Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Mchambuzi George Hope wa Uingereza, aliuchambua Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, uliofanyika Mei, 7, mwaka huu kuwa ulikuwa mkubwa kuliko siasa za vyama, andiko lake lilibeba kichwa; This Election is far bigger than Party Politics.
Vilevile mchambuzi Chris Trueman wa Marekani, aliwahi kueleza kuwa siasa za vyama zinapotea na badala yake nguvu ya ushawishi wa mtu mmoja inakuwa mtaji mkubwa. Kwa maana mwanachama wa Republican siku hizi humpigia kura mgombea wa Democrat kutokana na mvuto wake.
Kwamba, Barack Obama wa Democrat aliweza kumshawishi Colin Powell wa Democrat na kutangaza hadharani kwamba anamuunga mkono, akaahidi kumpigia kura na kushawishi wana Republican wengine kumchagua Obama. Powell alikuwa alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika muhula wa kwanza wa Rais George Bush.
Powell alisema alishawishika kumuunga mkono Obama kwa sababu hotuba zake zilimpambanua kama mtu mwenye maono ya kiwango cha juu katika kuistawisha Marekani.
Binafsi naunga mkono maneno hayo kwa kuchukua hoja hizo za Hope na Trueman kisha kuzioanisha na hali halisi nchini. Bila shaka, nguvu kubwa ya mgombea wa Chadema na Ukawa, Edward Ngoyai Lowassa, imekuwa na mapinduzi makubwa.
Kwanza tuseme kweli kuwa matokeo ya sasa yanadhihirisha kwamba Lowassa ni zaidi ya Chadema, na msuli wake ni mkubwa kuliko wa Ukawa. Tunaweza kukubaliana kwamba safari ya Lowassa Chadema imechagizwa na udhaifu wa sheria za nchi.
Laiti sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zingekuwa zinaruhusu uwepo wa Mgombea Binafsi, Lowassa asingeingia Chadema wala asingefunga ndoa na Ukawa. Angesimama peke yake na mshikemshike huu unaonekana sasa, ungekuwepo bila punguzo.
Lowassa hakuhitaji kuingia Chadema kwenda kumpa unyonge Dk. Willibroad Slaa aliyeamua kujiweka kando na chama chake, wala hakuwa na kusudio la kwenda kumkimbiza Profesa Ibrahim Lipumba Cuf na Ukawa. Lowassa hakuwa na namna.
Anaufikiria Urais, na kwa njia anazopita, inamtaka awe mcheza mpira mgumu (a hardball performer) ili kufanikisha malengo. Hata kama anajua anaumiza wengine, hana namna ya kuwatuliza. Kokoro au mkwabo kwa lugha ya Kigoma, hukusanya na visivyohusika.
Jinsi Lowassa anavyouelekea Urais, ni sawa na askari anayetumia kombora la kivita kumuua mtu mmoja, linapolipuka huua na kujeruhi walio karibu na mlengwa. Pale alipo Lowassa anamhurumia Slaa, anamsikitikia Lipumba lakini hana njia nyingine za kuwafurahisha. Mgombea binafsi angekuwa anaruhusiwa, pengine asingewajeruhi.
Kufikia hapo hatutapingana kuwa Lowassa amebadili siasa za nchi. Amekuwa ni kiungo kitamu katika uchaguzi wa mwaka huu. Amesababisha mvumo mkali ambao umewazindua hata wanaopenda kuilalia siasa, nao wameshtuka na kuifuatilia.
Amekuwa sababu ya walevi wa michezo na burudani, waliokuwa wakiita siasa uzushi, nao sasa ni washereheshaji wazuri wa mada za kisiasa vijiweni, ndani ya familia na zaidi kwenye mitandao ya kijamii.
