Sidhani kama Lowassa alikuwa muumini wa serikali tatu.
Hebu msikilize hapa anavyopinga serikali tatu!
No matter what he was. Kinachojalisha sasa ni mwelekeo wake na nia yake ya kuongoza mabadiliko.
Kama alikuwa muumini wa serikali tano kumi, mbili hata nne, ni sawa na wengine wenye mitazamo tofauti ambacho ni kitu cha kawaida tu katika jamii. Cha muhimu ni kwamba sasa amekwenda kwenye mstari wa Wananchi kama UKaWA inavyotka.
Lowasa hatafanya ya kwake ila atafanya ya UKAWA sawa na vile kila fisadi, jambazi na muungwana watakavyolazimika kufuata sera za UKAWA kwa hiyari ama kwa lazima.
TUNATAKA MABADILIKO NA MABADILIKO YANAPATIKANA UKAWA!. ukawa si ccm wala mtu binafsi.
Kwa hiyo viongozi wasio na dhamira ya kweli juu ya wanaowaongoza isipokuwa kutekeleza mahitai ya vyama vyao kwako sio tatizo??!!
Sidhani kama Lowassa alikuwa muumini wa serikali tatu.
Hebu msikilize hapa anavyopinga serikali tatu!
Kuhusu Katiba, alisema yeye ni muumini wa Serikali Tatu zitakazosaidia kuimarisha Muungano na kwamba msimamo wake huo aliouonyesha tangu miaka ya 90 wakati wa harakati za kundi la G55.
Alisema suala hilo litafafanuliwa vizuri wakati wa uzinduzi wa ilani ya uchaguzi Jumamosi wiki hii na wakati wa kampeni.
Mkuu OLESAIDIMU hapo kwenye bluu umenilisha maneno
Ukijaribu kunielewa kidogo ninachomaanisha ni kuwa, katika mazingira ya sasa na uhalisia uliogubika bunge la katiba, ni dhahiri kuwa kuna watu waliokuwa na msimamo tofauti na msimamo wa chama lakini kwa sababu ya ukweli kuwa political aspirations zao zinabebwa na maamuzi ya chama, mtu anaona ngumu ku-defect msimamo wa chama na analazimika kuufuata huo mkumbo ili mwisho wa siku asionekana kuwa "siyo mwenzetu" na kuhatarisha muelekeo wake kisiasa
Hili lilikumba pande zote...hata hao UKAWA wenyewe siyo kweli kwamba wote walikuwa wanakubaliana na huo msimamo (bila shaka unafahamu baadhi ya wbunge wa UKAWA ambao walionesha msimamo wazi na wengine hawakuonesha wazi) lakini kwa sababu ya mazingira ya "maamuzi ya wengi na ya pamoja" unalazimika kwenda na mkumbo hata kama hukubaliani nao kifalsafa
Kwa kusema haya, msingi wangu ni kuwa hili ni kosa....kushindwa kuonesha msimamo wako utakaoenda kinyume na msimamo wa chama ambacho ndicho kimeshika turufu yako kudumu kwenye siasa.....
But in all honest, hata kama ungekuwa wewe......heading to elections....una aspiration za kugombea ubunge au urais...unafahamu wazi walioshika turufu yako wana msimamo tofauti na ulionao...bila unafiki....msimamo utakua kufuata mkumbo ili "walioshika makali" wasije wakakukata
Mimi nisichoelewa watanzania ni kitu kimoja tu kwamba CCM pamoja na mengine wananalalamikia undugu na mgombea kutoka "mfukoni", sasa kama haya ni mabaya na hayatakiwi sijui kwa nini watu wanapohoji kama hayo hayawezi kutokea na upande B majibu yanakuwa yale yale ya kiimani tu. . . . .
Mtu ni mtu tu hatakiwi kuaminika moja kwa moja haswa mtu mgeni, watu wakiuliza wajibuni tu maelezo yatahitajika saana tu, undeni task force kabisa yawepo majibu, hii habari ya "atafuata tu". . . . .ni ya kimatumaini zaid kuliko uhalisia. . . . .
We unadhani Nkurunzinza mwanzo hakuaminiwa?!! Mbona kageuka? ?!!!
