Lowassa, Sitta, Kilango wapata pigo kubwa!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Sitta, Kilango wapata pigo kubwa!!!!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by samirnasri, Apr 2, 2012.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kambi ya wale wanaojiita wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama tawala cha CCM imepata pigo kubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki na chaguzi za udiwani katika kata 8 tofauti. Kambi hiyo ilitoa wafuasi wake watatu kushiriki katika kampeni za chaguzi hizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumsaidia mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari. Samuel Sitta ambaye ndio kiongozi wa kambi hiyo alipiga kambi jijini Mwanza na kuongoza kampeni katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kirumba na kushindwa kuwashawishi vilivyo wakazi wa Kirumba ambao walimchagua mgombea wa CHADEMA kuwa diwani wao. Naye Anne Kilango alipiga kambi huko kiwila kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwira lakini naye aliangukia pua kwani mwisho wa siku mgombea wa CHADEMA aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa CCM. Kama hiyo haitoshi, Christopher Ole Sendeka alikuwa mmoja wa wana ccm walioshiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki lakini pia ushawishi wake na ule wa Lowassa na wengine wa ccm haukutosha kubadili mawazo ya wananchi wa Arumeru ambo bila ajizi wamemchagua Joshua Nassari wa CHADEMA kuwa mbunge wao. Matokeo hayo kwa ujumla ni pigo kubwa kwa kambi ya Lowassa na Sitta ambaye wakati Fulani alionekana kuaminiwa na wananchi hasa wakati huu ambapo Samuel Sitta ameshaeleza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sasa wananchi wameonesha kwamba hawana imani hata na wana CCM wanaojipambanua kama wapinga ufisadi. Sasa nani aaminiwe katika CCM????!!!!!!!
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  classic analysis and well thought, big up mjomba wa DS.
   
 3. Y

  Yassin Madiwa Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes wakakae wakijua wako ndani yachama dhaifu, watoke wajiunge na CDM wapambane nje hawawezi kujifungia ndani na kusemana kwa maovu ndani ya chama wakitoka nje wanasema Kidumu cha cha mapinduzi" If can not fight withiin the system then get out Unafanya nini" tuendako ukivaa jezi ya kijani ushujaa wako automatically unaporomoja

  Pole CCM na Hongera CDM
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  utawaamini kwa lipi hakuna hata mmoja ndani ya ccm unaeweza kumuamini wenyewe tu hawaaminiani........ kila baya ni lao,,,,sumu ufisadi ujambazi wizi uchawi uwongo uliopindukia unafiki we angalia tu hili la umeme wala ukiulizwa darasani kama ni mtihani huwezi kuwa na jibu sahihi
   
 5. R

  Real Masai Senior Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawana lolote..Wote wana CCM lao moja hakuna aliye msafi.Hapa tunaitaji mabadliko kya dhati na CDM ndiye mkombozi wa Watanzania
   
 6. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbona hata kambi ya LOWASA imeangukia pua tu? In fact watu wamekosa imani na CCM
   
 7. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama wao ni wapambanaji wa maovu wanapata wapi nguvu ya kuwasema Wapambanaji na wapinga uovu wengine kama CDM na wanaharakati wengine. Mimi naona bora wale mafisadi wanaojulikana kuliko hawa wanafiki wanajiita wapambanaji na mara wanatetea chama chao ilikulinda maslahi yao binafsi( UBUNGE na UWAZIRI).
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  mpinga ufisadi anayepanda jukwaa moja na fisadi ni fisadi pia.
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nadhani uchambuzi makini lakini kwa Arumeru mashariki hapana. Arumeru mashariki tayari mgombea alikuwa kambi ya Lowasa ambapo ni tofauti na Sitta.
   
