Lowassa: Nimeshawishika, Nitagombea urais...!

John Okello

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
459
Reaction score
207


Katika Kurasa za magazeti ya Leo zimepambwa na tarifa mbambali za kurasa za mbele za magazeti zinaonyesha dhahiri Edward Lowassa kukubali kugombea Urais, Okello nimelifuatia suala hili kwa karibu mengi nimeyapata kutoka kwa Mashekh wa Bagamoyo. Ni ukweli dhahiri upande wa Jakaya katika dhamira yake ya dhati ni kumkabidhi Edward Lowassa ikulu ya magogoni.

Mengi katika vipaumbele vya ujumbe wa Jakaya katika ni kuhakikisha Edward Lowassa anaendeleza Yale ambayo ameyaacha ikiwemo elimu, Afya bora, miundombinu na kufuta umaskini kwa Watanzania wote.

Kumejitokeza makundi mbali mbali yakimtaka kugombea Urais, yeye binafsi amesema anafarijika kuona Watanzania wanasimama nae katika hili, mbali historia ya uongozi wake uliotukuka basi hii nafasi ya Watanzania kumuomba atangaze nia inampa nguvu hasa Dk. Jakaya kumtumia ujumbe mzito.

MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.

 
Waziri mkuu aliejiuzulu,Edward Lowassa, ametangaza rasimi nia yake ya kutaka kugombea uraisi kupitia CCM baada ya kuombwa kufanya hivyo na masheikh wapatao 50 kutoka Bagamoyo ambao pia walimkabidhi sh 700,000 kwa ajili hiyo.

Chanzo:Magazti Channel 10

My take:
Mbinu hizi anazotumia Lowassa ndio zitakazommaliza maana nina hakika wenzake ndani ya chama hawazipendi ingawa si kosa na ni utamaduni wa muda mrefu tu.
 
Anausaka urais kwanguvu zote huyu jamaa kias ananipa mashakha anataka kutufanyia nn watz…!!!
 
Lowasa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Atasababisha wananchi wale nyasi
 
Anausaka urais kwanguvu zote huyu jamaa kias ananipa mashakha anataka kutufanyia nn watz…!!!
Anataka kulipa fedha alizokopa kugharamia harakati zake za kisiasa
 
nani achague huyu senior Fisadi????
 
Huyu bwana anatupa mashaka maana anatumia nguvi nyingi sana kutaka kuingia Ikulu.

Ninawashangaa sana wanaomuunga mkono huyu bwana bila kujiuliza ana nia gani hasa na hii nchi.
 
Msimhusishe JK na tamaa ya madaraka ya fisadi Lowasa. Lowasa hauziki hata kwa senti tano
 
Hakuna ndani ya CCM kwa sasa mwenye ubavu wa kumzuia EL pamoja na mabaya yake. Hata mwenyekiti "wetu" pale magogoni inavyoelekea "kaufyata" na hana namna ya kumzuia. Kwa kifupi EL na timu yake wamewazidi ujanja........kina Mangula wao wanahangaika na wapinzani lakini tayari wameunguza vidole.....ukifuatilia sana sababu ya hilo "dili" kumbumbuluka unawaona EL na timu yake kwa mbaaali!
 
Inasikitisha sana kuona MTU aliyeshindwa uwaziri mkuu mnataka kumpa uraisi ni hatari sana. CCM chonde chonde tuondoleeni hatari hii ya Lowasa mbeleni mwetu.

Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Mwl Nyerere alishatuasa kuhusu watu watumia fedha ni wa kuogopwa ka ukoma.
 

Hivi Leo Ndiyo Anatangaza au Sasa Ndiyo Anatuthibitishia?
 
Pigeni kelele tu mwezi wa kumi na moja anahapishwa kuwa rais, lowasa is unstopable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…