Mtu anapoamua kubadili mawazo juu ya jambo linalohusiana na msimamo au kanuni fulani ni lazima awe na sababu za msingi za kumfanya kubadili mawazo. Kubadili mawazo kwa sababu ya sababu fulani za msingi ni jambo la kawaida na ni sehemu ya maisha, na hasa katika siasa. Kwa mfano, mtu akiamua kubadili mawazo juu ya suala la Muungano kwa mfano ni lazima ana sababu; kwamba alichokuwa anaamini kilikuwa hakina msingi na sasa ameona mwanga fulani. Lowassa anaweza kweli amebadili mawazo kwa sababu sasa ameona mwanga.
Lakini katika mazingira ya siasa za sasa ni vigumu kuona jinsi gani ameweza kugeuza mawazo baada ya kupewa nafasi ya kugombea isipokuwa amekubali kubeba mawazo ya wale ambao sapoti yake anaihitaji ili kuweza kwenda Ikulu. Kwa sababu hiyo itambidi aibeze CCM, aseme kinyume na yale aliyoyasema akiwa CCM na itabidi ajioneshe kuwa sasa amevaa joho jipya la upinzani. Kama hili ni suala la moyoni au la kisiasa tu hakuna anayejua. Isipokuwa angalau kama ametamka kwa kauli yake basi inabidi tukubali kwa kauli yake hiyo. Ila akishinda au kushindwa ndio tutajua anasimama wapi hasa kwani akishinda halafu akaamua kutokutoa full autonomy na akasimamia suala la Serikali Mbili kama alivyofanya akiwa CCM CDM watamfanya nini?
Siyo imani. Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana, ni hakika ya mambo yatarajiwayo. Sasa lipi hapa linalohitaji imani? Hujasikia mwenyewe akisema atasimamia rasimu ya katiba ya Warioba ambayo ndiyo msingi wa UKAWA? Hujasikia akisema namna ccm haifai tena kuongoza nchi? Ulitaka afanye nini ili ujue kwamba yuko chini ya UKAWA na si yo kama ccm ambayo raisi anajiweka juu ya katiba?
Huwezi kupiga ramli kwamba Nkurunzinza atakuwa sawa na kiongozi wa UKaWA. UKaWA haimpi mtu mmoja kujiamulia anachotaka kufanya. Kama ni u Nkurunzinza, basi huo mfano wake ni Ccm na kikwete wenu.
Kama unaswali lolote lile, wewe uliza na si kuanza kuwaambia eti waunde task force yakujibu maswali. Ukawa siyo wapika maneno kwamba kutoa majibu hadi iwe task force.
Wewe uliza swali ulilonalo utajibiwa precisely!. Nawala hilo haliisafishi ccm wala kuiipa legitimacy ya kulazimisha uraisi wakati Watanzania tumeikataa!.
Kama Lowassa katamka hivi hadharani nakubali kuwa ameanza kuelewa. Sasa nasubiri afanye jambo jingine. Akiri, hadharani kuwa Richmond ilikuwa ni makosa na ndio maana alijiuzulu kama Mkuu wa Serikali. Aombe radhi wananchi kwa yote yaliyotokea juu ya hilo na kwamba akipata nafasi ya kulisimamia upya suala kama hilo asingerudia makosa hayo. Aachane na mambo ya kama alihusika au la! Richmond ilitokea akiwa Waziri Mkuu- kwa vovyote alihusika ndio maana alijiuzulu. Akifanya hivi kura zitamfuata kama mafuriko ya Mwanza!
natangaza rasmi kuwasamehe wale wote watakaopiga goti na kukiri makosa yao juu ya uharamia walioitendea rasmi halali ya wananchi kupitia kwa tume ya warioba (msamaha huu haumhusu chenge )You are against wananchi if you don't support what they die-hard support.... Brilliantly played U-turn by Mr. Lowassa.
Mkuu,Hayo maneno kaenda kuyasemea kibanda maitiiiii...mwanza,dar na mbeya hakusema,anajua ndio wanachopenda kusikia watu wa kibanda maiti.
Mkuu,Ni bora ale peke yake kuliko lile kundi zima la ccm aka mchwa.