Lowassa ni kiungo kinachoweza kumpa hamu ya chakula asiyejisikia au aliyekinahi. Ndiyo maana waliokuwa wakiisema vibaya Chadema kuwa chama cha hovyo, siku hizi ndiyo kimbilio lao. Rejea matamko ya nyuma ya Dk. Milton Makongoro Mahanga, Goodluck ole Medeye na wengineo waliomfuata Lowassa Chadema.
John Guninita aliwahi kujiondoa CCM miaka ya 1990 kisha akawa mpaka Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Aliporejea CCM alisema maneno mengi ya hovyo kuhusu vyama vya upinzani na Chadema. Leo amerejea Chadema kwa sababu ya Lowassa. Unaweza kurejea misimamo ya Khamis Mgeja, halafu fikiria tu kuwa sasa ni mwanachama wa Chadema.
Lowassa ni superpower! CCM yenyewe imesinyaa, hayo matokeo ya Slaa na Lipumba ni rashasharasha tu. Mgeuko wa akina Mgana Msindai kukimbilia Chadema ni kijiupepo tu! Kimbunga chenyewe ni jinsi ambavyo CCM imekuwa kimya, Lowassa anatamba.
Tusipime msafara mdogo wa Dk. John Magufuli kwenda kuchukua fomu kwa ule wa Lowassa. Ambako tunatakiwa kuuona ukubwa wa Lowassa ni namna ambavyo vyombo vya habari vinavyosema naye katika sura chanya kuliko mgombea wa CCM.
Ipo hoja kuwa Lowassa amenunua vyombo vya habari, swali ni je, Lowassa ana pesa kuliko CCM? Tunaambiwa kuwa hata Chadema na Ukawa amewanunua, tujiulize, kama kweli hilo limewezekana, hatuoni kama huyo mtu ana uwezo mkubwa kuliko sayari hii?
Magazeti yaliyokuwa yanamuandama kwa kashfa za ufisadi, leo hii yanampamba vizuri. Waandishi waliowahi kutunukiwa tuzo kwa eti ni hodari wa kuchimbua madudu ya Lowassa, kwa sasa ndiyo watengeneza mapambio ya Lowassa. Ukiona hili ni la kawaida shauri yako!
Ni Lowassa peke yake ameweza kumzidi maarifa Shetani. Inajulikana binadamu ni watenda dhambi sana. Na kwa mujibu wa maandiko maratakatifu ya vitabu vyote, Torati, Zaburi, Injili na Kuran, anayeanguka dhambini anakuwa amepita njia ya Shetani.
Pamoja na binadamu kushawishiwa na Shetani kisha kutenda dhambi, haijawahi kutokea binadamu kumsema vizuri Shetani. Mtu anaweza kukutwa kitandani na mume au mke wa mtu lakini katika kujitetea, atamsema Shetani kuwa chanzo cha dhambi alizotenda.
Binadamu anaweza kucheza kamari kisha akamuomba Mungu amsaidie apate ushindi. Akishindwa na kuliwa fedha, papo hapo kibao kinageuka, anamlaani Shetani kwamba ndiye aliyemshawishi kucheza kamari ambayo ni haramu mbele ya Mungu.
Haijawahi kutokea binadamu kumsema vizuri Shetani na haitakuja kutokea. Binadamu akizaliwa, majina ya mwanzomwanzo kuyakamata mojawapo ni la Shetani, kwamba ni jitu baya. Tunaambiwa Shetani alikuwa malaika, tena ni ana sura nzuri (handsome) lakini michoro kuhusu Shetani ni ya kutisha.
Haitakuja kutokea binadamu amchore Shetani kwa sura na umbile zuri. Jambazi anavamia, anaua na kupora pesa lakini baada ya wizi hapigi goti na kumshukuru Shetani kwa kumpa maarifa ya ujambazi. Mbakaji anapokamilisha ushetani wake, hatamshukuru Shetani, badala yake atamlaani.
Lowassa ameweza kuwageuza waliomwita Shetani, sasa ndiyo wanaompamba kwamba ni malaika. Shetani anahitaji kukutana na Lowassa ili ampe maarifa. Kama imewezekana kwa Freema Mbowe na Tundu Lissu, watu wenye misimamo mikali. Kuna kitu cha kujifunza hapa!