 10. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HUWEZI KUPAMABANA NA MWANACCM FISADI ILI HALI MNAKAA PAMOJA,MNAKULA PAMOJA WATANZANIA SI WAJINGA HIVYO OLE SENDEKA HAWEZI KUSJAMBULIA LOWASA WAKATI MWISHO WA SIKU WANAJIFUNGIA NA KUHESABU MAPATO PAMOJA,HATA SITTA HAWAZI KUWASHAMBULIA MAFISADI AMBAO NI RAFIKI WA ALIEMTEUA NAE AKAKUBALIWA KUTEULIWA. Nawatakia safari njema CCM hakuna msafi anaeweza kuwaambia watanzania atabadili hali ya utawala hali yupo ndani ya utawala mbovu.
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Umesema neno. Huwezi kupinga ufisadi, ukaenda kupanda jukwaani na fisadi Lowassa, ujue utawakera wananchi. Tena CCM kampeni zao waliogopa kusema mafisadi, sasa wananchi wakaona wanawaona mabwege, Siyoi (aka mkwe) alithibitika kutumia rushwa, CCM wakazidiwa kete na Lowassa (sijui walilamba ngapi) wakampitisha na wakaenda kumkampenia, sasa hapa hakuna aliye CCM anayeweza kusema kitu hapa, wote wangegoma kwenda Arumeru kama Nyerere alivyogoma Musoma akashinda Ndobho wa NCCR-Mageuzi
   
 12. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,034
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Iloangaka sio kambi ni chama cha majamawazi mkuu we vipi chichiemu imegeuka kambi tena ?. Kambi ni kitu kidogo sana. Chama ni kitu kikubwa tumeangusha ccm tena full mkoba .yani .mkapa. Sita el. Kilango. Ole sendeka.(nenda kapigane).wasira tyson wao chali. Lusinde na matusi yake. Bila kusahau mwigulu .watu awakujali tunguli .za maji mafupi.. Wamendwa huyu BOY WA MZUNGU haaa haaa haaa....uku ifakara plesha inapanda plesha inashuka kwii kwii kwii huu hushindiumekuja siku mbaya sana j3 ingekua j 2 mida hii ni monde tu K4c chama cha demekrasia maendeleo
   
 13. v

  vngenge JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  E.L bado ana nguvu na anakubalika kwa wananchi, Atakumbukwa kwa mengi kuumwa kwake kumechangia kushindwa. Pengo lake linaonekana. Mzee wa vitendo hakika ndo karata ya mwisho 2015. Wanasiasa watendaji kama huyu mzee namfananisha na Rais Kagame.Maneno mengi co kipaumbele cha kizazi hiki. Action speeks louder than words. Lwaigwanani for presidency 2015
   
 14. o

  obseva JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 450
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 80
  It is the time for change,change and change, change is irresistible, nonnegotiable and intolerable, when people want change you can not ask them to wait, either you have to follow changes or you have to quite!!!!. GOD Bless Tanzania and GOD bless Tanzanians.
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280

  Hakika saa ikivunjika mshale haisomi majira kamwe.
  Samahani mkuu, how old are you??
   
 16. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  This is not a classic analysis...hata siku moja haiwezekani sitta kuwa kambi moja na lowassa...lowassa ndiye aliweka kambi ymtu wake arumeru....ole sendeka alisharudi kny kambi ya lowassa zamani sana kwani nimbunge maslahi ancheki upepo unavovuma.....so ni kambi mbili za lowassa(arumeru) na sitta (kirumba na mbeya )ndo zimeshindwa.......
   
 17. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hao ni wapambanaji wa maslahi binafsi, hawana lolote.
   
 18. J

  Juma Hamis Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ARUMERU alikuwapo fisadi LOWASA na ndiyo maana wananchi wakatoa somo kuwa hataki Tanzania yenye mafisadi,mzee sitta anaipenda CDM ndiyo maana alikataa kuiba kura kama walivyopanga magamba,mzee ni msafi sana.
   
 19. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hawana lolote hao! wanafiki watupu, malengo yao wote ni kutafuta uongozi somewhere.
  HUWEZI KUPAMBANA NA UFISADI UKIWA NDANI YA CCM! hilo hata wao wanalijua, utaanzia wapi wakati mwenyekiti wao ndio kiongozi wa ufisadi?
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Waende CHADEMA kufanya nini? uwezo walionao hawa ni kuboa chama tu, acha wakimalizie malizie CCM kwanza, kwa umri wao wakiimaliza kazi hii itatosha kwao kupumzika.

  Na zaidi, hawa watu wanastahiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa matumizi mabaya ya mali ya UMA kuandaa taarifa ambayo waliiminya na kutoa taarifa pungufu Bungeni kwa misingi ya kuokoa serikali.Ni vigeu geu wanaostahiri hadhabu hawa
   
Loading...