Alipojiunga na vhama chenye msimamo huo ndio unapaswa kuwa msimamo wake pia. Je mlitarajia aende huko awabadilishe msimamo uliowaleta pamoja?Political U-turns not so bad... provided they work! We all know voters also do U-turns all the time!
Is it time to applaud politicians who U-turn?
If we look at other side, U-turn creates the impression of lack of grip and direction, and chaotic decision making to a politicians. Now, Mr Lowassa is open to attack, criticism, and ridicule from the opposition to Three tier government.
Lowassa U-turn is not new, politicians will promise just about anything to get elected. Unfortunately, as we know all too well, most of these pledges are consistently forgotten and broken, swept under the rug until the next election cycle.
Nawaza tu kama hii U-turn ingetokea kama angekuwa amevaa nguo za kijani na njano zenye nembo ya jembe na nyundo!
Mpaka Uchaguzi upite, tutaendelea kusikia mengi kutoka kwa wanasiasa wetu!
Kwa hiyo akisema ndio nini??!!
Wangapi wamesema??!!
Yaliyosemwa na yaliyotendeka uwiano ukoje??!!!
Kama kasema na wewe unasisitiza kwa alaiyoyasema hiyo sio imani??!! Kama sio hii ni nini????
Nkurunzinza anaweza toka pande yeyote kati ya vyama vinavyotaka kutawala na hilo ndio angalizo kwa yeyote mwenye akili sobber as compared na nyie wenye vyama na mnadhani kila anayehoji basi lazima awe na chama!!!!
Inasikitisha sana kuona watu mkihojiwa mnaanza ooonh CCM yenu mara ACT yenu. . . . .Hii mnaitoa wapi phobia isiyo na mashiko??!! Unadhani kila aliyemo humu ni mwanachama wa chama fulani??!!!
Legitimacy haiji kwa upande mmoja kuponda mwingine NO. . . . . Legitimacy ni matendo na kauli zinazotekelezeka. . . Ni zao la historia. Kila upande utajijengea legitimacy yake hilo halina mjadala isipokuwa kwa asiyekuwa na akili timamu tu!!!
Acha uongo vp kuhusu Warioba na Polepole n wanachama wa chama gani kweli! Hakuna jipya n kutafuta madaraka tu kwa njia yoyote
Sioni la kushangaza hapo, kama ni u turn Lowassa alishapiga tangu siku alipojiunga na UKAWA kupitia CHADEMA, Lowasa alijua UKAWA is primarily about the new constitution, hapo ndio mzizi wa kila kitu... yaani hakuna katiba ya UKAWA hakuna UKAWA, hapo ndio palipofanya watu waweke kila kitu pembeni waungane, hivi vyama vinne vina itikadi tofauti na mengi tu wanayopingana na kupishana wenyewe kwa wenyewe, ila vinakubaliana katika mambo mawili makuu...la kwanza rasimu ya katiba, la pili kuitoa ccm madarakani, wanachama wa hivi vyama wengi wao ni walala hoi ambao bila kujali tofauti za itikadi zao wanaishi maisha magumu chini ya utaratibu uliopo unaozidisha gap kati ya matajiri na maskini na kunyanyasa wale ambao ni tishio kwa utawala wa chama tawala hili tayari linawaunganisha pamoja. Lowasa kwa kusema mwenyewe kwa kauli yake kwamba atasimamia katiba iliyotakiwa na wananchi na iliweka UKAWA pamoja ni jambo la baraka kwa nchi hii, Lowasa asingeweza kwenda UKAWA kusimamia katiba iliyopitishwa na ccm hali akijua wazi ukawa ni Umoja wa Katiba ya Wananchi.
tunaihitaji hii katiba mpya ya wananchi like never before, katiba iliyopitishwa na ccm haitupeleki popote hata tumweke pale magogoni malaika original fresh kutoka mbinguni.
Alipojiunga na vhama chenye msimamo huo ndio unapaswa kuwa msimamo wake pia. Je mlitarajia aende huko awabadilishe msimamo uliowaleta pamoja?
