"NIKO TAYARI KUFA NIKITETEA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA"
Kama kwaida ya CCM wao hushangilia kila kitu na kuwaaminisha viongozi wao kwamba wanafanya vizuri hata kama wanaelekea shimoni. Ndiyo! Kwani wanaomshangilia Magufuli si wale wale waliomshangilia Kikwete? Naamini hata kama Magufuli angewaudhi namna gani hili la kuzuia mikutano ya upinzani watamshangilia mpaka jino la mwisho litaonekana. Naambiwa pia Dkt Tulia alimwagiwa sifa kedekede jana kwenye kikao cha CC ya CCM.
Hata hivyo napenda kuwakumbusha viongozi wangu hawa kwamba wanaposhangiliwa leo na hawa wanaoshangilia kila kitu wajiandae kuzomewa au kukejeriwa na hao hao wanaowashangilia. Kama hawaamini maneno yangu wamuulize mzee Kikwete. Lakini pia wakumbuke kwamba kuua upinzani si kazi rahisi, kama hawaamini wamuulize mzee Mkapa na Dr Salimin. Walitumia nguvu zao zote kuua upinzani ukashindikana.
Natabiri kipindi cha cha Magufuli kuibuka kina Dr Besigye wa Tanzania. Dr Besigye alivunja rekodi ya dunia kwenye kampeini za Uganda alipokamatwa na kushitakiwa mara 7 kwenye mwezi mmoja na leo tunavyoongea yuko ndani kwa tuhuma za uaini. Jana nilimuona Lowassa akisema yuko tayari kufa kutetea katiba mpya na kudai tume huru ya uchaguzi!
Kuna aliyetegemea kauli nzito namna hiyo toka kwa mwanasiasa mstaarabu na mpole kama Lowassa?