Hapa inabidi Shetani mwenyewe aache ubishi, kila siku yupo kwenye maisha ya kawaida ya binadamu, anashirikiana nao kutenda dhambi lakini baada ya matukio na matokeo, huwa hawawi pamoja. Inawezekana Lowassa akamsaidia Shetani maarifa, jinsi ya kumgeuza anayekusema vibaya leo, kesho akuseme vizuri na kukushabikia.
Ninapowaza jinsi Lowassa alivyomzidi maarifa Shetani, nakosa namna ya kumlinganisha na CCM. Sishangai kuona siku Magufuli alipokwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye vyombo vya habari halikuwa jambo la kushtua. Lowassa zamu yake ilipowadia, ikawa mtikisiko wa Jiji la Dar es Salaam.
Labda swali la kujiuliza ni hili; Lowassa amepata wapi maarifa ya wageuza waliomwita Shetani, leo wamnadi kuwa ni malaika? Nguvu za kuishinda CCM kushawishi vyombo vya habari kumuandika vizuri kila siku anazipata wapi?
Nguvu za kuwafanya akina Mbowe kumuona Slaa siyo lolote wala chochote siyo ndogo. Zinahitaji kuhojiwa! Zinapatikana wapi? Ni Lowassa mwenyewe peke yake? Msuli gani umetumika kuwafanya Cuf wamuone Lipumba si mali kitu tena, wakati walipata kumtukuza kama ‘Mungu-Mtu' wao?
Hiki kimbunga chake kinachotawala vyombo vya habari, vikiwemo vile ambavyo viliwahi kuwa adui yake namba moja, kina msaada wa nani? Waandishi waliotangaza kuwa wanawindwa wauawe na Lowassa, leo hii ndiyo maswahiba wake. Haya maarifa ya Lowassa siyo tu yanapaswa kuigwa na Shetani, hata Marekani.
Pengine siku zijazo Marekani wakishafanya mazungumzo na Lowassa, wataweza kuwafanya Wairan wawapende. Labda Marekani itawafanya Wapalestina, Walebanon, Waafghanistan, Wairaq na wengineo kuacha ugaidi na kuanza kuwa watetezi wa taifa hilo kubwa duniani.
Wanaompinga, wakati wanatoa hoja hasi dhidi ya Lowassa, lazima wawe wanakiri kuwa huyu mtu ni superpower, ana uwezo mkubwa wa kuyafanya yasiyowezekana yawezekane kirahisi kabisa. Kwa nini Magufuli siyo kipaumbele cha vyombo vya habari kwa sasa? Je, CCM haina uwezo wa kushawishi? Ameizidi maarifa CCM.
Wanaomshabikia, siyo kushangilia tu, ni vizuri kujiuliza nguvu alizonazo zinatoka wapi? Tusipuuze hoja kuwa amewekeana ahadi na watu kuhusu rasilimali za nchi yetu. Tuwaze mmojammoja, ni biashara gani inapigiwa chapuo baada ya Lowassa kuingia Ikulu?
Binafsi nawaza huu mkumbo (bandwagon) unachagizwa na nini? Sasa imekuwa fasheni kumshabikia Lowassa. Wale ambao siyo timu Lowassa wanaonekana hawaendi na wakati. Mwaka 1997, Charles Taylor ndiye alikuwa bandwagon wa Liberia. Watu hawakuambiwa kitu!
Taylor alimwaga fedha kwa vijana katika Uchaguzi Mkuu wa Liberia 1997. Pamoja na makatazo mbalimbali, watu hawakuambiwa kitu. Mwisho, Taylor alishinda kwa kishindo. Baada ya ushindi, Waliberia wanajuta mpaka leo. Tuwe makini tunapoutazama Uchaguzi Mkuu 2015.
by Luqman Maloto