Ungeshauri ccm wapigane na mfumo na siyo watu wanaowaita magamba. Nina hakika kama tatizo lingekuwa watu ufisadi ungekuwa umeisha siku nyingi.Ninachokiona hapa kuna haja kubwa sana ya kutoa elimu juu ya mabadiliko. Watu wenye uelewa mdogo hawawezi kutoa hoja za kuboresha zaidi sana wanaonyesha hofu ya mabadiliko. Wanaogopa kupoteza ama kutokea kwa wasiyoyojua.
Lakini jambo la ajabu, kuna kundi moja ama kwa makusudi au kwa ujinga, linajaribu kuwaaminisha watu kwamba mtu akihama kutoka chama kimoja na kwenda kingine, basi anahama na sera, mila na mazoea ya kule alikokuwa anayapelekea kule anakoenda. Na hili ndilo linawafanya wengine waone kama Lowasa kaenda kuharibu ukawa, na ccm wanaona kama ni kete ya kuwafitinisha wapenda mabadiliko kwamba Lowasa anahamisha ushetani wa ccm na kuuambukiza kwenye UkaWa.
Watu wanapaswa kujua wahamiaji wote wanakwenda CHaDEMA kwa kuwa wameona ni chama makini chenye misingi imara na uwezo wa kuongoza mabadiliko katika nchi. Na baada ya kuona hawaridhiki na mifumo iliyopo ikiwa ni pamoja na kunyimwa fursa za kuwaza mabadiliko ndani ya vyama vyao, wanatafuta uwezekano huo nje ya ccm.
Lowasa anayetumiwa kwa mema na mabaya, amesema alitafuta fursa za kufanya mabadiliko ndani ya ccm lakini alinyimwa na akaona mahala sahihi pa kufanay hayo ni CHADEMA. Sasa kwa nini watu wasiamini kwamba anakohamia anakwenda kuungana na manguli aliowakuta kuongeza nguvu ya mabadiliko?
Kwa nini waamini kwamba Lowasa ataharibu kundi lote la waadilifu wa UKAWA, pamoja na nia yake njema na wasione kama kundi la waadilifu wa UKaWA ndiyo misngi wa mabadiliko ya kuwabadilisha wtu mmoja mmoja na chi nzime kutoka kwenye u ccm kwenda kwenye Utanzania?
Lowasa should not be an agenda now. Tumwone yeye na wageni wenzake, pamoja na wenyeji wao kwamba wanafanya kazi moja ya kulikomboa taifa kwa misingi ya UKaWA na si uozo unaonuka kule ccm.
Ccm haipaswi kupewa nafasi ya kuendelea ku create confusions na hofu eti Lowasa amehamishia ufirauni CHADEMA kwa kuwa hata yeye anasema anasimamia katiba ya Warioba? What else? Ukawa siyo ccm kila mtu aamue kufanya atakacho. Kla mmoja anafanya vile UKaWA unataka.
Pengine kwa kuwasaidia ccm, ni vizuri wakashughulika na mafisadi wao walioota magamba sugu huko ccm ambao wameapa kuendeleza ufisadi at any cost.
UKaWA, waachie wapigania ukombozi waliopo na wanaoungana na hili jeshi ili kuongeza nguvu na kasi ya ukombozi.
Siyo imani. Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana, ni hakika ya mambo yatarajiwayo. Sasa lipi hapa linalohitaji imani? Hujasikia mwenyewe akisema atasimamia rasimu ya katiba ya Warioba ambayo ndiyo msingi wa UKAWA? Hujasikia akisema namna ccm haifai tena kuongoza nchi? Ulitaka afanye nini ili ujue kwamba yuko chini ya UKAWA na si yo kama ccm ambayo raisi anajiweka juu ya katiba?
Huwezi kupiga ramli kwamba Nkurunzinza atakuwa sawa na kiongozi wa UKaWA. UKaWA haimpi mtu mmoja kujiamulia anachotaka kufanya. Kama ni u Nkurunzinza, basi huo mfano wake ni Ccm na kikwete wenu.
Kama unaswali lolote lile, wewe uliza na si kuanza kuwaambia eti waunde task force yakujibu maswali. Ukawa siyo wapika maneno kwamba kutoa majibu hadi iwe task force.
Wewe uliza swali ulilonalo utajibiwa precisely!. Nawala hilo haliisafishi ccm wala kuiipa legitimacy ya kulazimisha uraisi wakati Watanzania tumeikataa!.