Dodoma na Singida.

“John Mnyika huyu ndiye mratibu mkuu wa mtandao wa Sumaye bila shaka unafahamu kwanini imekuwa rahisi kwa Sumaye kumtumia Mnyika. Ni wazi ki9la mwana chadema ana asiyekuwa mwanachadema anafahamu kwa nini

Kwa habari zaidi tafuta gazeti la Tazama Tanazania
 
Makanjanja wa Lumumba mmefulia, hamuwezi lolote. Nendeni mkajadili ya kwenu, mada za kipuuzi hizi,mmekosa kazi ninyi.
 
Sio Lowassa wala Sumaye atakayeupata urais....never....!!!!!! Watafute kijana anayekubalika kwenye chama wamfanyie mentorship ili angalau apambane na chama kubwa.
 
Gazeti lenyewe TAZAMA???!! angalia matoleo 20 ya nyuma ni MBOWE, CHALDEMA BASI hadi
 
Sumaye is very loyal to Lowassa, hawezi kwenda kinyume na Lowassa ndani ya CHADEMA...

Lowassa ndio kashika chadema, na kila mtu anajua hilo... hizi ni habari za uongo tu
 
Kwani kuna tatizo mtu akitaka kugombea URAIS? Hii haina shida, waache wawe wengi then wachujwe abaki mmoja. Mmesahau mlikuwa mnasema Lowassa alipendekezwa kwa mizengwe ya pesa? Sasa kama kuna mitandao ya urais imeanza hiyo ni dalili njema. Utakuaje kiongozi bila kujenga mtandao wa kuku-support? Hata TRUMP alikuwa na mtandao.
 
Back
Top Bottom