Dr. Willibrod Slaa
Public Figure
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,524
Wana JF,
Propaganda haina nafasi katika vita dhidi ya Ufisadi. Tarehe 15 September, 2007 tulisimama kwa hiari yetu, tukiwa na akili timamu, tukijua tutatukanwa, tutatishiwa maisha,tutahukumiwa waongo na wazushi, tutaambiwa tutaburuzwa mahakamani. Bila uwoga tulisimama na kutaja List of Shame.
Leo, hakuna wa kututmia, wala mwenye uwezo wa kutununua. Kama hatukununuliwa, wala kutishiwa haitatokea hata sasa. Tutaongeza majina mengine kwenye List of Shame kwa hiari yetu, tukiwa na dhamira safi, bila kumsingizia mtu, wala umbeya. Wanaobisha watoke hadharani, hata wale ambao kwnye macho ya jamii wanaonekana hawana kitu. Inaonyesha tu jinsi watu wasivyojua mapana ya neno "ufisadi" kama tulivyolitumia. Wasichojua wengi ni kuwa fedha za EPA zilitoka kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja ni "Vijimemo". Nilikuwa nasubiri wenye vimemo hivyo watoke hadharani kukanusha. Bado tunawasubiri. Hapo ni patamu kwa kuwa kama hawaknufaika nayo binafsi, basi watatueleza vimemo vyao vilipotoa hela hizo hela za umma zilipelekwa wapi. Hii ndiyo kai tunayofanya siyo kumsafisha yeyote.
Kama ni kauli niliisha kumwuliza Lowasa Bungeni (check your Hansards properly) mwaka jana baada ya Bunge kufunga mjadala wa Richmond alieleze Taifa kwanini alijiuliza wakati "aliyeidhinisha: Richmond kwenye Baraza la Mawaziri bado anadunda. Kuvua magamba hakutakuwa kamili kama kila mmoja wao (not excluding any of them) hatawajibika kwa kiwango cha kuhusika kwake. Katika hili tueleweke. Narudia tutaendelea kupiga kelele mpaka wote wahusika wajivue "Gamba", ili kujivua Gamba kuwe na maana inayoweza kueleweka japo kidogo. Niliwahi kutamka JK anavyohusika na Dowans, wamejikanyaga wote, lakini wenye macho leo wanaelewa Role ya JK ilikuwa nini.

Hii habari inathibitisha kuwa ni kweli baadhi ya viongozi wa CHADEMA, CUF, Tanzania Daima na magazeti mengine wako mfukoni mwa mafisadi... Tanzania kweli safari bado ndefu kufikia uhuru kamili.